Mpenzi wake amechukua fani ya Engineer, na anaogopa atakuwa mchafu

Yuko Civil mkuu, ebu mwaga nondozi za uzoefu hapo
Mkuu civil ni nzuri kupita kiasi haina kuchafuka,,akiwa na ordinary diploma ana soko pana la ajira kama foreman kusimamia barabara,,majengo,,na pia kufanya kazi idara za maji na vituo vya kupimia uzito wa magari kote hakuna kuchafuka na mishahara ni mizuri,,akiwa na degree ndo ana wigo mpana zaidi.Civil ni nzuri na inakupa uwezo wa kufanya kazi nyingi za maana.
 
Mwambie aache uoga kama maelewano yapo kati yao waendelee na relation yao.
 
apo alipokua nae kipindi yuko form 5 alikua anasoma pcm au pcb, anasoma engineer kozi gani, mbona kozi za maingineer pia zina sector ambazo unakaa ofisini. uyo rafiki yako itakua ana matatizo binafsi
 
Yuko Civil mkuu, ebu mwaga nondozi za uzoefu hapo
civil ndio kua mchafu? unafikiri atatoka na nguo za kazi tangia nyumbani. hata kama engineer wa civil humkuti site 24 hours. pia ana nafasi ya kua structural engineer na kutulia ofisini tu
 
Yan huyo kumbe hajui maengeneer wanakula viyoyoz maofisin mweh na kuvaa suti....hao madaktar asithubutu ahahaha baba ni daktar bingwa wa upasuaji
Mchana busy hospital usiku umelala kidogo gari la hosp hili hapa "mzee unahitajika hosp kuna operation" mara polisi wanakutaka wewe kwa post nini sijui ahahahaha sie tunamwonaga jumapil tena kwa machale sana
Aoe msichana asilete visingizio labda kama amemchoka anatafuta sababu
Ila prof Ya mtu sio kigezo cha uchafu aache kabisa ....hajaona wauza mkaa smart nini huyo
 
Wandugu ebu munipe njia nimtie moyo huyu rafiki yangu hajitambui wala hana raha kabisaa.

Rafiki yangu huyu alichumbia mchumba tangu huyo mchumba akiwa form five, sasa huyo mchumba anasoma masomo ya Engeneer na anaona kama amepoteza matarajiao yake.

Mara ya kwanza alijua mchumba wake atasomea udakatari or phamacy. Ila kwa sasa ndio hivyo anasoma Engeneer na nimejitahidi sana kumshauri lakini hataki kusikia japo analia sana kwa vile anampenda sana binti hakuwa na mpango wa kumuacha alikini sasa ndo ivo tena.

Hoja yake iko sehemu hii.
1. Mke Engeneer hawezi kuwa nadhifu hata siku moja.
2. Atamuacha na kusafiri kila mara huku yeye akilea watoto
3.Hataweza kushiriki kikamilifu katika familia kwa ubize wa kazi zake

Sasa wanajamvi wazoefu ebu munipe nondozi za uzoefu nikamshauri huyu rafiki kabla hajafika mbali .

Angalizo, ushauri huo usije ukaniumbua mimi baadae.

Karibuni.
poor perception hiyo, mwambie abadilike.
 
huyu jamaahajielewi kabisa,..professional na uchavu vina relate vipi.....mwambie mzugaji hana nia
 
Yuuu tena aje awe anatembea kwa magoti kabisa aombe radhi,engineer it great and wanderfull professional in the world,uchafu ni Tabia ya m2 binafsi,na pia huyo mpenzi inabidi aunde mazingira ili abadilike!!take care cc siyo wasociologist,teacher even nursing
 
Marekebisho

Ni Engineer sio engeneer
Anasoma engineering (uhandisi) na sio anasoma engeneer/engineer (mhandisi).
Mchango wangu ndio huo mengine jiongezeni wenyewe.
 
Wandugu ebu munipe njia nimtie moyo huyu rafiki yangu hajitambui wala hana raha kabisaa.

Rafiki yangu huyu alichumbia mchumba tangu huyo mchumba akiwa form five, sasa huyo mchumba anasoma masomo ya Engeneer na anaona kama amepoteza matarajiao yake.

Mara ya kwanza alijua mchumba wake atasomea udakatari or phamacy. Ila kwa sasa ndio hivyo anasoma Engeneer na nimejitahidi sana kumshauri lakini hataki kusikia japo analia sana kwa vile anampenda sana binti hakuwa na mpango wa kumuacha alikini sasa ndo ivo tena.

Hoja yake iko sehemu hii.
1. Mke Engeneer hawezi kuwa nadhifu hata siku moja.
2. Atamuacha na kusafiri kila mara huku yeye akilea watoto
3.Hataweza kushiriki kikamilifu katika familia kwa ubize wa kazi zake

Sasa wanajamvi wazoefu ebu munipe nondozi za uzoefu nikamshauri huyu rafiki kabla hajafika mbali .

Angalizo, ushauri huo usije ukaniumbua mimi baadae.

Karibuni.
Huyo jamaa kama hamtak huyo manz amwambie sio kuleta sababu zisizo na mashiko
 
THE FACT IS... HUYO HAJUI ENGINEERING IPOJE... ANAWATAZA MAFUNDI WA MITAANI NDO ANADHANI NI MAINJINIA....
1. Kusafiri hakuna fani maalumu.... Kusafiri ni hitaji ya kazi husika kwa wakati huo.... Inawezekana kawaona wahandisi wa minala anadhani wandisi wote wapo hivyo....
2. Wahudumu wa ndani ya ndege anawaweka kwenye kundi gani..??? Ni wasafi halafu wanasafiri..
3. Haya wa usalama wa taifa anadhani wamesoma kozi zipi.. Wanasafiri au la..??
4. Haya manesi wanaokwenda night na kusafiri na wagonjwa wanapopew rufaa anadhani ni wahandisi..??
5. Marubani je..??
6. Madaktari bingwa leo wapo huku, kesho kule na mara hukoo.. nao ni wahandisi..???\
7 Haya, wachungaji anaowaona kwenye mahubiri nchi mbalimbali wakiwa nje ya nchi zao nao ni wahandisi..??
8. Haya, Anakumbuka makatibu tarafa walivyokuwa wanahama leo hapa kesho pale ..??? Nao ni wahandisi..??
9. Hao wanaomsafirisha kwa basi, treni, meli etc nao je..???

AKITAKA MCHUMBA WAKE ASISAFIRI... AKIMALIZA AMWANZISHIE KAMPUNI AMBAYO HAITAJIHUSHA NA MASUALA YANAYOHITAJI KUSAFIRI... MY GOD... HIVI IPO HIYO KWELI..???

UCHUMBA MWINGINE UNA MASHERTI YA KUTAFUTIANA KUACHA KUSOMA TU.. mxshieewwxxxx
 
mwambie aache kuwa mwoga, uchafu ni tabia ya mtu mwenyewe na kama ameweza kukaa nae mda wote huo tangu a-level nadhani atakuwa anajua tabia za mwenzake. Mzee ni mhandisi wa majengo alisoma civil eng moja kati ya vitu nnavyo kumbuka ni kwamba tangu nakua mzee alikuwa na life flani la peke yake peke yake. Kwanza sikumbuki mara ya mwisho kumuona kavaa suruali ya kitambaa na viatu vyeusi
Yeye ni mtu wa raba na sendoz havai jeans ila kuna suruali flani zina kitambaa kigumu cha material ya jeans hizi tuzionazo zimening'nizwa madukani zenye rangi tofauti tofauti kama brown, black, green na nakadhalika. Mwanzoni nilikuwa nashangaa life style ya mzee ila ss hv nimeanza kuielewa na kuikubali maana nami tangu nimemaliza sekondari suruali za vitambaa na viatu nimekuwa navipiga vita sana. Nakumbuka kuna siku sikumnyooshea mzee suruali zake na umeme ulikatika, kesho akavaa moja ya bukta zake na akaenda job fresh na jioni akarudi kiroho safi. Sema ni mtu ambae hapendi kazi za kukaa sehemu moja naona anapenda kushinda site kugombana na mafundi kuhakikisha kazi zake zinaenda sawa. Mda mwingine naona kama nimeanza kuiga life yake hasa kwa upande wa mavazi, mda mwingine navaaga nguo naenda job huku nyuma watu wananishangaa huwa nasemaga nguo ambayo naona mi imenifaa siku hiyo ndo inavaliwa kiukweli sinaga time ya kuchagua nguo yeyote iliyombele yangu ndo inavaliwa. Wakuu nimeona bora niwajuze maisha yetu yalivyo, najua tuko tofauti na kuna wengine wananyonga tai na kwenda kwenye madaraja kusimamia kazi zao ila sie wengine tuko kawaida tu.
 
Huyo jamaa yako hana mapenzi/nia ya kumuoa huyo mwanamke.
Aende pwani akapewe nke.
 
Back
Top Bottom