4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 7,021
- 8,161
Chunguzeni kama walitoka kwenye chama chake ukweli ujulikane kama ni upande usiojulikana mambo yawe wazi , daily lalamika mambo ya kijinga , vyombo si vipo acheni tumia akili zenu vibayaAkiwa Singida katika mikutano yake hivi Juzi, Mh. Tundu Lissu alidai tena kwamba, anawindwa na watu wasiojulikana kama ilivyokuwa kipindi cha miaka ya 2016, 2017 pindi akiwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya watu wa TANZANIA
Ilikuwa ni kama mchezo hivi, mara masikio ya Watanzania na duniani kote, ikasikiaka habari mbaya za kushambuliwa kwa risasi nyingi mh.Tundu lissu na hatimaye kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu
Ni miaka kadhaa sasa imepita tangu tukio hilo baya kabisa na la kihistoria katika nchi yetu tangu kuwepo kwa vyama vingi nchini mtu maarufu na kiongozi katika nchi kushambuliwa kwa risasi tena ni mchana kweupe!
Mungu asaudie isijirudie tena ili tuendelee kuishi kwa amani, upendo na mshikamano
Kwa kuwa wapo Watanzani wengi ambao walioamini kwamba, mashambulizi hayo pengine yalitokana na amri ya Rais wa aliyekuwepo kipindi hiko hayati John Pombe Magufuli na wengine walitofautiana na uvumi huo huku wao wakiamini kuwa, huo ni mchezo tu wa Ndani kwa ndani wa wana Chadema, huku wakirejelea mambo ambayo yamewahi kujitokeza katika chama hiko na kutolea mfano wa wengi waliowahi kukumbwa na kadhia hizo ndani ya Chadema, mfano, Chacha Wangwe, kina Zitto, Sumaye na wengine wengi na hao wato wakitoa shutuma kwa kiongozi wao mkuu wa chama
Na sasa kuna kinachoendelea ndani ya Chama hiki kikubwa kabisa cha upinzani nchini, Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kuna makundi mawili sasa yakivutana na kutwishana lawama za upande mmoja wamepokea mlungula wa pesa za CCM ili kuvuruga uchaguzi wa ndani na kiongozi mmoja kwenda mbali zaidi kuhoji dhidi ya ujio wa Mh.Samia katika maadhimisho ya siku ya wanawake kichama
Mambo haya yameendelea na kuibua hisia kali ndani ya Chama, ni ukweli ulio bayana kwamba, Chadema hawako pamoja, yapo makundi mawili, moja likiwa upande wa mwenyekiti wa Chama (MBOWE) na la pili upande wa makamu Mwenyekiti (TUNDU LISSU)
Kunapotokea madai ya mmoja kuwindwa na watu wasiojylikana, wakati huo huo ndani ya chama hakuna umoja na maelewano hayapo, wale watu waliokuwa wakiamini kwamba, Kushambuliwa kwa lisasi mh Tundu Lissu kulitokana na Chadema, watakoleza habari hizi na kuziamini zaidi
Chonde Chonde, Chadema kaeni myamalize, siku zote adui hutumia mlango wa udhaifu na kushambuliana nyinyi kwa nyinyi ili awamalize na msijue kwa wepesi
UMOJA NI NGUZO YA USHINDI
INAWEZEKANA TENA KWA CHADEMA KUWA WAMOJA!
Pia soma