Mother's Day: Leo ni siku ya Wakina Mama Duniani, umemkumbukaje mama yako?

Happy Mother's day,mbarikiwe wanawake wote mliojitolea kwa moyo wote kutuleta duniani sisi wanaume
de40db7c0fea29fce3c85fb54ebec6ca.jpg
 
Happy Mothers Day my beautiful Mother ROSE!
You are absolutely right buddy! No any other woman, believe me, can be more beautiful than your mother! Otherwise your father would have gone for that other woman and, most likely their combination of genes wouldn't have coalesced to become YOU!
 
Kwa kunilie na hadi kufikia hapa nilipo sipati maneno mazuri ya kukushukuru.

Tulizaliwa wengi katika familia, ukaweka upendo sawa kati yetu kwako hakuwepo aliye bora Zaidi.

Lakini kamwe hukuipenda tabia ya ndugu zangu kuniita mjinga kwa kuwa tu sikuwa na uwezo mzuri shule ya msingi.

Wewe tu ndo ulikuwa ukinipa moyo kwa kila namna.
Ulilia machozi siku nilipopigwa sana na Baba baada ya riport yangu ya darasa la tatu mwalimu alipotoa maoni kuwa Mimi ni kichwa Mani. Lakini kamwe hukunikatia tamaa hata kidogo.

Wale wenye akili hakuna hata mmoja aliyefika hata kidato cha tano.
Lakini Mimi niliyekuwa kichwa maji ndiye niliyefika chuo.
Na leo nimekuwa Yusuph wa familia.

Nafasi yako Mama inabaki kuwa ya pekee tu maishani mwangu.
Mungu akupe maisha marefu, furaha na amani vifurike moyoni mwako.

Happy Mothers Day.
 
Happy mother's day my darling mom mungu akupumzishe mahala pepa...happy mothers day my sister yo my 2nd mom
 
Kwa kunilie na hadi kufikia hapa nilipo sipati maneno mazuri ya kukushukuru.

Tulizaliwa wengi katika familia, ukaweka upendo sawa kati yetu kwako hakuwepo aliye bora Zaidi.

Lakini kamwe hukuipenda tabia ya ndugu zangu kuniita mjinga kwa kuwa tu sikuwa na uwezo mzuri shule ya msingi.

Wewe tu ndo ulikuwa ukinipa moyo kwa kila namna.
Ulilia machozi siku nilipopigwa sana na Baba baada ya riport yangu ya darasa la tatu mwalimu alipotoa maoni kuwa Mimi ni kichwa Mani. Lakini kamwe hukunikatia tamaa hata kidogo.

Wale wenye akili hakuna hata mmoja aliyefika hata kidato cha tano.
Lakini Mimi niliyekuwa kichwa maji ndiye niliyefika chuo.
Na leo nimekuwa Yusuph wa familia.

Nafasi yako Mama inabaki kuwa ya pekee tu maishani mwangu.
Mungu akupe maisha marefu, furaha na amani vifurike moyoni mwako.

Happy Mothers Day.
So touching and impressive remarks! There can hardly be better remarks than these! Asante mkuu. Umeandika kwa hisia mno. Mungu ambariki mama yako mzazi ambaye hata hivyo hukupata ujasiri wa kumtaja kwa jina.
 
Happy Mothers Day The ALMIGHTY SUPREME CREATOR OF THE UNIVERSE!
Amen Ra
Leo ni siku ambayo duniani kote tunawakumbuka na kuwaenzi mama zetu. Sote tumezaliwa na mama zetu. Hata kama wapo wachache ambao kwa bahati mbaya, kwa sababu hii au ile hawakuwahi kuonja upendo na mahangaiko ya mama zao, lakini ukweli wa jumla ni kwamba yako mambo ambayo bila mama zetu yasingefanyika, kubwa ktk hayo ni kutubeba tumboni hadi tukafikia umri wa kuwa tayari kuwa hai bila kuwa matumboni mwao.

Malezi yanaweza kuyafanywa na mtu yeyote mwenye mapenzi mema, lakini “role” ya mama (mzazi au mlezi) kwa mtoto ni “indisputable”. Sisi tuliozaliwa na kukulia vijini nyakati hizoo hili ni kweli Zaidi. Naomba wana JF wote muungane nami:

1. Kumpongeza mama yangu mzazi Dorotea na mama zetu wazazi na walezi wote
2. Kuwaombea pumziko la Amani mama waliotangulia
3. Kuwatia moyo mabinti wanaoogopa majukumu ya kuwa “mama”
4. Kuwasamehe akina mama waliofanya makossa makubwa ya umama kwa watoto wao
5. Kulaani vitendo vilivyo kinyume na hurka sahihi ya umama kama utoaji mimba, kutupa na kutelekeza watoto, nk.
6. Kulaani akina baba wanaowatesa, kuwatumikisha na kuwatelekeza mama wa watoto wao
7. Kulaani watoto waliowatelekeza wazazi wao, hasa mama zao
8. Kulaani serikali zote duniani zisizoweka mipango sahihi kwa ajili ya afya na ustawi wa mama na mtoto, na
9. Kila mtu ampongeze mama yake hapa kwa kumtaja jina
Happy Mother’s Day!
NANI KAMA MAMA?
View attachment 509075

View attachment 509076

Wakuu samahani, nimeshindwa ku-attach wimbo/video wa Christian Bella Ft Ommy: Nani Kama Mama. Aliye nao ktk file format ndogo atusaidie, Plz!
 
Mungu awabariki na kuwapa hekima,busara na upendo zaidi akina MAMA wote,waishi vema.
Nakupenda sana MAMA na waMAMA wengine wote duniani.
[HASHTAG]#happymothersday[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom