Moshi Vijijini acheni siasa za kuchafuana, muda bado

james mwakyusa

New Member
Feb 19, 2024
2
1
Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 jimbo la Moshi vijijini lilimpata mbunge wake,Profesa Patrick Ndakidemi kupitia chama cha mapinduzi(CCM)baada ya kuwashinda wapizani wake akiwamo mpinzani wake mkubwa kwenye kura za maoni,Morris Makoi.

Falsafa ya chama cha mapinduzi ni kwamba,baada ya mgombea kupatikana kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama,makundi yote huwa yanavunjwwa na wagombea wote kwenye kura za maoni kuungana kumsapoti aliyeshinda.

Falsafa hii imekuwa tofauti sana katika jimbo la moshi vijijini hasa kwa waliaongushwa kwenye kura za maoni ndani ya chama,Morris Makoi na kundi lake wameanzisha harakati za makusudi kumchafua Ndakidemi,wengine wakidiriki kusema wazi kuwa hawatompa ushirikiano,hii ni hujuma kwa chama cha mapinduzi na kwa wananchi pia.

Waswahili wanasema asiyekubali kushindwa si mshindani,Morris Makoi na kundi lake wameonyesha kuwa si washindani wa kweli,ameamua kuunda kundi lake la madiwani na watu wengine ndani ya chama kuhakikisha anafifisha mikakati ya kada mwenzake kutekeleza majukumu yake.

kwa nini Makoi na si mwigine?,inajulikana walioingia kwenye kura za maoni ni wengi na baadaye akapatikana mshindi lakini mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Moshi ameonyesha dhahiri harakati zake za kumpinga kada mwenzake.

hatua hii inaswamisha juhudi za mbunge kuwahudumia wanannchi na licha ya maonyo kutoka kwa viongozi wa ccm wilaya na mkoa,bado harakati hizi ovu zinaendelea na hivi karibuni makoi alialika madiwani wanaotoka upande wa Moshi vijijini kwa ajili ya chakula na kuwawezesha posho wakati wa kurejea makwao.

kama alikuwa na nia ya kuwaalika madiwani wote kwa nini wale wa Vunjo ambao wanaunda baraza la madiwani wa halmashauri ya Moshi asiwajumuishe kwenye hicho chakula?,kwa nini tusiamini huu ni mpango mkakati kuelekea uchanguzi mkuu ujao?

Makoi anashindwa kuelewa kuwa kabla hujamchafua mwenzako hebu jitafakari wewe ni msafi kwa kiwango gani,huna makando kando na je na wenzako waanze kufukunyua mabaya ya kwako,tutafika?

Zipo taarifa za chini chini kwamba Makoi una kesi ya uhujumu uchum(ECO CASE) namba 1/2023 katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi Jijini Tanga kupitia kampuni yako ya Baraka Printers,wananchi wa moshi nao watataka kujua uliimalizaje?,ulilipa pesa ambazo ulipata isivyo sahihi au?,

Moshi vijijini acheni siasa za kuachafuana hakuna aliyemkamilifu,

nawatakia mchana mwema,nitarudi hapa kesho
 
Uchagani tuongee biashara siasa za kijani wapi na wapi??
alafu moshi ni Chadema Sasa hayo mambo ya pwani(SISIEMU) mmeanza lini?? Fisiemu Waachieni wacheza singeli
 
Bungeni imekuwa ni sehemu ya watu kwenda kupiga pesa sio kwenda kusemea kero za wananchi tena.
 
Mbunge ameona uchaguzi unakaribia anatafuta sababu za kushindwa kukamilisha ahadi kwa wananchi. Unakwamishwaje kuteleleza kazi zako na mtu Yuko mtaani?
 
Hilo jimbo anakwenda kulichukua Lucy Owenya, waambie wenzako waache hizo vurugu zao kwani hakuna yeyote ukiwemo wewe atakayepata chochote hapo come 2025.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Zipo taarifa za chini chini kwamba Makoi una kesi ya uhujumu uchum(ECO CASE) namba 1/2023 katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi Jijini Tanga kupitia kampuni yako ya Baraka Printers,wananchi wa moshi nao watataka kujua uliimalizaje?,ulilipa pesa ambazo ulipata isivyo sahihi au?,
Hii kesi hata mie naijua vyema na inasemekana alihonga sana mahakimu kuua kesi hii!
Si hivyo tu ana makandokando mengi hata ktk kiti alichokalia kwa sasa, asipende vita ya mawe wakati anaishi 'nyumba ya vioo'
 
Hii kesi hata mie naijua vyema na inasemekana alihonga sana mahakimu kuua kesi hii!
Si hivyo tu ana makandokando mengi hata ktk kiti alichokalia kwa sasa, asipende vita ya mawe wakati anaishi 'nyumba ya vioo'
Wabunge wengi waliopitiskwq na CCM wala hawakuwa chaguo la wajumbe wala wananchi. Aacha malalamiko na pia angangamale kulipigania jimbo lake.

Watia nia wengine wakianza kujipitisha jimboni hiyo ni hala kwao. Hiyo nafasi pia inapaswa kuwa iwepo katika kofia ya urais. Kwa kuwa aliyepo madarakani hajawahi kupishwa na vikao muhimu vya CCM ili aweze kugombea nafasi hiyo, isipokuwa JPM.

Madai ya kutaka kutoa fomu moja kwa aliyepo madarakani, ni kwenda kinyume na katiba yao wenyewe. Ni tamaa ya kikundi cha watu wachache ambao wanafaidika na udhaifu pamoja na fursa za kifisadi zilizopo katika utawala huu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom