Morogoro: Waziri wa Maji Jumaa Aweso awaumbua mamlaka ya maji Morogoro, tangu mwezi February hawajaweka dawa ya kutibu maji katika matenki yao

Nishapata majibu kwanini Moro Typhoid inaongoza vibaya mno
Hatari, waluguru wanafyatua kimba milimani kwenye vyanzo vya maji, mamlaka ya maji inasafirisha kuja majumbami kwa njia ya mabomba ya maji bila hata kuyatibu, ni kawaida kukutana na maji kama tope au hata yana majani 😂
 
Hii kwa kweli inashangaza, tangu mwezi February mwaka 2024, jamaa wanasambaza maji kwa wananchi yakiwa hayajatibiwa (treated).

Kwa hiyo kwa muda wote wananchi wamekuwa wakinywa maji yenye vimelea vya magonjwa.

Si ajabu mkoa wa Morogoro una maambukizi makubwa sana ya magonjwa ya matumbo, hasa amoeba, typhoid. Maji ni machafu, lakini bili za wananchi wanalipa.

Namshauri Waziri awape Ewura mamlaka ya kufanya ukaguzi wa maji walau kila wiki, kwa vipimo maalum, na taarifa iwe inawasilishwa wizarani na mkoani.

Haiwezekani serikali ipo, lakini miezi mitano watu wanakunywa maji machafu. Hizi mamlaka ziwe monitored, si kwenye kupeleka maji tu, bali kupeleka maji safi
Yaani kabisa mtu anaamini maji ya mamlaka za maji hapa Tanzania unaweza ukayanywa bila kuyachemsha..!! Really..!!??
 
Sometimes kwenye kuoga au kusafisha uso, yatapita tu hata kidogo mdomoni, au chai kama haijachemshwa vizuri, kachumbari, maji ya kunawa, au kama kikombe cha maji ya kunywa hakijakaushwa vizuri, sio lazima unywe
 
Hii kwa kweli inashangaza, tangu mwezi February mwaka 2024, jamaa wanasambaza maji kwa wananchi yakiwa hayajatibiwa (treated).

Kwa hiyo kwa muda wote wananchi wamekuwa wakinywa maji yenye vimelea vya magonjwa.

Si ajabu mkoa wa Morogoro una maambukizi makubwa sana ya magonjwa ya matumbo, hasa amoeba, typhoid. Maji ni machafu, lakini bili za wananchi wanalipa.

Namshauri Waziri awape Ewura mamlaka ya kufanya ukaguzi wa maji walau kila wiki, kwa vipimo maalum, na taarifa iwe inawasilishwa wizarani na mkoani.

Haiwezekani serikali ipo, lakini miezi mitano watu wanakunywa maji machafu. Hizi mamlaka ziwe monitored, si kwenye kupeleka maji tu, bali kupeleka maji safi
Halafu kwa mtindo huu hata ufukuze mawaziri kila siku ni kuwaonea tu, huku makatibu wakuu wakibaki!! Wafrika tuna laana ya asili!!
 
Back
Top Bottom