Elewa Hapo naongelea Acient asyrian empire,hii Ni Kati ya empire za mwanzo kabisa baada ya Sumeria, Akkadian,na Mesopotamia,
Mkuu hapa ndani ya hii Post yako kuna madini adimuElewa Hapo naongelea Acient asyrian empire,hii Ni Kati ya empire za mwanzo kabisa baada ya Sumeria, Akkadian,na Mesopotamia,
So kumbe it happen ,Adam Ni jina la ki Akkadian au asyrian,
Kwahiyo whoever wrote the story of Adam in Genesis could have gotten inspiration from Adam,the Asyrian king,
The same as whoever wrote the story of king Solomon did get insipiration from Asyrian king Shalmanesser,or the King David story,from Aram King Been hadad
umenishawish kwamba kwa kiasi fulani lakini ilikuwaje tena wakatokea waafrika na wazungu kuja kukutana mbona sisi hatukuwa na nyaraka zozote za kuwapa wao badala yake tumekuja kupokea kila kitu kwao mpaka cha kuamini.Historia ya mnara wa Babeli inaelezwa kwa undani kwenye biblia katika kitabu cha Mwanzo 11 katika mistari michache tu. Hii ni stori fupi tu ya mnara wa Babeli unaweza kusoma kwa undani katika mistari au maandiko hapo chini ili kujua zaidi juu ya Babeli na maana yake katika biblia.
Kizazi cha Nuhu kilikuwa kinaishi katika Mesopotamia ndani ya Babeli na kuchagua kuishi katika nchi ya Shina. Kizazi chao kikazidi kukuwa huku wakiwa wanaongea lugha moja wote. Muda ulivyozidi kwenda watu wa Babeli wakaaamua kujenga mnara mkubwa kama alama ya nchi yao na kujionesha kwa mataifa mengine ukuu wa nchi yao ya Babeli. Watu wa Babeli walitaka kujenga mnara ambao unaweza kufika mpaka mbinguni, ili wawe kama mungu na wasimuhitaji tena mungu kwenye maisha yao ndipo hapo wakaanza ujenzi wa mnara huo na kuuita mnara wa Babeli.
Babeli ni mji maarufu sana ndani ya Mesopotamia ambako kwa miaka ya sasa mji huu unapatikana maili 59 Iraq kusini magharibi mwa Baghdad ambao ni mji mkuu wa Iraq.
Jina hili linatokana na lugha ya ki-akkadian (Bav-ill) lenye maana mlango wa mungu 'Gate of God'.
Historia ya biblia inatuonesha maeneo mbalimbali ya mabadiliko ya dunia mfano Uumbaji, anguko na gharika la NUHU. Kwa kufuatilia mfululizo mzuri wa matukio ya kibiblia ambayo yalishawahi kutokea na ni ya kweli tunaweza tukaelewa asili ya maisha yetu na kuachana na mambo ya EVOLUTION OF MAN. Babeli ndiyo ulikuwa mwanzo wa mgawanyo wa mataifa na mkanganyko wa lugha ulimwenguni.
Baada ya Nuhu na familia yake kushuka kwenye safina katika milima ya Arafati, Mungu aliwaagiza waende kuzaana na kutawanyika mbele ya uso wa nchi. (\mwanzo9:1) , wao wakaamua kuishi Babeli nchi iliyokuwa chini ya Nimrodi (Mpinga kristo) ambapo hapo ndipo ujenzi wa mnara wa Babeli ulipoanzia. (Baadae tutaona ni kwanini Nimrodi alikuwa mpinga kristo). Mnara huu wa Babeli ndio uliokuja kuwa makutano ya kuabudia miungu na sio Mungu muumbaji.
KWANINI MUNGU ALIAMUA KUANGAMIZA BABELI?
Katika utawala wa Nimrodi, miaka mingi baada ya uumbaji kukamilika, Ndipo ujenzi wa mnara wa Babeli ulipoanza. Ikumbukwe mpaka muda huu nchi ilikuwa sehemu moja. Baada ya gharika kutokea na Nuhu na familia yake kusalimika, ulimwengu mzima ulikuwa sehemu moja kwa sababu dunia/nchi haikuwa na watu wengi na ndio maana Mungu alimwagiza Nuhu baada ya gharika kuisha kuwa waende wakaijaze nchi.
Hapo ndipo Nimrodi na wenzake walipoamua kujenga mnara mkubwa sana kwa malengo makubwa mawili.
1. Kujitafutia jina wao wenyewe juu ya nchi
2. Kufika mbinguni
Nimrodi akaanza kujenga mnara ambao ulikuwa mkubwa sana mpaka hapo mungu aliposhuka chini na kuamua kuuangamiza huo mnara kwa kuwachafulia lugha zao.
Mungu hakuiangamiza Babeli kwa sababu aliwaogopa wanadamu au labda aliona kuwa wanadamu wanaweza kufika mbinguni, hapana. Dunia sasa hivi ina maghorofa makubwa sana hata tunaona ndege zikienda hewani lakini hakuna ambayo imeshawahi kufika mbinguni ambako mungu yupo, kwa hiyo mungu hakuwahofia wanadamu kabisa ila kulikuwa na sababu za msingi zilizofanya mungu afanye vile.
Mungu hakupendezwa na kiburi na kutokutii kwa wanadamu. Ikumbukwe kuwa dhambii hii hii ya kiburi ndiyo kwanza ilimuangusha shetani kutoka mbingu mpaka nchi, pia dhambi hiyo hiyo ilimuangusha Adamu ndani ya Edeni na dhambi hiyo hiyo iliangusha Babeli kuu ya Nemrodi.
Watu wa Babeli walitaka wakae sehemu moja kinyume na matakwa ya mungu. Ikumbukwe mungu alimuagiza Nuhu waende wakatawanyike mbele ya uso wa nchi, lakini wao wakaamua kufanya kinyume na amri ya mungu ili wajitwalie utukufu wao wenyewe (KIBURI).
Dhambi kubwa iliyofanya mungu awachafulie usemi wao ilikuwa "Na tujifanyie jina wenyewe", Je wakati huo kulikuwa nchi ambayo walikuwa wanataka kushindana nayo? Je walitaka nani awasifu? Kulikuwa na nchi ya jirani? Ila walikuwa wanashindana na Mungu mwenyewe.
Nimrodi alikuwa na makundi matatu
1. Kundi la kwanza lilikuwa kwa ajiri ya kumuua mungu
2. Kundi la pili walikuwa na kazi ya kutengeneza mishalie kwa ajili ya kumuua mungu
3. Kundi la mwisho kwa ajiri ya ujenzi wa Babeli
Tembelea (skiba 2012) kwa mapitia .
Hapo ndipo utakapogundua kuwa Nimrodi alitaka kwenda kukaa kwenye kiti cha enzi cha mungu.
Hayo yote ndiyo yaliyomchukiza mungu na kuamua kuwachafulia usemi wao ili wapate kujifunza na kuwalazimisha kugawanyika mbele ya uso wa mungu
HII INAENDA SAMBAMBA KABISA NA ANGUKO LA SHETANI KWA KUTAKA KUWA KWENYE KITI CHA ENZI CHA MUNGU
View attachment 757831
Inahitaji iman kuielewa imani,na ushahid kuelewa sayansiKuna wakati biblia inaacha maswali mengi kuliko majibu. Ukiwa mtu wa facts lazima utaona kuna tatizo mahala!
Anyway, tusubiri majibu mkuu!
Hao walikuwa vidume hadi mungu mishale ikampata? Napendaga documentary za myth niliangalia aztec na zeus nk zinavutia mno
Hii huwa ni story au ukweli?Jengo la umoja wa Ulaya limejengwa kwa muundo huohuo wa Babeli. Na ktk viti vya bunge la Ulaya kiti namba 666 hakina mkaaji coz hajaja bado.
Mkuu walijenga GETI la kufika mbinguni ila sio mnara physical zaidi walijenga tu pyramid kubwa sana la kufanyia matambiko ndio ukaitwa mnara ila kazi yao kubwa ilikuwa kumfikia Mungu kiroho sio kimwili kama ingekuwa hivo ina maana NASA wangeshakuwa wamefika mbinguni kitambo sana kutumia rocket zao
heeeMkuu Hongera kwa kuleta mada nzuri hivi ila kitu kimoja tunakiruka ni kuwa Nimrod hakujenga mnara mkubwa kma tunavyofikiria kwamba ulitaka ufike mawinguni la hasha alitengeneza pyramid ya kawaida tu kama zile za misri na ushahidi huo upo sana tu ila kma angekuwa amejenga mrefu zaidi ya pale hata msingi au mabaki yangekuwepo ila mpaka leo hakuna ushahidi wa uwepo wa mnara mrefuuuuuuu hivo kma bulj khalifa!!
Ila kinachosisitizwa ni kuwa Nimrod akishirikiana na mwanaye Mardon walikuwa na nguvu za kiroho kubwa sana na katika wakati wao ndio walitawala koo zote za shem ham na japhet maana yeye ndio alikuwa mrithi wa VAZI la Adam ambalo yeyote anayelivaa ndio anakuwa na nguvu za ajabu za kurithi toka kwa Adam na yye alilipata kupitia babaye Ham ambaye aliliiba kutoka kwa Nuhu baada ya gharika .... Hivyo walitaka kufika mbinguni kiroho zaidi kwa kutengeneza GETI la kuwafanya waende mbinguni..... So kikubwa hapa ni kwamba walifanya matambiko makubwa sana na kutumia sayansi ya hali ya juu ya kutengeneza GETI litakalowafanya wafike mbinguni na kumuua huyo Mungu na ndio maana geti lilipoanza kutokea walirusha mishale ambayo ilirudi na damu!!! na ndio Mungu hapo hapo akashuka na kuwatawanya ili wasiendelee na nia yao ya kufika mbinguni.
Hivyo tunapowaza mnara tuwaze kuwa walijenga kiroho ila kimwili ulikuwa mnara mkubwa ila wa kawaida tu kma ile tunayoona Misri au Azteca ila kikubwa hapa ni MATAMBIKO na SAYANSI waliyotumia ndio ilimshtua Mungu hadi akaona wana NIA (sio uwezo) wa kumfikia!!! Akaona awatawanye
Shukrani kwa mada nzuri mkuu
Roho yako baada ya wewe kujifia itapata shida na adha kubwa sana milele.Mungu hayupo simple kama nimrodi alivyofikiri.. Ila hii historia aliipokea nani?