TANZIA Mmiliki wa baa maarufu Magomeni, Hussein Macheni ameaga dunia ghafla nyumbani kwake

Leo ndio nmejua kwanini huyu D alikua anatoa elimu ya UKIMWI kwa nguvu sana, kumbe mambo yalianzia kwa macheni
Kwanini tunakumbushana vifo tukiwa usingizini?

Imenibidi nidamke nipige push ups mbili tatu ndo nirudi kwa bed.

Ziraili hatabiriki...
 
Papa Macheni, mzee wa madini, kijana wa da'salam.

Lala salama boss.
Mmiliki wa baa maarufu ya Macheni iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Hussein Macheni amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Magomeni.

HM.jpg


Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba Macheni alianguka ghafla majira ya saa 3 asubuhi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo iligundulika kuwa tayari amefariki.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Muhimbili kusubiri taratibu nyingine. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN.

Chanzo : Global Publishers
a
 
Back
Top Bottom