Mmachinga kaniuzia kanyanga,nimfanyeje?

Alikuuzia sh ngapi? Pale unaponunua kitu cha bei rahisi ambayo ni below the market price inabidi ujiandae kwa vyote. Kisheria huna la kumfanya maana sheria inaonya, 'buyer be ware'!
Isitoshe hajapewa hata risiti.....wanakimbia kulipa kodi kama angeenda dukani akapewa bidhaa narisiti yake wala hii hoja isingeletwa humu
 
Acheni shortcut jamani siku nyingine mtapigwa vitu vyenye thamani kubwa kuliko hicho cha elfu 40... siku hizi machinga ni wahuni sana sio watu wa kuaminika hata kidogo kwani watakuletea kitu chenye thaman kubwa watakuuzia cheap ukijua umepata kumbe wamekuingiza mjini BTW pole sana ndugu yangu
 
Hawa chinga wanajua wanachofanya. Kutetea ujinga si jambo. Licha ya kuamini kuwa wanajitambua ili kupunguza maumivu assume imeibiwa. But in reality we got to fight this habit. Serikali imeshindwa, sisi tusishindwe. Njia nzuri ambayo mie huitumia huwa nawaambia naomba ile fake. Hapo utawajua na utaweza kupata original, ingawa ni original ya kibongo.
 
Alikuja ofisini kwangu akanitangazia biashara yake ya vitu mbalimbali ikiwemo ya power bank. Kwa kweli nilikuwa na mpango huo ndipo nilipomuagiza aniletee power bank yenye uwezo mkubwa kwa ajili ya tablet yangu.

Nilipomkunbushia aniletee aliomba nimfuate alipo ndipo aliponikabidhi hiyo power bank ambayo baada ya kuichaji niliitumia kwa dakika 5 tu ikawa imeisha chaji. Nimempigia simu kumjulisha na akaahidi kuniletea nyingine lakini kama siku 2 hivi ameamua kuzima simu yake kabisaa.sasa najiuliza nimfanyeje nikimuona?

Watanzania inabidi tuwe wakweli na sio wababaishaji!
Pole mkuu. Hapo chukulia kama umetoa hela ta tuition vile. Maana kama hilo somo umelihifadhi na utaweza kulifanyia kazi hapo mbeleni basi hujapata hasara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom