Mliiua pareto kiwanda mkapeleka Rwanda, mkaua General Tyre kiwanda mkapeleka Kenya, halafu vijana mnataka wajiajiri!

mockers

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
12,806
35,229
Shame on you,

Kiwanda cha pareto pale mafinga mlikiua Kwa makusudi huku mkijua ukanda wa kuanzia kyela hadi njombe wanalima pareto na kiwanda kiliajiri vijana wa kitanzania wengi.

Mkaenda kuua kiwanda cha matairi ya magari General Tyre cha Arusha na mashine mkang' oa mkapeleka kenya.

Mnatoa ajira za vijana wenu Kwa makusudi halafu kesho mnaenda kuwaongopea vijana wajiajiri tena bila mfumo bora wa mitaji na elimu.

Hua nawafikiria sera zenu nashindwa kuwaelewa mnajali matumbo yenu na sio watoto wenu wa Kitanzania.

MNALAANA SANA NINYI
 
Kufa kwa viwanda hivyo kulitokana na kufeli kwa sera ya ujamaa uliokuwa ukitegemea kilimo. Baada ya bei ya mazao ya kilimo kuanguka katika soko la dunia, fedha za kuendesha viwanda hivyo ilikosekana na hiyvo kufa.
 
Mwanasiasa akikwambia ni usiku, toka nje ukahakikishe maana utakuta ni mchana
 
Kufa kwa viwanda hivyo kulitokana na kufeli kwa sera ya ujamaa uliokuwa ukitegemea kilimo. Baada ya bei ya mazao ya kilimo kuanguka katika soko la dunia, fedha za kuendesha viwanda hivyo ilikosekana na hiyvo kufa.
Na vilikopelekwa wao ilikuaje ? Unajua historia ya ubinafsishwaji wa viwanda ni sera yao iliyokuja kuokoa viwanda na walivigawa na vingine kuuzwa Kwa bei sawa na bure, china alikua na ujamaa, urusi alikua na ujamaa, vietnam alikuaena ujamaa wao mbona viwanda havikufa
 
Sera ya ubinafsishaji ilikuja baadae sana ambapo viwanda hivyo vilikuwa vimeshakufa na vilivyokuwepo vilikuwa vinapumulia mirija na vilivyobinafisishwa havikuleta matunda kwa sababu ya siasa uchwara.
-huko vilikoenda mfano kenya ilikuwa rahisi kiwanda kusurvive kwa sababu wakenya wana uzoefu wa kuendesha viwanda na sera yao ya ubebari.
-Urusi na China ni ukomunisti na sisi tulikuwa na esocialisti kwaio ni vitu viwili tofauti na vilevile mazingira na uwezo wa china na urusi ulikuwa tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom