Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,606
- 4,262
Umesahau kuwa akiongea mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa "mungu" ameongea?Katika muendelezo unaoashiria matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya wakuu wa wilaya nchini, mkuu wa Wilaya ya Njombe mama Msafiria amemuweka ndani mwenyekiti wa mtaa wa Buguruni iliyo katika wilaya hiyo baada ya Mabishano yaliyotokea baina yao.
Mabishano hayo yalitokea baada ya mwenyekiti wa mtaa kuhoji uhalali wa mkuu wa wilaya kushinikiza, Mwenyekiti huyo ang'olewe katika kiti hicho wakati bado kuna kesi mahakamani. Kuwekwa ndani kwa Mwenyekiti huyo kuliambatana na kunaswa kibao.
Siku hizi imekuwa hali ya kawaida ya Wakuu wa wilaya kutumia mabavu pale wanaposhindwa hoja au kubanwa.
Kimsingi hakuna tishio lolote la amani na usalama lililosababishwa na Mwenyekiti huyo wa mtaa aliyewekwa ndani masaa 48
Ni muhimi kwa Wizara yenye dhamana Na TAMISEMI ikawa makini na viongozi wa aina hii, wanaonea watu nawanasababisha hasira ya wananchi dhidi ya serikali yao. Hili tukio la mama msafiri lichunguzwe na hatua stahiki dhidi yake zichukuliwe.
Ibara ya Tisa ya katiba inakataza aina yoyote ya uonevu katika nchi hii, kwa hiyo ni matumaini yangu haki itatendeka!
Chini nimeambatanisha Sauti ya Majibizano yaliyopelekea Mwenyekiti huyo kuwekwa ndani!
By the way, huyu ndiyo yule tuliyeambiwa alichapwa vibao na mama huyu au ni mwingine?