Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Capt.Mstaafu Chiku Galawa, kuokoa Milioni 250 Kila Mwaka Kwa Kutumia IPAD!.

Hiyo ni bajeti iliyopitishwa kununua makatasi. Ikapigwa panga ikanunulia Ipads sasa makaratasi basi.
Paskali
katika harimashauri zinazo kimbiza kifisadi mbozi ni moja wapo : had former pm mizengo aliwakatalia zawadi yao
wanaweza wakabana lakini fungu wakaliamishia kweenye tumbo la wengine
 
Asante kwa kumalizia. Amekuwa mpole kama amemwagiwa maji baridi. Ni bora angekaa kimya kuliko kuleta habari ambayo ni ya kawaida na isiyo na mjadala. Anyway, tumempoteza huyo.
Sio lazima kila habari iwe ni mjadala, nyingine ni just an info pack

Paskali
 
Wananchi wawe na ipad watume barua kwa email na kujibiwa kwa email muda wote wawe online.
Mkuu Babati, wanaotumia hizo karatasi za milion 250 sio wananchi bali viongozi, hivyo wanaopaswa kuwa na I pads kwa mujibu wa taratibu ni viongozi na sio wananchi, ila wewe kama mwananchi ukiwa na iPad yako its an added advantage kwa sababu issues zako zote za huduma zozote utazimaliza online.

Baadhi ya idara tayari ziko online ikiwemo TRA, TIC, Brela, EPZA, etc.

Paskali
 
Rim paper moja average ni tsh 10,000 so kwa 250ml ni matumiz ya rim paper elf 25 kwa mwaka mmh.
Nafikiri kuna vitu huvielewi. Hapo mtoa mada kaongelea mfano madiwani. Mkoa unakuta unazo halmashauri 6 kila halmashauri unalo baraza la madiwani.

Unapoongelea stationery expenditure usiongelee karatasi tu ndugu yangu hapo kuna Cartirage (wino), kuna kuna repair/maintenance za photocopy machines, nk
 
Kwa aina ya madiwani tulionao sijui kama hili litafanikiwa.
Wapo madiwani hawajui hata kusoma kwa ufasaha na kuandika vizuri.
Sifa za kukuwezesha kugombea udiwani ni za chini sana.
 
Kila mwaka? Kwani mkoa wenyewe una miaka mingapi? Siasa bwana!
 
hivi tafsiri ya kiswahili ya photocopy na printing ni makaratas?
Mkuu Bonny, karatasi ni karatasi, photocopy ni kudurufu na printing ni kuchapisha.
Huduma zote za kuchapisha, kudurufu na ku bind zinatumia karatasi.

Paskali
 
Mkuu Babati, wanaotumia hizo karatasi za milion 250 sio wananchi bali viongozi, hivyo wanaopaswa kuwa na I pads kwa mujibu wa taratibu ni viongozi na sio wananchi, ila wewe kama mwananchi ukiwa na iPad yako its an added advantage kwa sababu issues zako zote za huduma zozote utazimaliza online.

Baadhi ya idara tayari ziko online ikiwemo TRA, TIC, Brela, EPZA, etc.

Paskali
Okey asante kwa ufafanuzi mkuu
 
Mkuu Bonny, karatasi ni karatasi, photocopy ni kudurufu na printing ni kuchapisha.
Huduma zote za kuchapisha, kudurufu na ku bind zinatumia karatasi.

Paskali
Okey sawa mkuu labda mie niliangalia karatas zaid badala ya swala zima la kudurufu na kuchapisha kwa ujumla
 
Nafikiri kuna vitu huvielewi. Hapo mtoa mada kaongelea mfano madiwani. Mkoa unakuta unazo halmashauri 6 kila halmashauri unalo baraza la madiwani.

Unapoongelea stationery expenditure usiongelee karatasi tu ndugu yangu hapo kuna Cartirage (wino), kuna kuna repair/maintenance za photocopy machines, nk
nafikir ungeusoma huu uzi ulipoandikwa tu ungeelewa namaanisha nin kuna some editing ndio maana unaona nauliza swali tofauti
 
Ni vizuri tungefahamishwa na gharama za hizo iPads zilizonunuliwa.
Kwa kweli sikuuliza, kwa sababu kilichonipeleka Songwe sio hicho, bali katika maelezo ya Mkuu wa Mkoa, niliiona hii ni habari.

Songwe nako kuna waandishi, I hope they will take it from there na waandishi wengine investigative watataka kujua kama ni kweli hiyo budget yote ni ya karatasi tuyo? , bei ya rim, mzabuni ni nani, alipatikanaje? . Then unakwenda kwenye national wide kama mkoa mmoja tuu unaspend milioni 250 kwenye makaratasi tuu times mikoa yote, ukijumlisha na wizara zote, then utapata gharama serikali ya Tanzania inazotumia kwenye karatasi ,bearing in mind, rims zote ni imported, halafu tafuta gharama ya kuanzisha kiwanda cha karatasi!. Then kumbe tunaweza kubana matumizi by use of ICT only, why we don't?!, nobody knows!, then utakubaliana na mimi, sometimes on somethings, we Tanzanians we must be mad! .

Paskali
 
Nafikiri kiini cha habari hii ya Pascal Mayalla kipo kwenye aya tatu za mwisho;
Nimeona watu wengi wamesoma hii habari juu juu bila kuelewa dhamira kuu ya mleta uzi.
Nilitegemea tujikite zaidi kwenye mambo yafuatayo;
1. Je ni kweli agizo hilo la mkuu lina tija, kwenye kubana matumizi na kiusalama pia. Je nini kifanyike kuliboresha tamko lake?

2. Je ni kweli kuondolewa kwa hizo mil.250 pamoja na kufuta vikao, posho n.k Kutaathiri mzunguko wa fedha mkoani Songwe, kama bwn Mayalla alivyodai?

Kwangu mimi naona uzi huu, ulitutaka kutafakari na kwenda mbali zaidi ya kilichofanywa na wachangiaji wengi.

Huu ni mtazamo wangu binafsi juu ya uzi huu.
 
Back
Top Bottom