Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,158
- 3,108
Wakuu,
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya mwananchi yeyote atakayeonesha viashiria vya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika kesho Novemba 27, 2024 nchini.
"Siku ya kesho ya kupiga kura kila mtu atunze amani. Nitoe hofu kwa kila mwananchi kwenda kupiga kura kwenye vituo bila wasiwasi. Lakini ikitokea kuna uvunjifu wowote wa amani sheria zipo sisi tuwaambie tutachukua hatua"
Senyamule ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 26, 2024 Ofisini kwake huku akisisitiza kuwa ni jukumu la kila mwananchi wa mkoa huo kuendelea kutunza amani kuelekea uchaguzi huo.
Soma pia: Msimamizi wa Uchaguzi Dodoma: Marufuku viongozi kujipitisha kwenye vituo vya kupigia kura