Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,464
Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee tarehe 10/1/2023 ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya kuwakamata wazazi/walezi wa watoto 70 waliokuwa wamekimbilia AFTGM Masanga kukwepa ukeketaji na baadaye kurejeshwa kwa wazazi wao baada ya kipindi cha ukeketaji kupita.
Akizungumza katika nyumba salama zilizopo katika Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Mzee amelitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara na Kanda Maalum ya Tarime/ Rorya kuwakamata viongozi wa Serikali za Vijiji na Mitaa ambamo mabinti hao walikuwepo kwa kutokutoa taarifa za matukio ya ukeketaji kwa Mamlaka zinazohusika kabla hata baada ya ukeketaji.
“Haiwezekani wazazi na viongozi wa vijiji na mitaa wanaoishi na hawa watoto waache watoto ambao walishakimbia kukeketwa bila ya wao kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika ili kuwanusuru watoto hao au kuwachukulia hatua watu wote wanaohusika na ukeketaji” alisema Mheshimiwa Mzee.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi wa Serikali, Siasa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) katika Mkoa wa Mara kujitathmini kuhusu namna wanavyosaidia au kukwamisha mapambano dhidi ya ukeketaji katika Mkoa wa Mara.
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara amelaani tamko lililotolewa hivi karibuni na wazee wa mila wa koo za Wakurya kuruhusu ukeketaji kuendelea hata baada ya msimu wa kawaida wa ukeketaji kuisha na kufanya matambiko ya kuruhusu ukeketaji kuendelea katika kipindi ambacho kilizoeleka sio cha ukeketaji.
“Tamko hili la wazee wa mila linarudisha nyuma jitihada za Serikali na wadau wa maendeleo kupambana na ukatili wa kijinsia na hususan ukeketaji katika Mkoa wa Mara, hatutakubali kuwavumilia, tutawachukulia hatua wote watakaohusika” alisema Mheshimiwa Mzee.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara Mheshimiwa Patrick Chandi Marwa ameeleza kuwa wananchi wa Mkoa wa Mara wanatakiwa kulipa umuhimu suala la kupambana na ukatili wa ukeketaji kwa wasichana na wanawake.
Amewashauri wazee kuendeleza mila nzuri zenye kuleta maendeleo ya jamii na kuacha mila mbaya kama za kukeketa wanawake kutokana na athari za mila hizo katika jamii.
“Tatizo kubwa ni kuwa mwanamke akitahiriwa anaolewa haraka, kuna umuhimu wa kutoa elimu zaidi kwa wanaume ili waache kuoa wanawake waliokeketwa na wote wanaojihusisha na ukeketaji wa wanawake ”alisema Mheshimiwa Chandi.
Mheshimiwa Chandi ameeleza kuwa wazazi wengi wanapenda watoto wao wakeketwe kwa sababu ya matumaini kuwa watoto wao wataolewa na watapata mali nyingi na hususan ng’ombe.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa, Kamati ya Usalama ya Wilaya za Tarime, Serengeti na Butiama, baadhi ya maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Menejimenti za Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Serengeti na Butiama.