Mkuu wa Mkoa Dar, tunaomba urudishe kituo cha Mwenge kama stendi kuu

Tatizo la Makumbusho ni barabara udongo na vumbi zinazoelekea stand. Ni kichefuchefu mwanzo mwisho.
 
Hahahaha kama ni wewe niambie ilikuaje siku ile.
Ukaibiwa pochi mwenyewe ukashindwa hata kuita mwizi ukasema tu "mamaaaa yule kaniibia unalialia tu pale" basi mi nikamuona anakimbia ndo nikaanza kula nae sahani moja nikamkimbiza weeeee nikambiza nikamkimbiza nikamkimbiza kumbe mwenzie mjeda michezo hiyo nishazoea......mwishowe nikampata nikakuletea tu pochi yako ukafuta machozi pale ukasema asante.....nilitaka kuchukua namba ya simu sema ulikua bado mdogo nikavunga!!
 
Ahsante kwa kunivunja mbavu, maana nilikua nimepooza tu hapa :).....
Sikulia, ila nikawa nataka kwenda polisi ndio raia wa pale wakasema mdogo wetu kaa hapa vitu vyako vinaletwa,
Kweli baada ya dkk 10 ndio namuona kijana wa makamo,
Mrefu, mweusi, ana mwili uliojengeka kimazoezi, kaja mpk nilipo akanikabidhi pochi yangu,
Akasema niikague, nikakuta kila kitu kipo vile vile, akanipandisha dala dala na kunilipia nauli, tangu hapo sikuwah muona tena,

Nadhani atakua mtu mzima kwa sasa coz ni kama miaka 10 imepita.
 
Niliibiwa cm yangu pale yaan na pesa juu nilikosa had nauli ya kunirudisha home; msamaria mmoja akanipa nauli ya kunirudisha home; nilichofuata sikununua. Nilirud nyumbani kama mgonjwa vile. Mwenge pasirudishwe kituo; nipo radhi kutembea.
Kweli Tanzania kuna mambo. Kwa akili hizi tutaendelea? Ukiibiwa ukiwa sehemu A basi ile sehemu ndio yenye nuksi na iadhibiwe!
 
Niliporwa pochi hapo Mwenge, ilikua na cm na hela,
Namshukuru Mungu kuna mwanajeshi alimkimbiza yule kibaka mpk akampata nikarudishiwa vitu vyangu.

Natamani ningemuona tena yule mwanajeshi nimpe ahsante ya kiutu uzima, maana kipindi hicho nilikua kabinti kadogo tu.
Kumbe ndio wewe niliokukimbizia mwizi wako ni PM tuongee mengi mama yangu
 
Akili finyu! Kituo kibaki makumbusho! Watu mtembee mmezidi uzembe! Route ya Mwenge - Mawasiliano iweje kama sio uvivu? Kwanza ilitakiwa Mwenge - Mawasiliano pasiwe na kituo cha dala dala hapo kati watu watembee tu!
 
Hakuna kituo salama hapa Dar vyote vimejaa mateja muhimu ni hatua stahiki zichukuliwe kukamata hawa mateja ndio chanzo cha uhalifu vituoni mfano mzuri kwa mtogole.
 
Mpwa si unaona vijana wa sasa walivyowashapu kuchangamkia fursa za ngono au mahaba....je ushapu huu wangeuelekeza kwenye fursa za kiuchumi....si tatizo la ajira lingekuwa historia...

Naam!
Hakika kama vijana wetu wangetumia uzoefu wao wa "kuchangamkia fursa",
Katika mambo ya kujikwamua kiuchumi, wangekua wamepiga hatua sana.

Ujana maji ya moto,
Fainali ipo uzeeni.
 
Me naon mwenge pale ilirahisisha sanaa watu kwenda sehemu tofauti na ilikuwa centre ya mjini,ubungo, mbezi kwa msuguri kila mahali alsfu pia kuhamisha kituo pale imeharibu kabisaaa bishara za mlimani city maana hasaa kuweka mlimani city pale kwa ajili ya kituo kile naonaaa....
 
mi binafsi naona pale mwenge pako vizur sama kuliko makumbusho sababu mwenge pale centre nzur kuliko kule makumbusho kumejificha mno
 
Cha msingi waboreshe barabara za kuingia kituoni kwani mbovu mno..! Hata mawasiliano barabara ni mbovu Sana..!
 
Ahsante kwa kunivunja mbavu, maana nilikua nimepooza tu hapa :).....
Sikulia, ila nikawa nataka kwenda polisi ndio raia wa pale wakasema mdogo wetu kaa hapa vitu vyako vinaletwa,
Kweli baada ya dkk 10 ndio namuona kijana wa makamo,
Mrefu, mweusi, ana mwili uliojengeka kimazoezi, kaja mpk nilipo akanikabidhi pochi yangu,
Akasema niikague, nikakuta kila kitu kipo vile vile, akanipandisha dala dala na kunilipia nauli, tangu hapo sikuwah muona tena,

Nadhani atakua mtu mzima kwa sasa coz ni kama miaka 10 imepita.
Umevikamata kweli vipanga vya JF. Kuwaambia ni miaka 10 iliyopita vikagundua vingine vilikuwa chekechea, vimekimbia
 
Kila anaye_comment hii topic ana jambo lilimsibu kutokana na mwenge -MMENIWAKILISHA.
 
Back
Top Bottom