Mkuu wa majeshi Korea Kaskazini anyongwa kwa tuhuma za ufisadi

Na Rais ndo anapaswa kuwa hivyo, unachekacheka hovyo we shoga!? Sifa ya mwanaume na kiongozi ni kuwa serious. Nashangaa hapa bongo kila siku watu wanatimuliwa kazi ila cha ajabu mali zao zipo palepale.

Kwan! Huyo bonge nyanya mzee wa kunyoa viduku umemuona hacheki? Anacheka na ukisinzia kazini, keshoyake anakiweka uwanyani anakufumua na lile la kutungulia ndege. Saafi!
 
Una maana akiuke Katiba au abadilishe? Unajua implication za Rais kuamua kukiuka katiba?

No impact no implication whatsoever; at least sio katika vinchi hivi vya kiswahili visivyokuwa na taasisi imara za utawala wa sheria! Rais ni Alpha na Omega kama ulivyoona ile alama aliyoapishwa nayo JPM pale uwanja wa uhuru 5/Nov/2015; And you have seen it all; nani wa kumuwajibisha ikiwa wabunge wenyewe ndio hao wachumia tumbo; kila kinacholetwa na serikali ni NDIYOOOOO!!
 
Kwan! Huyo bonge nyanya mzee wa kunyoa viduku umemuona hacheki? Anacheka na ukisinzia kazini, keshoyake anakiweka uwanyani anakufumua na lile la kutungulia ndege. Saafi!
Inawezekana akawa anacheka, analala hovyo hovyo ila nchini kwake husikii kesi za kipuuzi zinazogharimu taifa kama Tanzania.
 
Inawezekana akawa anacheka, analala hovyo hovyo ila nchini kwake husikii kesi za kipuuzi zinazogharimu taifa kama Tanzania.
Utazisikiaje? Tanzania kuna uhuru ndio maana unazisikia ... appreciate that fact!
It is suppression of it not absence!
 
Utazisikiaje? Tanzania kuna uhuru ndio maana unazisikia ... appreciate that fact!
It is suppression of it not absence!
Nahisi kama tutaelekea katika mabishano, na sitaki huko tufike. Unasema labda kwao hakuna uhuru wa habari, kwani Tanzania uhuru upo sana!?
-Hivi unaweza ukaficha idadi ya mauaji ya pembe za ndovu kutoka 200,000 mpaka 40,000? Huko zimapoenda wamejuaje!?
-Utaweza kuficha kuwapandisha ndege twiga hapa Tanzania, je huko waendako utafanya ni siri!? Sio Wamerakani ndio waliofumua hili jambo?
-Wameramba Trilion 3, sio Serikali ya South Africa waliosema kuna watanzania wameficha Trilion 3 na moja ya majina yao ni Mnadhimu Mkuu wa JWTZ kipindi kile bwana Abdulahman Shimbo!? Tanzania vyombo vya habari havikuwa huru, sawa. Je, mbona taarifa tulipata!?
-Kila siku magunia na mizigo mizito ya madawa ya kulevya tunaipitia Bandarini bila watu kujua, mbona huko Australia ilipofika tulijua!?
-Unanunua vichwa vibovu vya treni na Radar, hivi vitu ni vya sayansi. Kama ni kipya utaona ni Quality yake na life span yake wala huitaji mpaka mwandishi wa habari akuandikie.


Kwa kumalizia labda niseme tu kuwa unaweza ukaficha mambo nchini kwako ila uchafu wako utaandikwa nje, sasa wewe ulisikia Ufisadi ukitajwa China au Korea bila mtu kufilisiwa mali na kuchukuliwa hatua? Tanzania si tunamwambia tu ajiuzuru au tunamwachisha kazi lakini mali zake bado zipo palepale?
1. Majina yao hatuna?
2. Mali wanazomiliki TISS hawazijui?
3. Uthibitisho kwa kuonesha kwamba wameligharimu taifa haupo?
4. Kikatiba ukiachana na Rais hao wengine hawana jukumu la kushtakiwa?

Tanzania hatupo serious katika mambo ya msingi yahusiyo maendeleo ya Taifa. Tumebaki kutawaliwa na kuliwa mali zetu na CCM.

Nimesikitika sana kuona nchi inayoongoza kwa kuuza Tanzanite ni India, kisha Kenya na ya tatu ndo Tanzania.
Hizi Rasilimali na ardhi nzuri na kubwa bora Mungu angezipeleka Kenya au Rwanda wanaojitahidi kila siku kuinua uchumi wao, sio sisi kazi kurudia uchaguzi ili Chama Tawala kibaki madarakani.

*** Samahani kama Nilitoka Nje ya Mada ***
 
Wapumbavu watanzania mbona Magufuli anawafukuza alafu mnalalamika...
 
Back
Top Bottom