Mkutano wa Nishati Afrika (Africa Energy Summit) 27-28 Januari, 2025

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,857
4,866
Tanzania inakuwa nchi mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Kuhusu Nishati (Africa Energy Summit) utakaofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe kwa siku mbili 27-28 Januari, 2025.

Mkutano huu unaandaliwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika. Waudhuriaji ni pamoja na sisi wenyeji Tanzania Marais wa nchi za Afrika 24, wawakilishi wa wakuu wa nchi na serikali za Afrika 21; Wakuu wa Taasisi za Kimataifa sita (6) wakiwemo Rais wa Benki ya Dunia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na Rais wa Taasisi ya Rockefeller; na Washirika wa Maendeleo watano (5) watashiriki Mkutano huo. Aidha, jumla ya washiriki wengine 2,600 wa ndani na nje ya Tanzania wamejisajili kwa ajili ya Mkutano huo.


Tarehe 27

Rais wa Benki ya Dunia, Ajay Banga, amesema nishati ya umeme ni haki ya binadamu kwani huwezesha watu kufanya wanachokitaka katika nyanja nyingine za maisha ya kila siku.

"Tukiweza kuwaunganisha watu milioni 300 kwa miaka ijayo, si tu kwenye umeme bali pia na huduma za kidijitali, tutafungua fursa za Afrika hususan ajira kwa miongo ijayo, na tunaweza kufanikisha hilo kwa siku hizi mbili, na haya sio bila shaka, sio mazungumzo matupu.”

GiYH6XUXMAA29WS.jpeg
===========================================================

Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dkt. Akinumwi Adesina ameipongeza Tanzania kwa kufikisha nishati ya umeme hadi ngazi ya vijiji hali inayoendelea kuchochea maendeleo na ustawi kwa wananchi vijijini.

Amesema Tanzania ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika kwa kufanya vizuri katika uwekezaji wa miundombinu na miradi ya usambazaji iliyoiwezesha nchi hiyo kusambaza umeme katika vijiji vyote 12,318.

“Naomba nitumie fursa hii kumpongeza Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha wananchi wa Tanzania kufikiwa na nishati ya umeme katika vijiji vyote, jambo hili linastahili kupongezwa kutokana na umuhimu wa nishati hii katika maendeleo “

“Mkutano huu unalenga kuifungua Afrika kwenye eneo la nishati ya umeme, kuhakikisha wananchi katika nchi za Afrika wanaunganishwa na umeme”.

Akinumwi.png

GiYOsebX0AAaAhr.jpeg


=======================================================

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Tanzania inachukulia mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika - Misheni 300 kama kichocheo cha utekelezaji wa Sera yake ya Taifa ya Nishati inayolenga kuendeleza nishati endelevu, uhifadhi na ufanisi.

Mhe. Dkt. Biteko ameeleza kuwa, pamoja na maendeleo ya nishati tunayojivunia, bado nchi inahitaji uwekezaji zaidi katika sekta ya nishati kwani matarajio yake ni kukuza shughuli za kiuchumi hususan katika sekta za viwanda, madini na huduma za ukarimu jambo ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati zaidi katika sekta ya nishati.

“Sera hiyo pia inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati na kuongeza mchango wa nishati mbadala katika mchanganyiko wa uzalishaji ili kuimarisha upatikanaji, uhakika na usalama wa nishati”

Dotto.png

GiYOsdDWgAAnx5Z.jpeg

GiYH6WdX0AASwTr.jpeg

GiYHQmGXQAALe8k.jpeg

GiYH6WfWAAAkCyr.jpeg
 

Attachments

  • 1000068638.jpg
    1000068638.jpg
    89.8 KB · Views: 1
Wazo ni zuri kuwa na umeme wa kujitosheleza, kushirikiana ni kitu kizuri.

Bila umeme wa kuaminika hakuna maendeleo yoyote. Wakati mwingine wanawapiga vita wanaotaka kuleta umeme wa kuaminika.

Tatizo nchi nyingi Afika hazina mikakati thabiti na haziko serious kivile.
 
Back
Top Bottom