Mkurugenzi aliyetenguliwa Mafia, kuchunguzwa kwa Ubakaji

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,383
8,132
1713551155658.png

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji linamchunguza aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia (DED), Mkoa wa Pwani, Kassim Ndumbo kwa tuhuma za kufanya ngono na mfanyakazi wake wa ndani (jina limehifadhiwa) anayedaiwa kuwa na umri chini ya miaka 18.

Hatua hiyo imebainika saa chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutengua uteuzi wa DED huyo usiku wa Aprili 18, 2024 akiwa Istanbul, Uturuki alikoenda kwa ziara ya kikazi.

Hata hivyo, taarifa ya kutenguliwa kwake iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus kwa vyombo vya habari haikueleza sababu za hatua hiyo.

Taarifa zilizoifikia Mwananchi zinadai kuwa Ndumbo anatuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti huyo, jambo lililobainika baada ya mkewe kugundua.

Pia Soma:
- Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Kassim Seif Ndumbo

- Kiongozi wa Halmashauri Mafia adaiwa kumbaka Dada wa kazi. Je, Utenguzi alifanya Rais unahusiana na tukio hili?
 
Shida ipo kwa mke wake. Mambo ya nyumbani yaishe nyumban tu. Wanawake wanatakiwa kuwa na Siri. Siri za ndani ziishie ndani. Jamaa akifungwa mke hakuna faida yoyote anapata
Mke tayari ana bwana anayemsumbuwa akili, anataka Jamaa afungwe ili akammanulie Kwa uhuru.

Tuishi nao Kwa akili, sasa huyu ni mkurugenzi pesa ipo, Vipi Sisi tunaoungaunga?
 
Mani kitobo kimemponza, ofisini ukimkuta bonge la muheshimiwa,bosi mkurugenzi kitambi meneja
Wanaokwenda Jela SIO wote wana hatia

Juzi kuna Mzee alichomekewa kesi ya ulawiti nikaambiwa nikamuhoji vizuri maana Polisi walishamkamata Mzee wa watu wakamtia ndani Safari mahakamani kwenye kumbana dogo akasema hajalawitiwa na huyo Mzee Ila Mama yake wa kufikia ndio alimpanga aseme hivyo sababu Mzee alikua anamtaka kimapenzi kwa hio akataka afungwe kwa kesi ya ulawiti Ila ukweli dogo hakua amelawitiwa, ndio baada ya kugundua hivyo zikafanywa process Mzee akaachiwa

Usicheze na Mwanamke
 
Back
Top Bottom