Hebu tuachane na haya mambo ya Kiba vs Diamond kwanza tuangalie wanamuziki/wasanii wetu wengine wanafanya nini.
Binafsi nimependezwa sana na kibao cha Q-Chillah akishirikiana na mwenzie T.I.D ambao awali walikuwa wanaunda kundi la Top Band kabla ya kuachana na kila mtu kufanya mziki kivyake (Solo).
Sasa wamerejea na kutoa kibao hiki matata ambacho kimenitia wazimu kabisa maana hapa tu ninapoandika hii post kiuno kinauma kwa kuserebuka....lol
Kibao hiki hakika kimerejesha hadhi ya mziki wetu wa nyumbani (mduara) na kiukweli Q- Chillah nimekuvulia kofia kuwa wewe ndio MKALI WA HIZI KAZI.
Sio kwa kulalamika kule.....umesema wanakuita Sheitwani nami nakuita Ibilisi kabisa.
Kama kuna mtu ambaye hajasikiliza hiki kibao kakosa mengi,hakika UTAKIPENDA TU!
Mie hiki kibao ndio my favourite song sasa......
"Mtoto mdogo mdogo,kabeba mkungu wa ndizi....omamaa omaaa eeeeeh"
Acha kabisa.
Mkuu unamaanisha au utani?Kweli wewe ni ziro...yaani unashangaa na mtoto kubeba mkungu wa ndizi? Je, ukiwaona wale watoto wanaobeba Lumbesa utasema nini, utajiua au?
Mkuu unamaanisha au utani?
Sijakuelewa kiukweli.
Na wapi nilikosema nimeshangaa mtoto kubeba mkungu wa ndizi?
HahahahahahaaaHalafu nifah kwa muonekano wako tu mdada mwenye shape ya kimanyema,wale wamanyema wa zama zile,inaonekano hapo kiunononi mmmhhh iwe boooju,na exaust ni balaa.
Basi huo mduara,ingekuwa unauchezea njenje pale,dah ningekaa nyuma na ile"nchecheme nchecheme leo...oyaaa",
Hapa natafuta huo wimbo ulioukatikia
Hahahaa,wacha we mwanamke nyonga,itabidi asee wakuchukue uonyeshe ujuzi wako....Hahahahaaa hujaacha ule 'wazimu' wako tu?
Hii video kama akina Q-Chillah wangeniomba ningewafanyia mabalaa tena free of charge.
Usije ukadanganyika ukaenda na wewe...Hahahaa,wacha we mwanamke nyonga,itabidi asee wakuchukue uonyeshe ujuzi wako....
Hahah, ntaendaje na mme wangu hajaridhia..afu nimekumiss kwakweli..Usije ukadanganyika ukaenda na wewe...
Ungeniua kwa presha...Hahah, ntaendaje na mme wangu hajaridhia..afu nimekumiss kwakweli..