Mkubwa fela anastahili sanamu ya heshima

Chaos Master

JF-Expert Member
Jul 7, 2021
636
1,310
''MKUBWA FELA ANASTAHILI SANAMU YA HESHIMA.

Usiku wa jana sijalala kabisa, kwani nilizongwa na kumbukumbu ya safari ya Muziki na maisha.

Mbali ya kuwakumbuka watu wengi, Kichwani mwangu ilikuja picha ya darasa lenye Watoto Wanne wenye Masauti yanayogonganisha mashairi yasiyochosha.

Ni kweli nilikuwa nikiliwaza darasa lenye historia kubwa nalo ni "YAMOTO BAND".

Ni miaka mingi imepita toka kundi hili lililowahi kuwa na mvuto mkubwa livunjike.

Na leo sijawaza juu ya kwanini limevunjika!?..Bali nimewaza na kutafakari Uthubutu, Malengo, Kujitoa na Uwekezaji uliofanywa na @mkubwafellatmk

Kwa hakika Natamani kuona Kundi hili lilowahi kuundwa na @mbosso_ @enockbellaofficial @bekaflavour NA @aslayisihaka wanaandaa Tamasha la kutambua, kushukuru na kumpongeza MKUBWA FELA.

Ndio wakiandaa onyesho hili itakuwa wameenzi mchango wake Kwa vitendo, na nayaongea haya kwa pumzi hii niliyojaaliwa leo.

Natamani kuona JUKWAA MOJA, HESHIMA KWA FELA TUKIWA HAI.

Najua naweza kukwaza hisia na matakwa ya Wahusika, lakini MKUBWA FELA ni Mtu muhimu kwakuwa aliwafungulia milango ya Mjini na Muziki.

Natamani MKUBWA FELA ajengewe SANAMU pale Temeke,...kwakuwa kukuza kipaji kimoja kunahitaji miaka zaidi ya mitano, lakini MKUBWA FELA alikuza vipaji vinne kwa muda mfupi. Mzee wa jua la utosi zingatia hili @chambusso

Oooh...nimeshituka Sasa, kumbe kulishapambazuka, Lakini YAMOTO BAND, JUKWAA MOJA NI SHUKRANI INAYOISHI.
#godfathertale #MALENGO '' @babutale
 
Walisema fela aliwajengea nyumba hao watoto kila mmoja Sijui ni kweli.

Ila we unadhani ni kiasi gani fella ametengeneza kupigia hao watoto?fella anaangalia naslahi yake ndo maana akawaacha akakimbilia wasafi kupata maslahi mapana
 
Biashara yao Ilikua GG Fella alikua anafaidika lakini Hata YAMOTO walinufaika chief, Financial na hata kukuza majina yao Kwan hadi leo ugali wao ni mchango wa fella kuwapa majina
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Walisema fela aliwajengea nyumba hao watoto kila mmoja Sijui ni kweli.

Ila we unadhani ni kiasi gani fella ametengeneza kupigia hao watoto?fella anaangalia naslahi yake ndo maana akawaacha akakimbilia wasafi kupata maslahi mapana
Kikubwa aliwafungulia njia hata kama ingekuwa amepata billions, when you invest lengo kuu ni kupata faida ila kwa aliyeonyeshwa njia hata akitemwa inabidi ajiongeze mwenyewe kuendelea kuanzia hapo alipoachwa.

Kuna boost nyingine hazilipiki hata umpe mtu kiasi gani ukilinganisha na jina unalokuwa umetengenezewa.
 
Back
Top Bottom