Mkiachana na mwanamke hakuna mgao wa mali. Anatakiwa aondoke na begi lake la nguo

Sio aondoke na begi la nguo, kila mtu achukue kilicho kwenye jina lake, basi.

Kama magari , viwanja vipo kwa jina la X , basi X atachukua vitu vyake.
Hapo hamna ndoa hapo ni partnership. Sasa unadhani mke atakubali kubaki nyumbani? Na yeye lazima atataka kutoka na yeye afanye kazi atafute mali zake. Sasa hiyo ni ndoa au uhuni?
 
Kuna sheria za Marekani za ajabu imagine uki mdivorce mke wako mgao wa mali pasu pasu . Trump amependekeza kuifuta hiyo sheria ametuwakilisha vyema wanaume. Mwanamke anatakiwa aondoke na begi lake la nguo tu
Hata kama Sheria hiyo itafutwa, bado tatizo hilo la Wanawake Watalaka kuendelea kunufaika kutokana na talaka litaendelea kuwepo. Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba kiuhalisia majanga ya Wanaume Watalaka kuendelea kufilisiwa Mali zao mara tu baada ya ndoa kuvunjika chanzo chake hasa ni wao wenyewe Wanaume. Wanaume wengi sana huwa hawapo makini kabisa kuhusiana na suala zima la kulinda Mali zao wanazozichuma wao wenyewe ili zisiweze kuporwa na Wanawake matapeli wa ndoa, matokeo yake hao Wanawake matapeli wa ndoa wanapata mwanya wa kupora mali zote kabisa za mwanume mzembe kwa kupitia njia ya talaka.

Hata bilionea Bill Gates wa Marekani kwenye ile talaka yake na yule aliyekuwa mke wake alikubali kiurahisi kugawana mali zake na huyo mtalaka wake baada ya kugundua kwamba alifanya makosa makubwa sana kwa kutokusainiana Pre-nuptial Contract na huyo mtalaka wake kabla ya yeye kuamua kufunga ndoa na huyo Mwanamke. Bill Gates alikosea kutekeleza jambo hili na kushindwa kusainiana mkataba huo licha ya kwamba alikuwa anajuwa wazi kabisa kuwa yeye alikuwa anamiliki Mali zake alizochuma yeye mwenyewe peke yake.
Wanasheria wake walimshauri akubali tu matokeo ya kugawana mali zake na mtalaka wake kwa sababu makosa alikuwa kishayafanya yeye mwenyewe katika hatua za awali kabisa za kipindi Cha Uchumba wao.
 
Hapana, kila mtu achukue kilicho kwenye jina lake.., kwanini utake kuchukua kisicho chako?

Sheria hii inasababisha wanawake wengi kudai talaka bila sababu za msingi ili kufilisi na kutapeli jasho la mwanaume..
kuna mmoja alitaka niandike jina lake sehemu , nilimsoma na kujua ni mkora mwenye tamaa ya mbali sijui hata alifia wapi Yule kiumbe
 
Kuna sheria za Marekani za ajabu imagine uki mdivorce mke wako mgao wa mali pasu pasu . Trump amependekeza kuifuta hiyo sheria ametuwakilisha vyema wanaume. Mwanamke anatakiwa aondoke na begi lake la nguo tu
Hapana kuna kitu kinaitwa prenup agreement. Unapaswa kumsainisha mwanamke.
Ukisahau hilo utafyokotolewa
 
Back
Top Bottom