Mke wangu hawezi kabisa kuishi na dada wa kazi

Inaelekea hujaacha kale ka mchezo kako ka kutekenya wadada wa kazi kiuno wakideki
 
Yani umuache mke wako kisa anagombana na mfanyakazi au kwa sababu mnagombana nae sana!? Ujue wanawake wengi wana roho mbaya sana na hasa walopatia vtu ukubwani. Unakuta anamuona mfanyakazi n mtu mweny dhiki sana sasa anataka kutumia hali ya housegirl kum Nyanyasa.
 
Maswala ya Dada wa kazi kwa upande wa kiumeni kiukweli kinaumiza sana, utakuta mambo mengi ya kurekebisha pale nyumbani, Dada wa kazi anatekeleza huku baba akiona kila kitu, sasa kinachoumiza zaidi ni pale mdada anapokaripiwa maneno makali na muda mwingine kutukanwa kabisa, Automatically wababa wengi hawapendi kuona haya mambo, huruma inamjia anaanza kuwa upande wa Dada wa kazi kwa vile ni mnyonge pale ndani na hana mtetezi mwingine. Haya yakiendelea kuwa karibu mwisho wa siku utakuta baba anaanza mahusiano na mwisho we anakuwa na wake wawili ndani ya nyumba, Mmoja ndo wife na wa pili ni Dada wa kazi(kwa siri).Haya mambo yanasababishwa na Wake zetu. Kaa na mtoto wa mwezio kama mwanao. Ukifanya haya sizani kama baba atachepuka na Dada wa kazi. Mahusiano ya Dada wa kazi na baba yanaanza pale tu Dada wa kazi anapoanza kuacha majukumu yake kama mke, na mke kuwa na tabia ya kumnyanyasa Dada wa kazi.
 
Mbona simple hiyo? Usiweke dada wa kazi, mwache yeye awe anafanya kazi zote, Mtoto muwekee hata bill sehem akirudi toka shule apige msosi kama mwezi mmoja hivi atajua umuhimu wa dada wa kazi
 
Jaman mbona hamtoi ushauri hilo ni tatizo la wengi sana, na mm ni mwanamke nimejionea kwa rafiki yangu tulijifungua pamoja watoto hadi sasa watoto wana mwaka 1 ila huyi rafiki yangu toka anamimba wasichana wa kazi wanakimbia hadi mwingine alitoroka wakati rafiki yangu amepata uchungu wa kujifungua wakati yupo hosoitar nyumban dada wa kazi anatoroka na hadi leo amebadilisha wasichana wa kazi hata idadi sikumbuki, hadi juzi ananiambia anataka apeleke mtoto kijijin kwa bibi yake mimi nikamshangaa mtt bado mdogo asimpeleke akasema amechoka kukaa na wasichana wa kazi, ila kwa ufupi mimi namfahamu kabla hajaolewa anatabia ambayo hata mmewake tunamuonea huruma kuishi na yule mwanamke koz mmewake mpole sana ila mwanamke anatabia za kununa hovyo bila sababu harafu mchoyo sana hadi kuna cku walikunywa chai dada wa kazi hakushiba akaenda kwenye friji kuchukua sless za mkate akachukua 2 anataka kufunga mlango wa friji akamkuta na kumwambia ludisha sasa hivi yule dada akaludisha mimi nikamwambia acha uchoyo ukitaka uishi na dada vzr usimyime chakula wengi huwa wanapenda kula harafu inatakiwa uishi nae kama mdogo wako kabisa usimfanye akakosa raha, lakin hata mume wake analalamika mkewake anampa shida ya kutafuta madada kila cku hata mtoto hanaharibika kisaikoloja kila cku unambadilishia mtu wa kumzoa sio vzr, kwa ukweli rafiki yangu tulikuwa tunakaa nae hosteli ila kila akiishi na mtu lazima wakosane hawezi kuishi na mtu vzr tukajua labda akiolewa atajirekebisha lakin wapi sasa hatujui sijui ataweza kuishi na nani mwanamke anakuwa mchoyo hadi chakula!
 
Huwa msichana ninamruhusu kwenda kusalimia ndg zake kila weekend mke wng hatak kabisa hizo habar anataman amuone kila siku

Mkuu kwny mambo yetu huwa namuheshimu sana mke wng kwan amebarikiwa kila IDARA

Wewe nae unaingilia mipaka ya ndani unaona sawa wewe kumpa ruhusa???hilo ni jukumu la mkeo...
 
  • Thanks
Reactions: nao
Wanawake wengi wana tatizo na Mahousegirl, HG ni wa kupita tu. Usiachane na Mke kwasababu ya HG, Mwachie mwenyewe aangaike nao, akiondoka atafute mwingine akipata poa, akikosa kimpangowake.
 
Wanawake wengine wana Gubu jamani hawawezi kuishi na watu nakushauri na wewe jaribu kumchunguza mkeo harafu uwe unamfundisha jinsi ya kuishi na wadada wa kazi sio kila dada wa kazi anatabia mbaya hapana wengine ni wazuri ila tunaishi nao vibaya.
 
Kaka. Pole sana, usimuachilie huyo mkeo kunyanyasa dada wa kazi, ujue dada wa kazi ndio anayebaki na watoto wako, muda mwingi. Wadada huanza kutesa watoto wanapoona wanadharauliwa na kunyanyaswa na mama. So usiache watoto wako wateseke. Simama kiume, mwambie mkeo aache tabia hiyo, house girl mwomesheni upendo kama sehemu ya familia yenu, hata upendo wa kinafiki.
 
Mkuu jeuri za wanawake huwa zinaanza polepole, leo anamchukia kila housegirl, hukemei. Kesho anamchukia kila jirani, hukemei. Kesho kutwa anamchukia kila rafiki yako, hukemei, unanung'unika tu. Wiki ijayo anamchukia kila ndugu yako na hatimae wazazi. Unakuwa hujui uanzie wapi kukemea.
Mjenge mkeo apende kuelekeza kwa upole, na kuchukia kwa kukunja sura, badala ya kubwatuka kwa sauti.
Jingine, jaribu kuwaongelea vizuri hao majirani ukiwa na mkeo, pengine mnayoyaongea ndio humfanya awachukie.
 
Kama anagombana na dada wa kazi kwanini usibadilishe na uweke kaka wa kazi. Pengine watapatana vizuri tu
 
Unasema una mwanamke ambaye unaishi naye, tena ukasema mkeo???!!!!! Huna hakina ni mkeo au mwanamke tu?

Ila kwa ushauri tu mambo ya wadada wa kazi yaache, Potezea kabisa. Akifukuza we kaa kimya, usihangaike wala kuulizia au kutafuta mwingine. We hakikisha tu anatimiza majukumu yake kama mama!

Mwelekeze UPENDO pia, ajifunze kuheshimu, kupenda watu na kuelekeza kwa utaratibu
 
Huyo ana ghubu mkuu!
Kosa lako hukuchunguza tabia yake kabla hujamuoa.
Hakuna ulazima wa kutarikiana nae, chamsingi acha kumsakama au kuwaka sana juu ya hiyo tabia yake. Jenga mahusiano mazuri na majirani zako na jukumu la yaya muachie yeye kila ratiba.
Akikuzingua sana mtulize kwa kumzaba vibao viwili vitatu bila maneno mengi atajinyosha mwenyewe!!
Sasa unamshauri amzabe vibao bila hata kujua wahusika wanafananaje? je kama Mama ni Asha Boko na Jamaa ni Eric Omondi......azabe kibao alafu asokotwe kama dawa ya mbu....ile ya kuchoma.
 
Mbona unaingilia mambo ysiyokuhusu. wanawake wengi wako hivyo. nyamaza tu na uendelee kuangalia tu yanayoendelea labda akitaka kumpiga na kumjeruhi ndio uingilie mkuu.MAYAYA NI JUKUMU LA MAMA NA SHAMBA BOI NI JUKUMU LA MWANAUME. NI MIPAKA SASA LABDA TUSEME WEWE UNATAKA UHUSIANO NAYE. sisi tukishaingia home ukishapewa shikamoo yako unanyoosha bedroom.kwa usalama wa ndoa.
Kabisa naeza sema wadada wengi wana matatizo maana wanahisi wanatumikishwa hata kama hawataki na ni wakorofi lakini kuna walio wema pia.Cha muhimu mkeo awe na busara na hekima ktk kuishi na watu hatakiwi kujiona yeye ni bora kuliko yeyote anatakiwa awe na unyenyekevu hata anaemfanyia ubaya ajisikie aibu lakini mpk majirani hapo tatizo lipo na ndugu sasa si ndo ishu ingine.Hekima hekima hekima na hili ni tatizo la wamama wengi.
 
Back
Top Bottom