Mke wangu anachat na li mtu wanaitana "MY"

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
13,517
22,461
Aisee! Huwa naichunia simu ya mke wangu kwa kuogopa BP na pia namuamini maana ana kautulivu kimuonekano na maisha tulioishi hajawahi kuniletea mazombie mpaka yanitishe na kuhisi sio mwaminifu.

Sasa leo weekend nipo kitandani nimeshika simu yake aisee! Kucheki video za whatsapp nikajikuta nimeingia inbox yake kuna li mtu anachat nalo linaonesha linamcare huku linamuita "My" na yeye anajibu na neno "My".

Hapa nilipo nimeshapanic japokuwa wanasalimiana tu na kutakiana chakula chema ila kimenishangaza hicho kibwagizo chao cha kuitana "My" nataka niuwashe moto maana sijaelewa kabisa hiyo term "My".

Naogopa kuianzisha hii vita kabla sijajua wenzangu hii issue mnaichukuliaje maana nisije itwa Complicator wa term kumbe ni term ya kawaida tu.

NATAKA USHAURI SIO MATUSI.
 
Kwa mantiki ya Chats zao, MY humaanisha WANGU.

Ni neno la kawaida sana kutumika baina ya jinsia ke. Lakini pia linaweza kutumika baina ya jinsia ke na me.
Sasa kuitana huko sijajua wana lengo gani. Ila kwa experience yangu, ke na me wakiashaanza kuitana "my" basi uwezekano wa kukutanisha vikojoleo ni mkubwa.

Cha msingi, we muambie tu aache tabia hiyo. Kama umekuta salamu na wishes za mlo mwema, basi hiyo my yao haijawa Chronic bado. Ipo katika hatua za awali.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…