Mke wa rafiki yangu ananitesa kwenye WhatsApp

Pole kwa matatizo mkuu! Ushauri wangu endelea kuwa na msimamo thabiti wa kutomweka akilini mwako wewe endelea kuwa nae karibu kama shemeji yako hali halisi itajieleza. Pia bado kuna option za kiteknologia za kublock followers ambae si mzuri kwako ila hii iwe hatua ya mwisho sana.
 
Kama unapenda urafiki na mwenzako, mblock huyo mwanamke kwenye social networks zote. Akitaka kuwasiliana nawe atakupigia simu, pia nanusa yeye kuanza kukusingizia majambo.

Kukanya kwa maneno hakusaidii, na usiende kwao bila kuwa na mtu mwingine kama ukitakiwa.

Natumaini huwa haumjibu, sababu ndio atakumaliza nayo kama umemjibu chochote.
 
Alafu mkuu huu uzi umeweka details nyingi. "Embu edit fasta kabla watu hawajauona kwa wingi. Toa sehemu kama Singida, Mwanza, NMB nk ili watu wasiweze kuunganisha nukta! Mudi msaidieni huyu kiazi jinisi ya kuandika uzi bila kuhatarisha ndoa ya mwenziwe...
Inawezekana baada ya kutoa ndio akaweka hizo sehemu
 
Imeandikwa ktk Biblia.
Kut. 20:14 Usizini
Law.18:20 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi
Law. 20:10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naan, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauwa.
Uamuzi ni wako.
 
Hii thread itavunja ndoa za watu
Maneno kama Singida,Mwanza,NMB,Kampani yangu Mwanza,Rafiki wa miaka 6 nk
 
Wakushauri kwenye hili kweli? Mbona suluhisho lake liko wazi sana? Huyo ni mke wa rafiki yako sasa hapo kuna la kukushauri? Labd kukukumbusha kama umesahau kama ni mke wa rafiki yako mkuu
 
Bwana kaka mwambie hutaki majaribu ya kipuuzi hayo na umwambie humpendi kwani umpendae unae ndani tayari na yeye aliye mpenda wapo nae ingawa kasafiri, Funga siku mbili bila kula ukimuomba mungu wako akuepushe na huyo ibilisi naamini utafanikiwa na hatakutumia tena hizo picha.
Kwani hadi haya ashauriwee wakati anayajua? Labda kama amesahau tumkumbushe tuu
 
Kuna threads nyingine huwa hajina tija. Sanasana ni kuhatarisha ndoa, kazi na probably maisha ya mtu mwingine. I am sure kama mume au huyo mwanamke ni member hapa, atakuwa keshaconnect dots.

Ingekuwa kila mwanamke au mwanaume anayetongozwa anakuja kuomba ushauri huku, pasingetosha. Sometimes we only need to use our common senses a little bit to sort out very minor daily issues.
 
Anafikiri wewe ni kama yeye asiyejua thamani ya ndoa na urafiki. Prove her wrong, mwambie mumewe. That's what i would expect from a true friend.
Mkuu, tambua wanawake ni wajanja sana na pili watu wanaojifunika shuka moja usidhani ni rahisi hivyo kuwatenganisha.Ukitaka huyu jamaa agombane na rafiki yake na wasizungumze milele ni kwa yeye kumuambia mume wa huyo mwanamke.Kwani sinema itabadilika na huyo dada ndio awe muhanga wa kukosewa adabu na huyu jamaa.Huyu jamaa ni bora awe mkali na kumuonya kuwa atamtumia mumewe ujinga wake asipo acha mara moja.Atumie hekima wakati wa kulitekeleza hili, kwani akikosea mahali mke wake ataambiwa maneno tofauti na huyo dada,na ndoa yake yeye itakuwa mashakani.
 
Mwambie rafiki yako mapema lasivyo hawa wanawake wasahaulifu atasahau video au message na akikuta jamaa hatoelewa story zako hata kidogo.Nakushauri ongea na rafiki yako friendly na umwambie hupendi urafiki ukome
 
Salam ndugu zangu.

Nina rafiki yangu ambaye yeye anaishi na kufanya kazi Singida na mimi nakaa Mwanza. Hapa Mwanza yupo mke wake ambaye naye ni mfanyakazi wa benki. Kwahiyo, rafiki yangu huja Mwanza kumsalimia mke wake na kurudi zake Singida, anapokuwa Mwanza mimi ndiye kampani yake mwanzo mwisho. Tumeanza urafiki miaka 6 iliyopita kwahivyo familia zetu zimekuwa kama ndugu tu.

Sasa basi, huyu rafiki yangu anapokuwa hayupo (akiwa Singida), mke wake hupenda sana kunitumia threads, clips au picha zinazpashiria uvunjifu wa amri mojawapo ya vitabu vitakatifu. Anapenda sana kunitumia nyakati za usiku.

Nyakati zingine hujipiga picha akiwa kitandani na kunirushia zikiwa na ukumbe "karibu tulale". Video za kugegedana anapenda sana kunitumia.

Nimemkanya sana lakini haachi, mke wangu sijamwambia na siwezi mwambia kwani wataharibu uhusiano. Anaweza kunitumia video nyingiii, mimi simjibu hata moja lakini hakati tamaa.

Naombeni ushauri nifanye nini ndugu zangu,

Asanteni
Huyo mwanamke kafungashia lakini mkuu?
 
-Mmeanza urafiki miaka 6
-Mme anakaa na kufanya kazi Singida.
-Mke anafanya kazi Mwanza, na taasisi umeitaja (Bank)
-Jamaa anakuja Mwanza na akija wee ndo mwenyeji wake sehemu nyingi.
Kwa dondoo hizi ni rahisi sana kuvujisha siri kama jamaa yupo humu. So jichunge sio ajabu anakulia timing tu.
 
Mkuu nipigie mm pas hlo
Dili nile huo mzgo kama
Ww hutak

Fanya makeke unitupia
Direction pm mkuuu
 
Back
Top Bottom