Mkapa: Najuta

Akizungumzia ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) amesema, Mwalimu Nyerere aliona faida za ubinafsishaji na kwamba, aliona umuhimu wa kuibinafsisha benki hiyo.

Hapa heri angejifanya kasahau maneno mengine, make hili lilizua jambo.
 
Viongozi wa ccm ambao hawamuogopi Mungu wanawezaje kutukejeli kwa kujifanya wanaomba msamaha ?
 
Kwa hali ya nchi hii ilipofikia , kwa uminyaji huu wa haki za wananchi , naapa kwamba sitamsamehe mwanaccm yeyote nikiwa hai au mfu .
 
mimi kama mtanzania sitaki uniombe msamaha style hiyo. nataka vile vile ulivotumia nguvu na muda wako mwingi kuhakikisha anakuwepo huyu aliyopo sasa, umkalishe na umfundishe kusikiliza wataalamu na umuhimu wao katika maamuzi hasa yahusuyo maswala nyeti ya taifa. ukifanya hivo nitakusamehe..
 
Hata angeifilisi nchi yote tutamfanya nini?hii wanatuona kama mazoba ndo maana wako tayari kuiba kura ili chama chao kiwalinde
 
Sipendeleagi kusema haya but nimelazimika kuyasema walau kidogo; tokea nchi imepata Uhuru Magufuli ni rais 5 kukaa Ikulu na anafanya kua rais 3 Mkristo. Hawa 4 (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete) ni 2 tu ndio nimewahi kuwasikia kwa masikio yangu na kuwasoma wakiomba msamaha mahali walipokosea, tena wote wameomba msamaha zaidi ya mara 1 na wamefanya hivyo hadharani; ni Nyerere na Mkapa. Sijui ni kwasababu ya malezi ya dini zao kwamba lazima mtu atubie makosa na maovu yao au ni unyenyekevu (ambao nao still umekaa kimalazi ya Kikristo zaidi). Sina kumbukumbu kama nimwahi kumsikia Mwinyi na Kikwete kuomba msamaha (Mwenye kumbukumbu anikumbushe). Swali ninalo jiuliza, hivi hawa wengine ni kwasababu ya malezi ya kidini au misimamo ya dini zao au imetokea tu kama coincidence? Mwenye uelewa tafadhari.
Mbona hakusema hayo siku alipokabidh ofic,pia msamaha huombwa kwa Mungu haswa kwa jambo la umma na c kwa watu huenda huu ukawa unafiki!uongo na dharua!mbona hakiri kuhusu mgodi wa kiwira?
 
Hii ni moja ya speech ya ki.pu.mba.vu na kilo.fa zaidi toka kwa kiongozi kuliko upu.mbavu na ulo.fa aliouna kwa watu waliompa heshima ya kuwa kiongozi wa nchi.Ubinafsishaji anaojaribu kuujutia hapa ndiyo uliompa fursa ya kufanya biashara akiwa ikulu.

Kupitia Sera ya ubinafsishaji aliyoisimamia mwenyewe,aliweza kufungua kampuni ya ANBEN na kujimilikisha kinyume na sheria za nchi mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira.Leo hii anapojaribu kutoa kilio cha machozi ya mamba,anapaswa alisemee hili,akiri hadharani kuwa aliitumia ofisi ya Umma kujinufaisha binafsi.

Ni katika uongozi wake rais wa sasa alisimamia uuzwaji wa nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa huku baadhi ya nyumba hizo zikitolewa kwa "vidosho" wa wanene.

Pamoja na kukiri kushindwa kwake,uongozi wake uliacha majeraha mengi ambayo hayatasahaulika milele.Ni katika uongozi wake Taifa lilishuhudia mauwaji ya wapemba waliouliwa kikatili na majeshi yetu yaliyoapa kuilinda mipaka ya nchi yetu,lakini kwa mara ya kwanza badala ya kuilinda mipaka yetu,yaliwageukia Watanzania na kuwafyeka mithiri ya kuku alaye mayai yake.Kwa Mara ya kwanza nchi yetu ilizalisha wakimbizi baada ya kukimbilia nchi jirani ya Kenya kuukimbia mkono wa chuma na vifaru vya majeshi yetu vilivyokuwa vikiwaswaga kwa amri ya Mkuu wa nchi.

Huu waweza kuwa uchochezi kwa Tafsiri ya Policcm,lakini haya ninayoyaandika si uchochezi bali ni ukweli mchungu ambao viongozi wetu wanatamani waufute katika kumbukumbu za vichwa vyetu lakini hawawezi kwa sababu hawana mamlaka ya kutawala na kuzitiisha akili na dhamiri zetu,wataishia kutawala viwiliwili vyetu tu lakini si ufahamu wetu.

Viwiliwili wanaweza kuvitawala hata kwa taarifa za intelejensia feki ya policcm inayowapa kibali cha kuswaga watu kwa mabomu na Maji ya kuwasha.Unafiki wa watawala wetu na wapambe wao ukijaribu kuuweka katika viwango vya kidunia,waweza kuwa ni unafiki wa kiwango cha PhD.Mtu anakurupuka bungeni mithiri ya msukule na kuiomba serikali ijenge uwanja wa kumbukumbu ya push-ups na bado waziri mwenye dhamana badala ya kukemea upuuzi huo,anamuunga mkono kwa kuahidi kufikiri namna ya kujenga kumbukumbu hiyo.Kati ya push-ups na mauwaji ya Wazanzibar yaliyosimamiwa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni kipi kilipaswa kujengewa kumbukumbu?Wazanzibar waliouliwa makumi kwa makumi mwaka 2001,maadhimisho yake hadi leo hupigwa marufuku na jeshi la police kana kwamba waliouliwa Zanzibar walikuwa ni magaidi,lakini kutokana na mparaganyiko wa maono ya kiutawala,watu wanaomba kumbukumbu za push-ups na serikali inaridhia,je hoja za aina hii haziwezi kuwa kigezo cha kulifanya Taifa letu kuandikwa kwenye Vitabu vya maajabu ya Dunia kama Taifa la watu wa.pumba.vu zaidi Duniani?

Hii ni nchi ya ajabu sana ambayo ukijipa muda wa kuitafakari unaweza kuishia korokoroni kwa kuitwa mchochezi kwa kuwa tu unajaribu kusema ukweli ambao viongozi wetu hawapendi kuusikia.Mungu tusaidie kupata viongozi wenye hofu ya kweli kuliko hawa wa kumbukumbu za push-ups.Amen.
Kwi kwi kwi kwi 'vidosho"
 
Mkapa kama hakujibinafsia Mali za umma na kufanya biashara lkuru.. wakati anatoka madarakani alitangaza alichovuna? anatembeleaga migodi ya dhahabu na makaa ya nawe Kiwira)???? leo ndo anajifanya mzalendo??
 
Alikuwa jeuri na mbabe sana huyu... msamaha empty tu utasaidia nn...? I don't accept...!! NBC asidanganye watu, MWALIMU ALIPINGA sana sana... na watu wengi wasomi walipinga.. ila yeye alibinafsisha nakuwapa makaburu rafiki zake..!! Kama ana uchungu na nchi hii AKAUZE HOTEL YA KIMATAIFA ILE PALE DURBAN South Africa aliyojengewa na matajiri kama asante... na siku ya ufunguzi wa hotel hiyo ya KIFAHARI, alimwalika Mh. Nelson Mandela na ALIKATAA NA KUMUONA HAFAI, sbb MANDELA ALIJUA NI RUSHWA HIYO na kumwambia pamoja umehongwa na nchi yenu maskini na umepewa asante na matajiri si basi UNGEJENGA HATA KWENU TZ watu wako wapate ajira..!!

Huyu nae ni walewale..!!
Nadhani anafikiria kuwa hatutakumbuka yaliyotokea, au aloyafanya!
Nakumbuka kipindi hicho kils kitu kiliuzwa bei karibu na bure. Je twaweza kuvirudisha? Baada ya hopo ndiyo nilijitoa katika kuchangia siasa humu jamii kwani nilikuwa sielewi watu bado walikuwa wanamtetea ati analeta maendeleo nchini.

Hata hiyo hoteli alojenga kuna baadhi ya watu walisema sawa na walikataa kuwa ni rushwa ya wazi.
 
Ni jambo jema sana kwa kiongozi kuona makosa yake na kuomba msamaha. Pamoja na kuona makosa yake bado chama kinachoongoza nchi ni chama chake na bado ana nafasi ya kurekebisha makosa ambayo ameyaona.

Kwa miaka yote kumi alishindwa hata kumshauri Rais aliyekuwepo arekebishe hilo? Je sasa anashindwa kuona kuwa anaweza kushauri na kurekebisha?

Kuomba msamaha kunaenda sambamba na kufanya matengenezo katika njia aliyokosea.

Je kule kuuza nyumba za serikali ambazo zilijengwa kwa kodi za watanzania wote na baadaye kuuzia watumishi wachache wa serikali hilo analiona limekaa sawa katika vipimo vyake vya dhamiri?

Maadamu anaishi ashauri marekebisho katika njia alizokosea na hapo tutajua kweli anajutia makosa yake. Kwani bado watanzania wanaendelea kuteseka kwa maamuzi aliyoyafanya akiwa Rais na bado ananafasi ya kushauri kwa kuwa chama cha chake ndicho bado kiko madarakani.
 
Kwanini aombe msamaha kwa watu amboa hatuwezi kumfanya lolote hats kama tutaukataa msamaha huo. Akafie mbele! Aombe msamaha kwa Mola wake.
 
Ni heri wananchi kulalamika kuliko kiongozi tena wa juu (Rais) kulalamika hata kwa mambo ambayo yeye mwenyewe aliyatekeleza kwa akili zake zote na nguvu zake zote! Tujiulize huyu mzee alitakiwa ajifunze kabla hajawa rais iliatekeleze vizuri majukumu yake au baada ya kustaafu ili awakosoe wenzake? Je, wazee kama hawa wanaotaka kutuaminisha baada ya kutoka madarakani wakipewa tena nafasi watatufikisha tutakako kwenda?

Watanzania wenzangu tusisahau kauli zake! alikuwa tayari heri watanzania (wananchi) wale manyasi anunue Dege linaloweza ruka masafa marefu na mtu 1 tu hadi bara wasiloishi watu ( Antarctica) )bila kutua njiani. Kwanini wenye akili timamu wanaojua kauli kama hizi za watawala wasilalamike?
 
Mbona hakusema hayo siku alipokabidh ofic,pia msamaha huombwa kwa Mungu haswa kwa jambo la umma na c kwa watu huenda huu ukawa unafiki!uongo na dharua!mbona hakiri kuhusu mgodi wa kiwira?
Labda kwa kitabu kingine; kwa Biblia lazima uanze kuomba msamaha kwa aliyekukosea kwanza then ndio uende kwa Mungu. Yaani we unikosee mimi halafu unaenda kwa Mungu? Kwa mafundisho ya Yesu hata sadaka hutakiwi kutoa hadi umeenda kupatana na aliyekukosea then ndio urudi Kwake.
 
Labda kwa kitabu kingine; kwa Biblia lazima uanze kuomba msamaha kwa aliyekukosea kwanza then ndio uende kwa Mungu. Yaani we unikosee mimi halafu unaenda kwa Mungu? Kwa mafundisho ya Yesu hata sadaka hutakiwi kutoa hadi umeenda kupatana na aliyekukosea then ndio urudi Kwake.
kuwa muelewa ndugu!unadhani watz 45ml utawaomba msamaha kwny kongamano ambalo dhamira ilikuwa kujadili kitu kingine eti ww unaibuka na kuomba msamaha watu waliopo ukumbini!Huku ukiwadanganya na kuwadharau!yy amuombe mungu wake sio cc!cc tulikataa ubnafsishaj yy alilazimisha!
 
Back
Top Bottom