Mkapa Help This Guy

Status
Not open for further replies.
Masatu sina cha kuongeza, kula tano mkuu.

Nadhani unatakiwa usome between the line. Hii habari inasikitisha sana, ila kuna kitu ambacho ni kikubwa ambacho kimefichika hapa, hasa pale aliposema watoto wake wote watatu wamemtelekeza na hajui walipo. Mimi binafsi sielewi ila kama kuna wa karibu naomba atueleweshe hapa.


Nadhani hapo ni kumwonea tu Pro Mwandosya!



I just dont get it!

There seems to be many of you guys who have no idea of the situstion at Home.In particular,in the rural areas.Obviously,you'll went from the cities to abroad and have never stepped foot back in the village.
There are many cases like this;people who followed Mwalimu teachings religiously.
 
Lakini sikujua alitupiliwa mbali, ili aumie sana kimaisha, ingawa hajasahauliwa...

...Labda pia aliongopewa na wafanyakazi wenzake, pamoja na ndugu zetu wa usalama - wanaodhani wanaipenda nchi yetu kuliko wananchi wengine - waliotoa ushadi (perhaps concocted evidence against him) na kumharibia maisha.

Kuna sababu mbali mbali pamoja na wivu, na kupalilia unga - ngano! - zilizowafanya watu fulani kumwandama na kumtosa shimoni, kiasi cha kwamba imemlazimu aishi maisha hayo ya umasikini na taabu nyingi sana.

Bila shaka kuna viongozi wakubwa, wa taifa, walioamua anyamazwe na aishi maisha hayo: ili aumie sana, na pia to humiliate him, especially when you take into account the fact that he is a very proud man; not arrogant but proud and sefl-confident, also with a stubborn streak. I know him well. And he's very friendly; also he never looks down on anybody. But he's also very outspoken.


.
.
.

Last, but not least, mkichunguza zaidi, mtapata ukweli kuhusu Mwafongo. Na inawezekana atasaidiwa ikiwa viongozi wetu wataamua kufanya hivyo na kuwaruhusu rafiki zake wampe msaada, hasa kazi, hata ikiwa siyo ya uandishi tena.
Duh, mkuu Darubin heshima zoooote! Nimekubali JF kiboko!!!!
Nashukuru kutupa mwanga kuwa Intelligent officers lazima waheshimiwe maana ndio walioishika nchi. Lakini inatosha bwana, wamuhache mzee wa watu walau aone tamu ya maisha kwa muda mfupi uliobaki kabla hajawa RIP, alilitumikia Taifa licha ya kufanya kosa!
 
Darubini

Makala ndefu lakini hamna substance swali dogo la mstari mmoja lililoulizwa na MzalendoHalisi limebeba ujumbe mzito wa kuliko jamvi lako ulilotandika hapo juu.

Hivi mtu akirost lazima kuwe na mkono wa serikali? basi hata hao watoto wake wa kuzaa mwenyewe (naambiwa wapo Marekani) nao pia wanawekewa kazibe wasimsaidie baba yao?

Huyo itakuwa ulabu ndio umemfikisha hapo umeiona ile picha yake? look like someone in Ukhomboti Pub.
Si afadhali ya huyo alikuwa afisa mwandamizi kuna mawaziri kama Pfo Machunda,Tewa Said Tewa, Jaji Mwesiumo wapo hohe hahe nao pia wapo hivyo kwa sababu ya usalama wa taifa?
Asante....hiyo sentensi imenichekesha sana!
Mimi sikubaliani na hii notion kwamba mtu maisha yakimgonga...akaokolewe sijui na nani? Sasa itabid BWM hata wale aliokuwa na P1 awape pessa. Manake nao wako wengu tu huko Lupaso.
I mean let us not look for lame excuses za kutokufanya kazi.
Sasa mnataka kuanzisha "HELP FONG ACCOUNT" AU ?
My solution would be hao watoto wamtunze baba yao? Au labda Mr Fong anahitaji ushauri nasaha tu...jamani frustration inaweza ikakulemaza!
 
Thus Spoke Darubini the Cryptic.Zarathustra has nothing on him!

I remember it was once, twisted from "Light at the end of the tunnel" to be an oncoming train.

By none other.
 
Darubini,

Naona unawakuza mno usalama wa taifa kuliko uwezo wao.

Kama ni kumsaidia huyu mzee, kuna njia nyingi za kumsaidia
bila kuomba ruhusa usalama wa taifa.

Nimekaa Kyela kwa muda na nina uhakika huyu Mwafongo hayuko kule pamoja na kwamba kuna Mwafongo wengi sana Kyela. Angelikuwa Kyela ningemfahamu au hata kuwahi kusikia habari zake. Kweli Mwangota alikuwa wa Kyela na naifahamu vizuri familia yake yote.

Kulingana na Mwandishi alivyoandika, huyu yuko wilaya ya Rungwe. Itabidi kuangalia kama kuna watu wanamfahamu huko.

Mimi naona tatizo hapa, jamaa kuna wakati aliporomoka na marafiki
wameshindwa kumsaidia na kwasababu na yeye anakufa na tai yake shingoni, kaamua kuendelea kuteseka kuliko kuwapigia magoti hao waheshimiwa.

Hapa usalama wa taifa ni kama wanapata sifa isiyo yao. Lazima tukubali kuna tatizo hapa na tuangalie tunawezaje kumsaidia huyu mzee. Huyu mzee hahitaji handouts, kinachotakiwa ni kazi hata kama ni part time ili arudishe confidence yake na aanze kujitegemea.
 
Mkulima una pointi kuhusu kufa na tai shingoni.

Inaweza kuexplain kwa nini darubini alikutana naye Christmas lakini hakujua predicament yake.
 
Mkulima una pointi kuhusu kufa na tai shingoni.

Inaweza kuexplain kwa nini darubini alikutana naye Christmas lakini hakujua predicament yake.

Pundit,

Soma vizuri, Darubini hajasema alikutana naye Christmas.
 
Darubini,

kama nilivyosema hapo awali "Fong" inabidi aombe radhi na vizuri umesuggest njia mbali mbali za yeye kufikia hilo lengo na hatimaye kusaidiwa.............

Whaaaat?? no panick at all!!! haya endeleeni kutafuta na kudhani id za watu........the main point here is ikiwezekana huyu "Fong" asaidiwe.....hayo mambo sijui ya kuwa Ogah alikuwa na umri gani wakati gani...........nafikir ni irrelevant kwa hapa na kwa hii mada.........ukitaka kunifahamu just pm me.......
 
Mkuu Darubini heshima yako.

Umesema mengi yenye kuelimisha, asante. Lakini mengine yanafanana na matisho, mfano haya ya kutaka kujua ama kuonesha kumjua Ogah, jina halisi umri nk. Hapo utaniwia radhi mzee wangu, naona hapaoneshi nia nzuri.

Nikirudi kwenye mengine uliyoyasema ni ya ukweli na baadhi yetu yametukumba pia. Miongoni mwetu naamini wapo wanaokumbuka mgomo wa UDSM wa mwaka 1990, ile kesi maarufu ya "matusi ya nguoni" aliyotukanwa Chancellor wa wakati huo, Mtukufu (kama alivyoitwa wakati huo) Rais Ali Hassan Mwinyi. Chuo kilifungwa wanafunzi wakapewa maelekezo ya kuripoti kwa wenyeviti wa vijiji wanakotoka. Wakatimuliwa na FFU. Na kama vile haitoshi, ilitolewa amri kuwa ni marufuku mtu yeyote kuwaajiri vijana hao, la sivyo atakiona. Na kweli yeyote aliyejaribu kutafuta kazi, mwajiri akigundua tu kuwa u miongoni mwa waliosimamishwa UDSM anakutimua mara! Kumbuka hicho kilikuwa kipindi ambacho watu wenye elimu ya kidato cha sita walikuwa "mali" kwenye soko la ajira, wengi wakifundisha kwenye mashule ya binafsi, wakifanya kazi kwenye makampuni mbalimbali katika nafasi mbalimbali. Lakini waajiri walikuwa wanalazimika kumkataa mtu aliyesoma B.Com hadi mwaka wa tatu, au waalimu na wahandisi waliokuwa kwenye mwaka wa mwisho katika kozi zao, na kuchukua trainees kutoka form six na form four, kwa hofu ya "mkono wa serikali". Wale waliokuwa viongozi wa ile iliyoitwa MUWATA walikomeshwa zaidi. Ilikuwa ni makosa hata kuonekana unazungumza nae. Mtu akionekana amezungumza na mmoja wa hilo kundi la "ring leaders" alitishiwa yeye pamoja na familia yake. Kijana mmoja nakumbuka aliwekwa kikao na familia yake kumsihi amzuie rafiki yake asiwe anakuja kwao kwani kuonekana kwake pale kulikuwa kunaiweka familia hiyo katika "wakati mgumu". Yaani walifanyiwa unyanyapaa kabisa.

Kwa maelezo ya ndugu Darubini hapo juu, inaelekea huyu bwana Fong alifanyiwa kitu kama hicho walichofanyiwa hawa wa UDSM mwaka 1990, naye akashindwa kabisa ku-adjust na hali mpya. Hii inanifanya niamini kuwa njia alizopendekeza za kutatua tatizo hilo ni sawa, maana bila hiyo "ban" kuwa lifted hawezi kuajirika popote. Lakini bado nina mashaka na huyu mzee, baada ya isolation kwa miaka yote hiyo, ataweza tena ku-fit kwenye mazingira ya sasa? Cognitive faculties zake zitakuwa bado nzuri na zinazonunulika katika soko la leo?

Linalonishangaza kuliko yote ni hali ya huyo Fong kutokujua familia yake iliko, ama watoto wake kutokujua aliko au kumsaidia mzazi wao. Hii nadhani haina uhusiano wowote na mambo yaliyomkumba katika ajira yake na serikali, ila ni tatizo lake ndani ya familia yake. Hata serikali ikimtelekeza ama "kumshughulikia" mtu, sitegemei familia yake nayo imtendee hayohayo. Pengine ana personality disorder ambayo ndiyo imemfukuzia familia yake, na labda hiyohiyo ndiyo iliyompotezea ajira yake. Nashawishika kuamini kuwa huyu jamaa "aliifukuza" kazi kama "alivyofukuza" familia yake. Speculations tu. Labda msaada uanzie hapo kabla hajatafutiwa kazi nyingine, maana hatuna uhakika akipata kazi nyingine nayo hataifukuza pia!
 
Darubini,

kama nilivyosema hapo awali "Fong" inabidi aombe radhi na vizuri umesuggest njia mbali mbali za yeye kufikia hilo lengo na hatimaye kusaidiwa.............

Whaaaat?? no panick at all!!! haya endeleeni kutafuta na kudhani id za watu........the main point here is ikiwezekana huyu "Fong" asaidiwe.....hayo mambo sijui ya kuwa Ogah alikuwa na umri gani wakati gani...........nafikir ni irrelevant kwa hapa na kwa hii mada.........ukitaka kunifahamu just pm me.......

Mkuu,

Watu wanataka kukutambua? Wanatishia wana files zako za siri? Ukiona mtu anasema hivyo, jua hana kitu chochote.

Jamani kama watu hao wana uwezo huo mnaowapa, mbona nchi imejaa majambazi na wanashindwa kuwakamata? Mbona nchi imejaa mafisadi, wanashindwa kuwakamata mpaka Ernst & Young waingilie kati?
 
I may be missing something somewhere, hivi huyu Mwafongo mpaka wamkamie kiasi hiki atakuwa amefanya makosa kuliko hawa wafuatao?

1. Bibi Titi Mohammed - Muasisi wa Tanu aliehusika na mpango wa kupindua serikali akawekwa kizuizini na baadae kusamehewa kafa na heshima zote za kiserikali

2. Chief Abduallah Fundikira - Kinara na mwanzilishi wa upinzani Tanzania kasamehewa karudi CCM na ubunge wa dezo juu kafa na heshima zote za Serikali

3. Christopher Kasanga Tumbo - same as no 2 except hakupewa ubunge

4. Msururu wa wapinzani wakorofi akina Lamwai, Mtemvu, Nsanzungwanko, Dr Limbu, Dr Kaburu, Tambwe, Akwilombe, Makanga, Adama Malima, Njeru Kasaka, Michael Nyaruba, Salum Msabah, Raila Jidawi nk

5. Wahusika wa kesi ya uhaini ya Uncle Tom baadhi yao ni wanachama wa CCM

6. Wapinzani hai akina Mrema, Maalim Seif, Lipumba, Dr Slaa, Zitto, Mbowe (mpinzani?) nk

Hao wote hapo juu kwa namna moja au nyingine walikuwa au bado ni mwiba kwa serikali na hao wanaoitwa usalama wa taifa, iweje hao wasipewe kisago na hao so called usalama wa taifa badala yake ikiwa mzee Mwafongo tu?

Binafsi nilikuwa wala simjui mzee huyu kabla kuletwa kwa habari hii na naamini wengi wetu ni vivyo hivyo na kwa msingi huo nathubutu kusema hata kama alikuwa tishio kwa serikali basi ukorofi wake kwa kiwango chochote kile hauwezi kuwafikia hao watajwa wa hapo juu lakini mbona mambo yao ni shwari na mpaka leo wanapeta? infact Mbowe ana vimeo kibao na serikali ya mideni yake ya kwa mifuko ya jamii na bado anawakamulia serikali kama kazi.

Tumsaidie mzee wetu tu lakini hii habari ya kumtafuta mchawi sijui serikali, sijui usalama wa taifa ni upuuzi usio mithilika.
 
1.
Hawa ndugu zetu wa usalama wa taifa always liked to mingle with news reporters and even pretended to be reporters. But the people in the media knew who they were since they were not a part of them.
Usalama wa taifa, kazi yao ni kulinda taifa letu na hasa sisi wananchi n pia viongozi wetu, walikuzwa sana enzi za Mwalimu, lakini sasa yale yaliisha, tunaishi nao kwa kuheshimiana sio kwa kuogopana tena, unless one is mhalifu au anataka kupindua taifa, otherwise ni wananchi kma sisi wengine, ni hisia za kitumwa mambo leo kuwaogopa tuu bila sababu, tunajua kuwa hata hapa JF wapo, so what? Sisi kuendelea kumkoma nyani tu watu azima hawatishiwi nyau hapa!

2.
But, Ogah, you were probably too young back then, just a baby, when Mwafongo said that back in mid-1972. So you didn't even know him then. But sometimes it's wise to follow ancient wisdom telescoped telegraphically, and succinctly, into the adage: "Talk little, hear much."
Wooow!
Mkuu Ogah, weka vitu hapa mwanangu, hakuna file wala location, tunachojali ni hoja sio viroja, huyu Mwafongo, simjui vizuri ila ninafahamu kuwa kama anahitaji kusaidiwa na serikali, basi serikali iwasadie wengi, huko Mbeya, binafsi nimeshawan wananchi wengi ambao walikuwa kwenye nafasi kubwa serikalini lakini wameishia huko mashambani, ninamjua Udi Kaaabuka, alikuwa ofisa wa juu sana ubalozini kule Paris, nilipopita pale in the 1980s, na mara ya mwisho nilimuona kule Mwakaleli, Tukuyu anapiga matapu tapu kilabuni tena bila viatu miguuni, sasa serikali au Mkapa atasaidia wangapi? Majuzi tu hapa JF tuliwaktalia wale ndugu wa Mwalimu waliodai kuwa wametelekezwa, no wafanye kazi, kwa kweli binafsi siioni hoja ya msingi kwenye hii topic maana kama ni msaada wengi wanahaitaji sio huyu mtu mmoja tu!

Ukiyasoma vizuri maneo mengi hapa betweeen the lines ni kuwa kuna watu wanamfahamu huyo wafongo na huenda ni ndugu yao, wanajaribu kumpigia debe it is wrong kwa sababu wako wabongo wengi sana wanaohitaji kusaidiwa, lakini tukumbuke kuwa nguvu ni kazi na kujitegemea!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom