Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya External kwenda Majichumvi eneo la Migombani (Majichumvi) inayopita OBAMA BAR kuanzia Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mianzini kutokezea njia Panda ya Bonyokwa na Segerea inatutesa sana.

Mkandarasi alifunga njia kipindi chote cha mvua, tumeteseka vya kutosha maana diversion aliyotuelekeza tutumie hajairekebisha na imechimbika vibaya mno na imepita kwenye makazi ya Watu.

Bado mpaka leo ameifunga, tunatumia diversion hiyo hiyo mbovu na kaweka Walinzi Wamasai ambao cha ajabu wanaruhusu baadhi ya magari yapite kwenye njia Iliyofungwa kwa kupatiwa Fedha Kidogo.

Njia hiyo ni Muhimu kwa wakazi wa Kinyerezi na Bonyokwa wanaokuja Mjini, huyu Mkandarasi anatutesa zaidi ya Mwezi sasa na hakuna anayepiga kelele anafanya anavyojiskia huku watumiaji wa njia tukiteseka vya Kutosha!
 
Back
Top Bottom