Mjane aliyemwaga machozi mbele ya Rais Magufuli akabidhiwa nyumba yake

Huo sio utawala wa sheria. Meela ametumia vigezo gani?
Jino kwa jino, kwani huyo aliyedaiwa kumnyang'anya mke mkubwa alitumia vigezo gani? Mahakama zenyewe siku hizi usipokuwa na fedha hupewi haki heri tuende kwa mtindo wa kuwatumia tuliowapigia kura ndiyo saizi yetu.
 
Huo sio utawala wa sheria. Meela ametumia vigezo gani?
huyo mke mdogo huenda hakupewa na mahakama ila vikao vya jadi au serikali ya mtaa kwa kutumia hila. rc bila shaka ameona dhuluma akifuata falsafa ya hapa kazi tu na ndio maana mke mdogo ameambiwa kama hajaridhika aende mahakani. viva jpm.
 
Huyo mke mdogo alitumia nguvu km angefuata sheria basi mahakama ingekuwa upande wake kumtetea
 
Watanzania tuna tabia ya unafik sana....
Huyo mjane alipo dondosha chozi kwa kudhulumiwa, mlisema sana na kutoa maneno taka kwa viongozi wa serikali kutoingilia swala la mama huyo.
Leo mama huyohuyo mjane amerudishiwa malizake kwa wasimamizi wa serikali kuingilia kati swala la kudhulimiwa mama huyo, tena bado mnaongeeeea.
Kwakweli inafika wakati nashindwa kujua waTanzania tunataka nini sababu kilakitu tunapingatuuu
Hao ndio Bavichaaa bwana....walilalamika Seikali haisimamii haki,sasa wanapinga.Kwa kifupi huyo mama alishinda kesi ila mke mwenza na watoto wa kambo wakatumia udhaifu wake na uzee kumzuia kumiliki mali.Baada ya kuzungusha mikono sasa naona vijana wanakata mauno na baada ya kuchoka lazima wakae.
 
Yumkini akina mama hawa ni wa imani ya kiislamu; na uislamu una sharia zake katika suala la mirathi na wakf; na kwamba tayari kadhi yupo na anatimiza majukumu yake nchini. Kwa kuwa suala la mirathi na wakf ni suala la kiimani zaidi hususan katika uislam; Je, maamuzi haya ya serikali sio kuingilia dini? Itakuwaje endapo mke mdogo ataamua kufuata mkondo wa dini/kadhi kutafuta haki yake? Naona migongano isiyo ya lazima kati ya serikali na dini ikija kwa mbaali kwenye suala hili.

Kitu ambacho Serikali ilipaswa kufanya ni kuwashauri akina mama hawa hususan yule aliyelia kufuata taratibu stahiki katika kupata haki zao na kwa kumsaidia ingeweza kumwekea wakili au kumwomba Kadhi Mkuu kuingilia suala lile na kama ingeshindikana katika mkondo wa Kadhi basi mkondo wa sheria za nchi ufuatwe. Machozi yasiwe sababu au ishara kwamba aliyeyatoa ndiye mwenye haki. Huo ndio utawala wa sheria japo una machungu na gharama zake.
Hili suala huyo Mama alishinda kesi mahakamani ila mke mwenza na watoto wa kambo wakatumia uzee,upweke na udhaifu kufunga nyumba na kumzuia kulima.Siasa zitawauwa vijana.
 
Hao ndio Bavichaaa bwana....walilalamika Seikali haisimamii haki,sasa wanapinga.Kwa kifupi huyo mama alishinda kesi ila mke mwenza na watoto wa kambo wakatumia udhaifu wake na uzee kumzuia kumiliki mali.Baada ya kuzungusha mikono sasa naona vijana wanakata mauno na baada ya kuchoka lazima wakae.
Asanteni kwa ufafanuzi wa hili swala, maana kuna mdau mmoja huko juu amejitoa ufaham kana kwamba mama mjane amepewa shamba na nyumba yake kwa mkuu wa wilaya kuto kufuata sheria.
Jamaa niliamua kumpuuza tu kana kwamba alijifanya kwamba hajui jinsi sheria na haki zilivyokua zikidhulumiwa kwa nguvu ya pesa
huyo mke mdogo huenda hakupewa na mahakama ila vikao vya jadi au serikali ya mtaa kwa kutumia hila. rc bila shaka ameona dhuluma akifuata falsafa ya hapa kazi tu na ndio maana mke mdogo ameambiwa kama hajaridhika aende mahakani. viva jpm.
 
Watanzania tuna tabia ya unafik sana....
Huyo mjane alipo dondosha chozi kwa kudhulumiwa, mlisema sana na kutoa maneno taka kwa viongozi wa serikali kutoingilia swala la mama huyo.
Leo mama huyohuyo mjane amerudishiwa malizake kwa wasimamizi wa serikali kuingilia kati swala la kudhulimiwa mama huyo, tena bado mnaongeeeea.
Kwakweli inafika wakati nashindwa kujua waTanzania tunataka nini sababu kilakitu tunapingatuuu
Hujatujua kweli kuwa sie ni wanafiki reference::: Corruption corrupts: People are less honest in countries with fraud
 
Watanzania tuna tabia ya unafik sana....
Huyo mjane alipo dondosha chozi kwa kudhulumiwa, mlisema sana na kutoa maneno taka kwa viongozi wa serikali kutoingilia swala la mama huyo.
Leo mama huyohuyo mjane amerudishiwa malizake kwa wasimamizi wa serikali kuingilia kati swala la kudhulimiwa mama huyo, tena bado mnaongeeeea.
Kwakweli inafika wakati nashindwa kujua waTanzania tunataka nini sababu kilakitu tunapingatuuu
Kaka Kuna watu wana jifanya wanajua sheria humu yaaan wanabore kila upande wapo ka chaja za kobe
 
Kaka Kuna watu wana jifanya wanajua sheria humu yaaan wanabore kila upande wapo ka chaja za kobe
Na bahatimbaya hao wajuaji ukiwaambia wakuelezee fully saga story, utasikia anakujibu aliskia et.... na mwisho wa jibu atasema hajui sakata lilipo anzia hata kupelekea likafikia hapo lilipo fikia
 
Mkuu wa wilaya yupo sahihi, Kwanza huyo aliyedhurumu ni mke mdogo aliyeingilia ndoa ya mwanamke mwenzake, Kama kujenga hiyo nyumba aliijenga mke mkubwa hata kama ilikuwa ya udongo bado kiwanja kilikuwa cha huyo bi mkubwa, Mke mdogo alipoingia alikuta ama kuna nyumba au kiwanja cha mke mkubwa hivyo yeye mke mdogo hakuwa na haki kuishi pale badala yake alitakiwa amshawishi mwanaume wake wakanunue eneo jingine akajenge huko.na sio kuishi kwenye eneo la mwenzake na kufanya ujenzi hapo hana chake.
 
Mjane Aliyemwaga Machozi Mbele ya Rais Magufuli Akabidhiwa Nyumba Yake

Hatimaye mjane aliyemwaga machozi mbele ya Rais John Magufuli akidai kudhulumiwa mali ya urithi, amepewa nyumba na shamba baada ya Mkuu wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Crispin Meela kusuluhisha mgogoro wa umiliki wa mali hizo.

Hivi karibuni akiwa mjini Babati, Rais Magufuli alimuagiza Meela ahakikishe mjane huyo, Mwanaidi Mussa anapewa mali zake ikiwamo nyumba na shamba zilizokuwa zinadaiwa kuchukuliwa na mke mdogo kinyume cha sheria.
Meela alimkabidhi nyumba na shamba la ekari 2.5 mjane huyo juzi na kuagiza mke mdogo kama hakuridhika na uamuzi, akakate rufaa mahakamani.
Meela pia aliwataka wananchi kuacha kurubuniwa na watu wachache wenye maslahi binafsi na badala yake wafuate maelekezo yanayotolewa na vyombo vya sheria.

“Migogoro ya mirathi imeendelea kukithiri katika maeneo mengi nchini kutokana na watu kutofuata sheria za mirathi na wengine wakitaka kunufaika na mali zinazoachwa na marehemu,” alisema Meela.

Mwanaidi ambaye amezeeka, alidai kwa muda mrefu amewaomba viongozi wa Serikali ya mtaa anaoishi wamsaidie, kutatua tatizo lake lakini walimpuuza.
Mke mdogo, Asia Musa alidai kuwa nyumba hiyo aliyokabidhiwa Mwanaidi, aliijenga na mumewe kauli ambayo ilikinzana na ya mke mkubwa aliyedai kuwa wakati Asia anaoelewa alikuta nyumba ameshaijenga na mumewe.

My Take;
MaDC na MaRC tunaomba msimamie haki katika maeneo yenu ninaamini kuna wajane,wanyonge na mayatima wengi wanateseka.

maraisi wote waliofeli kuiletea jamii maendeleo walikuwa wanalenga kutatua matatizo ya mtu mmoja mmoja.

hivi wajane ni wangapi nchi hii na kwa staili hii ya kila mmoja kumlilia raisi ndio atatuliwe matatizo kweli tutafika?

binafsi nilitegemea agizo la kwanza lingeelekezwa kwa wizara zinazohusika kama ni mambo ya ndani au ustawi wa jamii au sheria na katika kuhakikisha matatizo ya wajane yanatafutiwa ufumbuzi haraka ndani ya mwaka mmoja pengine kusitokee mjane ambaye anasumbuliwa hajui la kufanya au anakosa haki yake.

na kwa huyu ingekuwa ni jambo la mwisho.

huyu kapewa lakini wengine mpaka watakapopata nafasi ya kumlilia raisi ndio wapate haki zao? si swala la kila mmoja wetu kusema anayofikirimkujibu bali mwenye nukuu ya raisi akitoa maagizo ndio aweke na kama hajaagiza badala ya kumtetea mkumbushe atoe maagizo.
 
Hao ndio Bavichaaa bwana....walilalamika Seikali haisimamii haki,sasa wanapinga.Kwa kifupi huyo mama alishinda kesi ila mke mwenza na watoto wa kambo wakatumia udhaifu wake na uzee kumzuia kumiliki mali.Baada ya kuzungusha mikono sasa naona vijana wanakata mauno na baada ya kuchoka lazima wakae.

Sikubaliani na sentensi yako ya mwisho ya "....mauno..." Hiyo sasa ni kejeli.
 
Note our argument, we are insisting on rule law. Let the judiciary dispense justice not magufuli
 
Back
Top Bottom