TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

BUKOBA MANISPAA YANG'ARA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI

332592744362a9417c828198626ca9c7.jpg


Pongezi kwa Meya, Naibu Meya, Mkurugenzi, Mbunge, Waalimu, Wazazi na wana Bukoba wote
 
TAARIFA YA MRADI DECEMBER, 2016

Utangulizi

Tushirikishane ni mradi unaowahusisha viongozi wa kuchaguliwa (mbunge na madiwani) serikali (halmashauri) na wananchi katika kurahisisha upatikanaji wa maendeleo. Wadau wakuu wa mradi huu ni Halmashauri ambayo ndiyo kitovu cha mipango ya maendeleo na utekelezaji wake, Mbunge ambaye ni msimamizi wa serikali (halmashauri), Jamiiforums ambao ni wasimamizi wa mradi na Wananchi.


Utekelezaji wa mradi unaanzia Halmashauri ambayo inasimamia miradi yote na inayotokana na vipaumbele vyetu ambavyo ni (1) Ujenzi wa Stand Kuu ya Mabasi, ujenzi wa Soko la Kuu na Soko la Kashai (2) Urasimishaji Makazi (3) Mikopo kwa Wanawake na Vijana, na (4) Bima ya Afya. Pia inatoa taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vipaumbele vyote. Mbunge katika mradi ni daraja kati ya manispaa na wananchi katika kuweka msukumo wa utekelezaji na kutoa taarifa kwa wananchi. Halmashauri na mbunge wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Jamiiforums ni mfatiliaji wa shughuli zote za mradi (utekelezaji wa vipaumbele) inatoa taarifa kwa wananchi juu ya mradi


TATHMINI YA MRADI YA MIEZI MITANO (5)

Mafanikio

(i)Utekelezaji wa mradi ulianza kwa changamoto ya upatikanani wa taarifa, awali ofisi ya mbunge na mbunge kwa ujumla hawakuwa wakielewa wajibu wao katika mradi hivyo ushirikiano wao haukua wa kuridhisha hivyo kusababisha ugumu katika kupata taarifa. Baada ya miezi mine (4) ya utekelezaji wa mradi, ofisi ya mbunge na mbunge walielewa wajibu wao na kuweza kushiriki vyema katika kutoa taarifa ya mradi

(ii)Swala la halmashauri kutoa taarifa kwa wananchi ni mtambuka na mradi umekua ukisisitizo hilo kwamaana ya kwamba taarifa ni mali ya wananchi hivyo inapasa ziwafikie ili waweze kushiriki. Lakini pia, ushirikishwaji wa wanannchi katika maswala ya maendeleo yao ni dira ya halmashauri ya manispaa ya Bukoba. Mradi umejitahidi kuwaelimisha viongozi wa halmashauri ikiwemo na mbunge juu ya swala hili na kuna mafanikio yameanza kuonekana mfano;

(iii)Mbunge na naibu meya wameanza kutoa taarifa mbalimbali na kuongelea maswala yanayohusu manispaa kupitia akaunti zao za facebook

(iv)Mbunge ameahidi kufanya mkutano kwa kila mwezi kwa kualika vyombo vya habari ili kutoa taarifa

(v)Mbunge ameahidi kuhakikisha kila kikao cha baraza la madiwani kuwa kinatangazwa katika vyombo vya habari na magari ya matangazo ili wanachi wafahamu na kuhudhuria

(vi)Mbunge ameahidi pia kuwa kila kikao cha baraza la madiwani kitakua kikieushwa katika televishen ya Bukoba (Bukoba Cable Network) ili wananchi ambao hawataweza kuhudhuria kikao hicho waweze kufahamu nini kinaendelea

(vii)Ushiriki na ufatiliaji wa wananchi wa mradi huu unazidi kuongezeka, mfano nisipoweka taarifa katika mkanasha kwa muda kadhaa watu wanaulizia sababu za kufanya hivyo. Na pia idadi ya watu wanaochangia na hata kupitia mkanasha wetu imekua ikiongezeka

(viii)Viongozi wamefahamu kuwa wananchi wanauwezo na nafasi ya kuwahoji kupitia mradi huu

(ix)Mkutano wa BUMUDECO 2017 ni moja ya mafanikio ya mradi pia


Changamoto

(i)Bado kunachangamoto ya meya wa manispaa kukubali mradi vyema na kushiriki vyema hasa katika swala la taarifa

(ii)Msukumo na ushawishi wa mbunge kwa halmashauri katika utekelezaji wa vipaumbele bado hauridhishi

(iii)Viongozi wa kuchaguliwa halmashauri ya manispaa ya Bukoba ni waonga wa kuongea na wananchi kwanjia ambazo ni rafiki na zinafikika kwa wengi kama mitandao ya kijamii. Mfano, kuna ambao wako kwenye magroup ya WhatsApp lakini hawawezi kueleza wala kujibu chochote. Tunao mkanasha wetu maalum wa Jamiiforums lakini wameshindwa kuutumia kuzungumza na wananchi waliowachagua. Viongozi wengine hawafahamu kabisa wala hawatumii mitandao ya kijamii

(iv)Njia za utoaji taarifa kwa wananchi bado ni za kizamani, haziendani na kasi ya teknolojia iliyopo. Mfano ni website ya halmashauri ambayo imetoa taarifa kwa mara ya mwisho 2012



TAARIFA

1. Ujenzi wa Soko Kuu

Matarajio katika ujenzi wa soko ilikua mpaka kufikia Disemba zabuni iwe imetangazwa na mshindi ametangazwa tayari. Pia tulitarajia kuwa wafanyabiashara wawe tayari wamehamishiwa katika soko la muda ili kupisha ujenzi. Ila haijawa kama matarajio yalivyokua kwa maana hata mazungumzo na muwekezaji hayajakamilika bado kwa maana bado andiko halijakamilishwa kutokana na halmashauri kushinwa kulipa ile million 50 iliyoitajika na mshauri OGM ili kukamilisha andiko. Lakini pia mbia na namna ya kupata 30% ya pesa inayotakiwa kutolewa na halmashauri bado haijafahamika

2. Ujenzi wa Stand
Bado taratibu zinafanywa ili kukaribisha wawekezaji wadogo wadogo kujenga kwa kufuata ramani na kwa mkataba maalum na halmashauri. Matarajio ilikua zoezi hilo litangazwe Disemba hii

3. Ujenzi wa Soko la Kashai
World Bank wamekubali kufadhili ujenzi wa soko hili. Matarajio ilikua ni zabuni kuwa imetangazwa na mzabuni kupatikana ifikapo kabla ya kuisha Disemba hii, lakini bado mabo hayo hayajafanyika

4. Mikopo kwa Wanawake na Vijana
Vijana na wanawake wanaendelea kupata mikopo katika SACCOS zilizoainishwa

5. Urasimishaji Makazi
Zaidi ya nyumba 1300 zimekwisha pata mchoro toka mradi uanze na zoezi la uchukuaji data (mipaka ya viwanja kwaajili ya mchoro wa TP) na kuhamasisha uchangiaji linaendelea

6. Bima ya Afya
Zoezi hili limekwama kwasababu mbunge hajaelekeza, kuhimiza halmashauri jinsi rahisi ambayo tulikubalia katika utekelezaji wa hili zoezi. Lakini kwa muda uliobaki inawezekana kufikia malengo kama litafanyika

HITIMISHO

Utekelezaji wa vipaumbele vingi umekua ukisuasua lakini bado kuna muda wa kufikia malengo kama kutakua na jitihada za ziada katika kufanikisha yote.

Imetolewa na

Afisa Habari - Bukoba

Tunaomba updates za tokea dec-january wadau, kukaa kimya haikuwa lengo letu juu ya masuala ya maendeleo
 
MWONEKANO WA MJINI WA BUKOBA MWEZI FEBRUARY

69514a96224f1b7c6156448d20e0187b.jpg
b0db4f7bc7603eb4feae2331c4368276.jpg
218e182b694ef3b6c45838a55792ea3e.jpg
5346d327abd9c7ad7b1a27fbc1b73020.jpg
b25b36f29bbc8fecb0fd94447fbe572d.jpg
Dada wewe ni katibu, mkikaa kwenye vikao vyenu kwani huwa haya hamyakumbuki kuyajadiri make kuishia tu kuyaweka hapa Jf wala sidhani kama itaweza kubadirisha kitu. Ungetusaidia kujua nyie mkikaa huko haya mashimo huwa mnayachukuliaje?
 
Ahadi mbona hazijaanza kutekelezwa? Huyu mbunge nini kimemsibu?
Ndugu yangu utaendelea kukubali kwamba huyu mbunge watu waliingia mkenge. Mie sijawahi kumkubali na sitakuja nimkubali. Kati ya watu hopeless na ambao watakuja kuonekana walofeli kupita maelezo ni pamoja na huyu jamaa

Ni hopeless na useless kupita maelezo, ukitaka kujua hili angalia mahandaki ya mjini, angalia mitaro ya maji, angalia U.wa kaitaba ndani ulivyo kichaka, ile miradi mikubwa achana nayo kwani wala si saizi yake na hatoiweza. Ila alivyo wa ajabu na yeye anadai waruhusiwe kuandamana, sasa unajiuliza hivi watu walimchagua ili wale maandamano
 
Sasa kwa mwendo wa hivi kuna faida gani wananchi hapo kulipa kodi? Kuna faida gani ya kumchagua mbunge wa upinzani? Kuna tofauti gani kati ya CCM na upinzani? Kuna faida gani na ni nini kazi ya baraza la madiwani hapo manispaa? Serikali ya mkoa kwa ujumla wanapata wapi uharari wa kuendelea kuwepo ofisini?
 
*IJUE KESI YA KIKATIBA NAMBA 9 YA JAMII MEDIA (HUKUMU NI TAREHE 22, FEBUARI 2017)*

*UTANGULIZI:*

Tarehe 4 mwezi tatu mwaka 2016 Kampuni ya Jamii Media inayoendesha mtandao maarufu wa JamiiForums ulifungua Kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania kesi namba 9 ya mwaka 2016.

Kesi hiyo inatarajiwa kutolewa hukumu kesho tarehe 22 Febuari saa 6 mchana.

*HOJA ZA JAMII MEDIA:*

Kesi hii ilikuwa na hoja zifuatazo;
- Kupinga matumizi ya kimabavu ya kifungu cha 32 cha sheria ya Makosa ya Kimtandao(CyberCrime Act), ambacho kimenainika kutoa nguvu kubwa kwa Jeshi la Polisi kutoa amri ya uchunguzi wa taarifa za siri/binafsi za watumiaji wa mitandao.

- Kupinga matumizi ya kifungu cha 38 cha Sheria ya Makosa ya Kimtadao ambacho kinapingana na haki ya mtu kusikilizwa endapo kifungu cha 32 kitakuwa kimetumika. Kifungu cha 38 kinalipa Jeshi la Polisi uwezo wa kwenda mahakamani na kusikilizwa bila uwepo wa upande wa pili (Exparte).

*NINI KINAWEZA KUTOKEA?*

Inawezakana Mahakama ikadai kuwa imeona kifungu cha 32 kiko sawa kikatiba ila ikumbukwe Jamii Media wanapinga 'Matumizi mabaya' ya kifungu hicho. Hoja yao inakolezewa kwa madai kwamba Jeshi la Polisi lilianza kutumia kifungu hicho bila kanuni kutungwa. Wanasheria wao wanasema kifungu hicho cha 32 kinakinzana na haki ya faragha, na uhuru wa kujieleza.

*YALIYOTOKEA KATIKATI:*

Katika hatua za awali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliweka mapingamizi ya awali ya kisheria sita, ambapo moja ya mapingamizi mwasheria wa serikali alisema shauri hilo namba 9 halikustaili kuwa shauri la kikatiba. Tarehe 24 Agusti 2016, Mahakama Kuu iliyatupilia mbali mapingamizi yote sita ya awali na kutoa amri kesi hiyo kuendelea kusikilizwa.

*KWANINI KESI YA KIKATIBA?*

Toka kutungwa kwa Sheria ya Makosa ya Kimtandao 2015, Jeshi la Polisi kupitia Kitengo chake cha Makosa ya Kimtandao "Cybercrimes Unit" na cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai "Criminal Investigation Department(CID)" wanadaiwa kuwa wakituma barua mbalimbali wakimtaka Mkurugenzi wa JamiiForums kuwapa taarifa za siri/binafsi za wateja wake kwa lengo la 'kufanya uchunguzi' na 'kuwafungulia kesi' baadhi ya watumiaji wa mtando huo. Polisi walikuwa wakituma barua hizo chini ya kifungu cha 32 cha Sheria ya Makossa ya Kimtandao.

Katika barua hizo zaidi ya kumi, zote zilikuwa zikitaka taarifa watu walioandika masuala ambayo Jamii Media wanadai zina maslahi mapana ya kitaifa(Public interest) na nyingne zikiwa za kisiasa.

Katika barua zote Jeshi la Polisi ziliweza kujibiwa na wanasheria wa Jamii Media, huku wanasheria wakionesha nia ya kutoa ushiriakiano endapo Jeshi la Polisi lingesema wazi makosa yaliyokuwa yametendeka na kama wangeeleza taarifa hizo za wateja zinaenda kutumika kwa maslahi gani. Hii ilifanyika kwa nia njema (Good faith) ili kuiwezesha JamiiForums kuangalia uhalali wa kisheria kabla ya 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi hilo. Mwanasheria pia alinukuliwa nyakati kadhaa akisema watumiaji wengi waliokuwa wakitafutwa walikuwa wameandika habari au kutoa taarifa za rushwa, ufisadi na ukwepaji kodi na hivyo aliishauri Jamii Media kuwaona kama waibua maovu “Whistle Blowers” wenye nia njema kwa nchi.

*KWANINI USHIRIKIANO ULISHINDIKANA!?*

JamiiForums ina wajibu wa kulinda taarifa za watumiaji wake kisheria na Kikatiba, lakini pia wanatambua wana wajibu wa kisheria kutoa ushiriakiano kwa Mamlaka kama kuna taarifa watahitaji, lakini lazima maombi hayo yafanywe chini ya amri zilizo halali na zinazofuata sheria na kuzingatia haki za binadamu.

Pamoja nia ya kutaka kutoa ushirikiano iyoonyeshwa na Jamii Media kwa Jeshi la Polisi katika barua zao zote zaidi ya kumi, Polisi walikataaa kutoa taarifa juu ya nia ya Jeshi hilo kwa wateja wao. Polisi walizidi kutuma barua na mnamo tarehe 4 Februari 2016, Jeshi la Polisi lilimuandikia Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, ndg Maxence Melo barua ya kuashiria kuwa lina nia ya kumshitaki chini ya kifungu cha 22 kwa kuzia uchunguzi wa Jeshi la Polisi.

*UAMUZI WA JAMII MEDIA:*

Baada ya Jamii Media kuona kuna vitisho vya kufunguliwa mashitaka walishauriana na wanasheria wao na kuamua kufungua kesi ya kikatiba.

Toka kesi ifunguliwe, Jeshi la Polisi walisimama kwa muda kuandika barua hadi mwezi Septemba 2016 walipomhoji Maxence juu ya Barua walizokuwa wakimwandikia na akiwanyima 'ushirikiano'.

Ulitokea ukimya wa Polisi tena hadi Disemba 13, 2016 walipomkamata ndg Maxence Melo na kumnyima dhamana kwa siku takribani nne(4) na kumfungilia mashitaka chini ya kifungu cha 22 huku Jeshi likijua wazi kuna kesi ya Kikatiba kuhusiana na suala hilo.

*KUHUSU HUKUMU:*

Hukumu ya kesi hii inasomwa kesho tarehe 22 mwezi Febuari 2017 chini ya jopo la Majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Mtukufu Koroso. Majaji wengine wanaosimamia kesi hiyo ni Jaji Mtukufu Kitusi na Jaji Mtukufu Khalfani.

*JE, NINI HATMA YA UHURU WA KUJIELEZA MITANDAONI?*

Tukutane Mahakamani!
 
Hizo barabara mpango wake ukoje kabla hatuaanza kujadiri ya mahakamani ambayo tunajua ugumu wake kwasababu huko ni sheria zaidi. Ya hapo manispaa na mipango ya jamaa (masoko n.k) viliishia wapi?

Na vipi kuhusu mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 yakoje na yale yaliyopitishwa 2016/17 utekelezaji wake miradi imefikia wapi?

Ndugu zetu, wananchi wanataka hayo, tusaidieni kujua hayo kwanza
 
ZOEZI LA URASIMISHAJI MAKAZI KATA KASHAI

Zoezi hili linaendelea vizuri Kashai, tayari nyumba 60 zimekwishapimwa katika hatua za awali za majaribio. Vikundi vitatu vinavyounganisha mitaa mitatu mitatu tayari vimesajiliwa. Na tayari uhamasishaji unaendelea kwaajili ya wananchi kulipia fedha kwenye akaunti maalum.

Pichani ni kipeperushi na Mheshiwa diwani Kabaju akisambaza vipeperushi kwaajili ya kuhamasisha wananchi kuchangia

da6e70f80c70f90aba9cad7ab26d33ae.jpg
7b61ece703e5b698654befd56ae327f9.jpg
04b03928763b2ad24915771cbd73a987.jpg
6beed02a8a32f7f3628fa7f07f28a9cc.jpg
a891068d5af4135d2b71cc2edbd9d595.jpg
f5af2636ec5a64fc80c2cb6b9424928e.jpg
67c378042f8f1f9b2c0d0239edd76e9a.jpg
d00a516204dfa08a5fd2564a9d4e05b3.jpg
8472cb09002065f748503f57bf576e03.jpg
 
Ndg Rweye hakika hujamtendea haki mbunge wa bkb mjini. Kumwita hopeless mtu ambaye hahusiki moja kwa moja na utekelezaji wa miradi haifai. Mbunge huyu amesaidia sana kuhamasisha wadau ikiwemo serikali kuu, mitaa, wawekezaji, diaspora ya bkb nk. Sasa unamlaumu vipi mpk matatizo ya uwanja wa kaitaba ambao ni jukumu la manispaa na tff? Mkurugenzi wa manispaa na uongozi wa mkoa wa washirikiane na mbunge na madiwani bila kujali tofauti zao kisiasa kuleta maendeleo kama mikoa mingine. Na tuwe wastaarabu ktk matumizi la lugha ktk social media.
 
Maoni yangu ni tofauti kidogo ni hali ya uchafu wa mwili na mavazi waliyo nayo wananchi wengi wa Bukoba. Ni aibu watu wetu wamegeuka kuwa wachafu kiasi hicho na hakuna hatua zinachukuliwa na viongozi kuanzia wa kuchaguliwa mpaka wa serikali. Vitoto vya shule za msingi ni vichafu kama 'washuti' wa miaka ya70 na 80.

Ni ombi langu kwamba mabwana na bibi afya wakishirikiana na viongozi wengine ondoeni aibu hii ambayo inatia sana. Bukoba iliyo kuwa na watu wasafi na maridadi sasa utadhani watu wake walio wengi wanatoka ktk kambi za wakimbizi.
 
Ndg Rweye hakika hujamtendea haki mbunge wa bkb mjini. Kumwita hopeless mtu ambaye hahusiki moja kwa moja na utekelezaji wa miradi haifai. Mbunge huyu amesaidia sana kuhamasisha wadau ikiwemo serikali kuu, mitaa, wawekezaji, diaspora ya bkb nk. Sasa unamlaumu vipi mpk matatizo ya uwanja wa kaitaba ambao ni jukumu la manispaa na tff? Mkurugenzi wa manispaa na uongozi wa mkoa wa washirikiane na mbunge na madiwani bila kujali tofauti zao kisiasa kuleta maendeleo kama mikoa mingine. Na tuwe wastaarabu ktk matumizi la lugha ktk social media.
Ndg. yangu sina tatizo na mtu, ninawashwa washwa hivi. Hivi ni kweli kwamba wewe unasimama badala yake ama wewe unaleta yale unayoyakusanya mwenyewe katika pita pita zako? Hatutaweza kuendelea wala kupiga hatua kama tutafika mahala tukaogopa kukosoana na ifahamike, tunakosoa palipopinda ili parudi kwenye mstari.

Nakupa mfano tu. Kupitia mabandiko yaliyoko hapa mbunge mwenyewe alikiri kwamba sasa atakuwa smart katika kuleta habari za maendeleo ya miradi yetu mikubwa, nioneshe update hii kwa miezi miwili iliyopita, iko wapi?

Alihaidi atakuwa mtumiaji mzuri sana wa mitandao na vituo vya redio kila mwezi kuhabarisha umma juu ya maendeleo katika jimbo lake, ni wapi umeona? hapa Jf ofisi yake iko live tokea?

Haya, hapa Jf kupitia kwa Dada Happy kuna habari inayomnukuu meya akisema tenda ya barabara mjini ishatangazwa lakini tokea mda huo mpaka leo hatuoni chochote zaidi ya madimbwi yaliyopigwa picha na kutuletea hapa Jf hata hapo juu yapo ya jana yakionesha uzuri wa stand yenu ya mabasi, utadhani ni machimbo ya madini kule Geita. Ni kwanini hizo picha hapa, simply ni kuonesha failure katika uongozi.

Hapo juu mkuu Timbilimu kauliza ni vipi hata wakazi tu wa mjini wanaonekana mavazi yanachakaa kuliko uko nyuma. Barabara ni chafu na sasa watu nao wanakuwa hivyo, viongozi wako wapi kuanzia wa kuteuliwa mpaka wa kuchaguliwa? Hivi hii ndo ramani mnayoitaka na kwamba tunyamaze? Unataka tuache kuwahoji madiwani na wabunge kuhusu haya eti twende kwa watendaji wa manispaa. Wewe unaanzaje kwenda kwa mkuu wa idara kuulizia hayo mambo wakati wawakilishi wenu mliowachagua wapo, wa kazi gani sasa kama maisha yenu hayawaumi?

Kama ni kusema halafu tukaonekana tuna tatizo na mbunge basi acha na iwe hivyo, na msituletee tena hizi picha za hivi. Kapige kisiwa cha musira na ndege wazuri walioko huko ili tuongelee uzuri wao kuliko kutuletea picha zenye taswira mbovu hivi na bado hamtaki tuulizane. Sasa kupitia kwako mh. na kwa niaba ya mbunge, tunaomba utupatie yafuatayo ili tusiendelee kuonekana wasumbufu kwa mbunge wako.

1. Ripoti ya stand, soko kuu na lile la kashai vilikofikia leo
2. Ripoti ya miradi ya bajeti ya 2016/7, iliyotekelezwa na inayotekelezwa
3. Muhtasari wa bajeti rasmi iliyopitishwa kwa mwaka 2017/8
4. Mihtasari ya vikao anavyokaa mbunge na wanajimbo kwa mwezi Jan/Feb, 2017.

Sie tunaoonekana tunamsema vibaya mbunge tunataka hayo, na kimsingi yako ndani ya uwezo wake. Na ni vizuri umshauri pia, hatua zozote anazochukua asifanye sirini. Aziweke wazi kwenye mitandao kama alivyotuhaidi ili tuone na tumpongeze panapostahili kuliko kufanya kimya kimya. Jf hatuoni, Fb hatuoni na si popote pia yanakoonekana. Awe digital aachane na analogy na ni vizuri zaidi aanze kutumia 4G.
 
Back
Top Bottom