Mizengo Pinda Waziri mkuu!

Kwa maoni yangu..ninaweza kusema kuwa kuna sababu mbili ambazo zinaweza kuwa zilitumika na Kikwete kumteua Pinda;
Moja ni uzoefu wake kwenye masuala ya kisheria..hii itamsaidia kuwaleta mafisadi mbele ya sheria bila kuvunja sheria!Hapo wananchi tuko upande wake!
Sababu ya pili inatia shaka..Huyu Mh Pinda kwanza kabisa ni mjamaa..then usalama wa taifa!Hizo sifa zinamfanya kuwa ni mtu msiri na unayeweza kumtegemea kwenye kurudisha nidhamu na kurekebisha loop holes ambazo zilisababisha news za ufisadi na mikataba mibovu kuvuja!Huyu jamaa anajua mambo mengi sana!Ila taarifa zinadai kuwa anaonekana ana mawazo mengi sasa na kwakuwa ana sifa ya uadilifu..then anaona itakuwa mzigo mkubwa kuwashughulikia mafisadi ambao amekiri kuwa ni watu wake wa karibu..kama vile Chenge etc!Htaweza kuchukua ushauri mwingine zaidi ya ule wa Mzee Mwiru!Akiwa mjanja atachukua ushauri wa Butiku ambaye wanafahamiana vyema na walifanya kazi pamoja chini ya Mwalimu kwa muda mrefu!

Jamani tunasema Pinda ana uzoefu na mambo ya kisheria kama vile ame practice law au aliuwa anafanya kazi za sheria, for all we know alikuwa anapanga mafaili ikulu mpaka 2000 alipokuwa mbunge.
 
Jamani tunasema Pinda ana uzoefu na mambo ya kisheria kama vile ame practice law au aliuwa anafanya kazi za sheria, for all we know alikuwa anapanga mafaili ikulu mpaka 2000 alipokuwa mbunge.

Kam mtu mwnye LLB anapanga mafaili ikulu sasa sijui wenye diplama za mzumbe IFM na vyeti vya Form six na NABOCE wanafanya nini pale Ikulu.

Inawezekana si chaguo la wengi na shepu yake si swano kama ya Lowassa, lakini ni vema tutambue kwamba hatutajua uwezo wa mtu mpaka pale akianza kufanya vitu vyake.
 
Jamani tunasema Pinda ana uzoefu na mambo ya kisheria kama vile ame practice law au aliuwa anafanya kazi za sheria, for all we know alikuwa anapanga mafaili ikulu mpaka 2000 alipokuwa mbunge.
Si amesomea sheria?sasa unafikiri walikuwa hawamuulizi masuala ya kisheria wakati akiwa ofisini?Hiyo ndiyo shughuli yake professionally..so its obvious ana knowledge ya kutosha kuhusu mambo ya kisheria!Halafu kumbuka alikuwa downa low cause hiyo ndo style ya wanausalama wa taifa!They always keep it in a "low low" Na sio necessary kwamba hapendi makuu!
 
Si amesomea sheria?sasa unafikiri walikuwa hawamuulizi masuala ya kisheria wakati akiwa ofisini?Hiyo ndiyo shughuli yake professionally..so its obvious ana knowledge ya kutosha kuhusu mambo ya kisheria!Halafu kumbuka alikuwa downa low cause hiyo ndo style ya wanausalama wa taifa!They always keep it in a "low low" Na sio necessary kwamba hapendi makuu!

Unaweza kusoma sheria halafu kupelekwa ikulu kuwa clerk wa intelligence unit, kusoma reports za Reuters na kuandika briefings.

How much legal experience does one get from that? Injabidi tujue alifanya kitu gani!
 
Je, Kwa kumteua Mizengo Pinda, JK Kaua hoja ya Ukaskazini kwenye uongozi wa TZ??

Hoja ya ukaskazini imetoka wapi? Kawawa mkaskazini? Mwinyi Mkaskazini? Salim Mkaskazini? Malecela Mkaskazini? Kikwete Mkaskazini? Mkapa Mkaskazini?
 
Unaweza kusoma sheria halafu kupelekwa ikulu kuwa clerk wa intelligence unit, kusoma reports za Reuters na kuandika briefings.

How much legal experience does one get from that? Injabidi tujue alifanya kitu gani!

Mkuu Pundit,

Heshima mbele mkuu!

Lakini inaonekana MP alipractice sheria kwa AG kabla ya Ikulu. have you considered that too? Na Intelligence alifanya kwa 4 yrs tu, inavyoonekana kwenye records.
 
..tuna Raisi Mchumi nakini haja-practice ktk taaluma yake.

..huyu naye ni Mwanasheria lakini inaelekea ame-practice kwa miaka 2/3 tu.

..tulikuwa na Waziri Mkuu bwana shamba, aliye-practice na hata akiwa waziri mkuu aliendelea kulima. Hatukuridhika.

..nafikiri haitofika mahali tutaridhika na yeyote. after all huyu ni Waziri Mkuu siyo Mwanasheria Mkuu.
 
Siku hawa viongozi waliopo madarakani in this case pamoja na muheshimiwa Pinda, watapo kubali ukweli kuwa, nyerere ndie alyeifisadi hii nchi kwa maamuzi yake mabovu, yote kwa muono wangu, kwani sijaliona jema hata moja la nyerere. Hapo ndipo kutakuwa na mabadiliko ya kweli. Haya masalia ya warithi wa nyerere ndio yanayozidisha matatizo kwenye nchi hii, kwani ikiwa kiongozi yeyote ataetuongoza anamuona nyerere hakuifisadi nchi hii, ingawa alituwacha tu masikini wakutupwa, basi sijui, sijui kiongozi kama huyo anajuwa ufisadi ni nini! Simply, kinachotakiwa ni viongozi wenye muono tofauti na itikadi za kinyerere. Za kumfanya kila mmoja awe masikini, masikini wa kutupwa.

Leo Tanzania, miaka karibu hamsini baada ya uhuru, ukitazama huduma za afya unatamani kulia na wenyewe wenye nchi hata mafuwa wanakwenda kujitibu nje ya nchi, wote kuanzia nyerere mwenyewe mpaka leo. Maji, wakati nyerere anapewa hii nchi, tulikuwa tukinywa maji ya bombani bila kuchemsha, leo inawezekana hilo? Elimu, hatari tupu tunaona ni hao watoto wa wenye nchi ndio wanapelekwa kusoma nje ya nchi, kwa nini? elimu yetu ni duni na wanajuwa hilo. Aaah alimradi kila kitu hohehahe, kuanzia uongozi mpaka huduma zote, nyerere kaziacha nyang'a nyang'a na bado tunaimba kila siku "baba wa taifa" mimi nasema tuimbe "baba wa ufisadi". Pinda anatokea huko-huko, hakuna jipya ataloleta. Labda akubali kuwa nyerere ndie alikuwa muasisi wa ufisadi na fisadi mkuu wa kwanza aliyeitia nchi hii kwenye lindi la ufukara na umasikini na uomba-omba na ufisadi wa kina. Akilijuwa na kukiri hilo, hapo kweli tutaona mabadiliko.
 
Zomba,
. Hapo ndipo kutakuwa na mabadiliko ya kweli. Haya masalia ya warithi wa nyerere ndio yanayozidisha matatizo kwenye nchi hii, kwani ikiwa kiongozi yeyote ataetuongoza anamuona nyerere hakuifisadi nchi hii, ingawa alituwacha tu masikini wakutupwa, basi sijui, sijui kiongozi kama huyo anajuwa ufisadi ni nini! Simply, kinachotakiwa ni viongozi wenye muono tofauti na itikadi za kinyerere. Za kumfanya kila mmoja awe masikini, masikini wa kutupwa.
Katika kundi la mafisadi, nakuomba nitajie mtu hata mmoja wa Nyerere kama sio creation ya JK..
Je, Sio nyie mlokuja na ari nguvu na kasi mpya?.. mkisema Nyerere alituchelewesha sasa leo mnawahi na mbio za marathon kwa kasi ya mita 100, tatizo limekuwa Nyerere....
Walopiga kura na kumsifia Lowassa, Karamagi, Msabah, na wengineo kina nani?.. Je umesahau mzee spika Pius Msekwa alivyotolewa si nyie mlosema hana kitu na kumsifia Sitta - kwani Nyerere hakumwona?.
Ndugu yangu tatizo sio watu ni direction tuliyochukua...
 
Zomba,

Katika kundi la mafisadi, nakuomba nitajie mtu hata mmoja wa Nyerere kama sio creation ya JK..

Je umemsahau Msuya, Mungai, Mkapa, Lowassa,Kinana...hawa wote ni kapu la Nyerere wamefugwa sasa wamekomaa..ask Ngombale hataki kabisa sura mpya ktk CCM.
 
MMASAI,

Tunachozungumzia hapa ni kipi haswa?......watu tuliokuwa serikalini toka wakati wa Nyerere ama kipi maanake hata huyo Freeman. Dr.Slaa, Zitto wote ni wajukuu wa Nyerere...hata huyu Waziri mkuu mpya ni mtoto wa Nyerere hivyo uzazi hautengenezi akili ya mtoto. Nyerere aliwakunja wakingali wadogo mkawatoa ktk dini, haramu ikiwa halali .. sasa wamejua tamu ya sukari, usenge sii haramu tena lakini lawama ni za Nyerere mzazi!..
List yote uliyoitaja ni matunda ya kile tulichopanda sisi wenyewe...hawakuwa na chochote hadi mwezi wa 10,1999..

Kuamini kwetu kwamba Ujamaa na hadithi zote za Kujitegemea ni dhana ambayo haiwezi kufanya kazi ktk dunia ya leo..Sasa imefanya kazi mnarudi nyuma kumtazama mzazi ambaye hakuwaambia kuweni mafisadi...
Swala la Lowassa linatokana na mfumo mbovu wa CCM mpya hii ya kina mtandao na Azimio la Zanzibar. Viongozi wote sii chama CCM wala chama cha mtaani, fedha mbele na tumejenga imani kuwa fedha ndio msingi wa maendeleo....
We all think that way! lakini sio malezi ya mwalimu.
 
Ushauri wa bure kwa mheshimiwa Pinda, waziri mkuu wa TZ. Jitahidi sana na usiruhusu mfanyabiashara Mhindi yeyote akakukaribia karibu. Fuata nyayo za mwalimu ambaye pamoja na kutokuwa mbaguzi lakini hakuwapa nafasi ya kumsogelea ukiondoe wafanyakazi wa serikali.

Nimekuwa nikifuatilia viongozi wetu tokea enzi za Mwinyi mpaka sasa, Wahindi wamehusika sana katika kuwaingiza viongozi wetu kwenye deals za ajabu ajabu na kuwaonyesha pesa.

Labda kinga kubwa kuliko zote ni kuhakikisha unakaa mbali na watu kama hao maana itaondoa hata perception iliyopo kwamba viongozi wetu wananunuliwa na Wahindi.

Watajifanya wanachangia maendeleo ya Mpanda, wanachangia CCM nk, lakini mbona hawakuwa tayari kuchangia wilaya ya Mpanda wakati hukuwa waziri mkuu? Kwanini hawachangii shule na kimya kimya na badala yake wanachia pale tu anapokuwepo rais, waziri mkuu au kiongozi mwingine wa juu?

Usipokuwa makini na hawa wafanyabiashara wa Kihindi, utajikuta unaishia kule kule kwa akina Lowassa ambaye pamoja na uchapa kazi wake, tamaa imemuangusha na sasa ataishia kuwa PM ambaye alikuwa fired kwasababu ya UFISADI.
 
Zomba, Katika kundi la mafisadi, nakuomba nitajie mtu hata mmoja wa Nyerere kama sio creation ya JK.....

mkuu, Mkandara majina umepewa, mbona unaleta ulalamishi tena???


kinachotakiwa ni viongozi wenye muono tofauti na itikadi za kinyerere. Za kumfanya kila mmoja awe masikini, masikini wa kutupwa. Zomba hii imetulia saana, tena weka msisitizo kuwa UMASIKINI SI KIGEZO CHA USAFI BALI UPUNGUFU!!!!!
Nakumbuka makaLa ya Johnson Mbako ktk raia mwema wiki hii aliposema KAMA ILIVYOKUWA NGUMU KUPATA WASIO DHAMBI 50 KTK MJI WA SODOMA, SOTE TUMEOZA KIMAADILI. KWA HAKIKA KWA NAMNA FULANI, WENGI WETU NI MAFISADI. TUNATOFAUTIANA TU KWA VIWANGO!!!!
 
Back
Top Bottom