Na Ronald Mutie.
Wakati wa mchakato wa usanifu, wataalam wa reli hii ya kisasa SGR kati ya Mombasa na Nairobi nchini Kenya walichukua hatua kadhaa zilizolengwa kushughulikia masuala ya mazingira, kama vile kulinda mimea na wanyama mbalimbali wa porini.
Tangu kufunguliwa kwake Mei mwaka 2017, reli hii ambayo ni kiungo muhimu cha usafiri kati ya bandari ya Mombasa na mji mkuu Nairobi, imepita kwenye maeneo yenye wanyamapori wengi wanaohama kati ya kaskazini na kusini.
Katika Wilaya ya Port Reitz mjini Mombasa, asilimia 64 ya kilomita za mraba 10 zimefunikwa na mikoko, ambayo ina jukumu muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi, kulinda bioanuwai na kutoa njia za uzalishaji.
Ili kuhakikisha ujenzi wa reli hiyo unafanikiwa bila kuharibu mazingira ya eneo la mikoko, wafanyakazi wa ujenzi kwa hekima walichagua njia ya kando.”Nimefanya kazi kwenye Reli ya Mombasa-Nairobi kwa miaka saba. Na kabla ya ujenzi, miti ya mikoko ilikuwepo, na baada ya ujenzi miti ya mikoko imebaki pale pale kwa sababu ililindwa,” anasema Kennedy, mfanyakazi wa ujenzi wa reli hiyo.
“Daraja liligeuzwa na kujengwa upande wa pili, walitaka kuokoa mikoko, wakati wa ujenzi wajenzi walikuwa wakitumia maji kutoka baharini kwenda kwenye eneo la mikoko ili kulinda miti hiyo na sio kuiharibu. Wajenzi walijitolea kulinda mikoko kwa sababu miti ni muhimu sana kwa jamii ya eneo hilo ambao huitumia pia kama dawa. Pia lazima walinde mikoko kwa sababu kuna samaki wanaoishi humo,” Samson, mjenzi mwingine wa reli hiyo.
Kwa vile mimea inaweza kufyonza kiasi kikubwa cha gesi chafu, wabunifu wa reli hiyo walichukua hatua za kulinda mimea ya maeneo yote. Kando na hayo, matumizi ya mafuta ya dizeli ya treni za mizigo ya reli ya Mombasa-Nairobi ni chini ya theluthi mbili ya yale ya usafiri wa barabarani, ambayo yanaweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 75.
Robo ya Reli ya hii inapita katika Mbuga ya taifa ya Tsavo, mbuga kubwa zaidi ya taifa ya Kenya na ambayo ni makazi ya takriban spishi zote za wanyama barani Afrika na yenye njia nyingi za wanyama wanaohama.
Kwa mujibu wa utafiti kuhusu ushoroba wa uhamiaji wa wanyamapori, vivuko 14 vya wanyama wakubwa na madaraja 79 yamejengwa kando ya njia hiyo. Madaraja yote yana urefu wa mita 6.5 au zaidi, ambao inaruhusu twiga kupita bila kulazimika kuinama.
Reli hii inaruhusu aina zote za wanyamapori kuvuka kwa uhuru. Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Wanyamapori ya Kenya Kitili Mbathi anasema alichunguza binafsi kando ya reli hiyo na hakupata athari mbaya kwa wanyamapori.
“Nimekuwa hapa mara kadhaa katika miaka kadhaa iliopita, kama miaka 20 hivi. SGR, sio tishio kwa wanyama, na treni haziwagongi.Sijawahi kuona. SGR inahudumia nchi za Afrika Mashariki, na wakati unapoitumia unaweza kuona mandhari ya kuvutia. Hata wanyama unaweza kuwaona ukiwa kwenye treni,” Apollo, mwongoza watalii wa ndani alisema.
Ili kulinda wanyama zaidi, njia za kuhama kwa wanyama wadogo zimejengwa kando ya reli na uzio wenye umbo la B kuwekwa kwenye sehemu tambarare.
Mbali na uzio na njia za kupitisha maji, kuna doria za kila siku za polisi wa wanyamapori kando ya reli.
Daraja la Mto Tsavo, mojawapo ya madaraja marefu zaidi ya reli nchini Kenya, lina nguzo refu na daraja la juu zaidi la mita 35.1, linalohakikisha hata twiga wanaweza kuvuka bila vizuizi. Kwa jumla kuna njia tisa kubwa za wanyama katika mbuga ya wanyama ya Tsavo pekee.
Na sio Tsavo tu sehemu ya Hifadhi ya taifa ya Nairobi kuna madaraja kama hayo na miundo mbinu mingine ya kulinda wanyama. Daraja la juu zaidi la kilomita 6.56 limejengwa kwenye hifadhi hiyo, na vizuizi vya sauti vimewekwa na kupunguza kwa ufanisi athari za kelele za treni kwa wanyama.
Mfano huu wa reli ya SGR ndio wito wa Umoja wa Mataifa wa kulinda asili kwa njia endelevu. Lakini pia kutokana na ongezeko la idadi ya watu duniani, maeneo ya makazi yameendelea kupungua huku shughuli za watu zikiingilia makazi ya wanyama pori.
Katika mkoa wa Yunnan nchini China kundi la tembo wa porini ambao walisafiri kuelekea kaskazini kwa miezi kadhaa mwaka jana wameishi kwa amani na wanakijiji jirani ndani ya makazi yao katika Hifadhi ya Kitaifa ya Mazingira ya Xishuangbanna, tangu walipowasili Desemba mwaka jana, na wote wako katika afya njema.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya idara ya usimamizi wa Misitu na malisho ya taifa.Kundi hilo lilizaa ndama Januari hii, na kisha kupoteza wenzao wawili waliojiunga na kundi jingine la kutafuta malisho katika Bonde la Tembo Pori katika hifadhi hiyo mwezi Februari.
Kwa mujibu wa Chen Fei, mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa Misitu na malisho katika kituo cha Utafiti cha Tembo wa Asia, tembo wengine waliingia ndani ya hifadhi ndogo ya Mengyang, na kukaa humo tangu wakati huo. “Kundi la tembo waliosafiri kuelekea kaskazini na kurudi wamedumisha shughuli ndani ya Hifadhi Ndogo ya Mengyang, ya Hifadhi ya taifa ya Mazingira ya Xishuangbanna, ambayo iko karibu na Vijiji vya Dadugang na Guanping.
Hii ni kwa mujibu wa picha za hivi karibuni za uchunguzi wa kamera. Ndama aliyezaliwa njiani anakua polepole na anaweza kusimama peke yake. Tembo wote wa kundi hilo sasa wako katika afya njema,” anasema Chen Fei.
Baada ya kuwasili, tembo hawa wa mwitu hawakuonyesha tabia yoyote ya kiajabu na waliishi kwa amani na jamii zinazowazunguka.
Kwa mujibu wa Chen, mara kwa mara tembo hawa walikwenda kwenye ukingo wa msitu kula mazao na kisha kurudi msituni, lakini hawajawahi kusababisha ajali yoyote mbaya, wala kuingia vijijini na kujeruhi watu.
Mwezi Machi 2020, tembo hao waliondoka kwenye hifadhi ya asili ya msitu huko Xishuangbanna, Mkoa wa Yunnan, na kusafiri takriban kilomita 500 kuelekea kaskazini hadi mji mkuu wa jimbo la Kunming na walifika Juni 2021.
Kisha walielekea kusini tena, na kurudi salama kwenye hifadhi hiyo. Safari yao kuu iliamsha shauku kubwa katika ulimwengu wa binadamu, na kuwapa watafiti nafasi ya utafiti wa migogoro ya binadamu na wanyamapori.
Kwa kuwa wataalam wengi wanaamini kuwa ni jambo lisiloepukika kwamba tembo wa porini watazurura nje ya hifadhi, wamechukua hatua ya kumudu mienendo ya wanyama hao kwa kupanda vyakula, kupanda miti zaidi na kufuatilia kwa zana za teknolojia.