Mitandao haijafanya watu kuwa wapumbavu ila imetudhirihishia watu wapumbavu kweli ni akina nani

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
3,064
9,331
Mpumbavu ndio atakae kuwa controlled na applications za simu.

Mpumbavu ndie atakae weka maisha yake rehani kwa ajili ya umaarufu na kushobokewa kwenye mitandao.

Mitandao imelalamikiwa sana, maybe at some liitle degreee ina athiri, maybe, lakini nafikiri mitandao imetoa nafasi ya wapumbavu kuonekana na kujulikana.
Imepelekea Wapumbavu hawa kufanya upumbavu hadi kupelekea kuathiri maisha yao wenyewe na watu wengine low minded wanaowafatilia huku wakidhani kufanya upumbavu kama wao ndio usasa na ujanja wa kileo.

Sasa we fikiria eti mtu ana pata depression eti kisa picha yake haijapata likes za kutosha, sasa mtu kama huyo utamfaninisha na mentallity yako ilio smart kweli?

Kwa usawa huu wa makalio na uchawa mitandaoni, eti na wewe pia una hangaika kupitia hizo trend kupelekea hadi kudhalilisha nafsi na utu wako utafikiri hauna options nyingine maishani.

It is a issue of mentallity. Wajanja hatuko katika rat race za mitandao. Sio kwamba hatuna mvuto au hela nyingi sana bali ni kwamba tu mitandao sio chapa yetu
 

Attachments

  • cT2iIMnGq46sQnSQ.mp4
    1.7 MB
Back
Top Bottom