MIKUMI: Mkulima aliyechomwa mkuki na Wafugaji apata nafuu baada ya matibabu

I see, serikali inalea sana wafugaji kana kwamba ni lazima sana watu kula nyama kuliko ugali au wali.

Naona kuna umuhimu wa kuwepo sheria inayotambulika rasmi ikiwa wafugaji au wakulima wataingiliana katika maeneo yao tena iwe kali na tozo za kuingia kwa mwingine iwe sio ya kirafiki.

Kila mfigaji angepewa/kuuziwa ardhi kulingana na idadi ya mifugo aliyonayo sio mtu ana ng'ombe 10,000 wakati hana hata eneo la ekari 5,walazimishwe kuwa na maeneo yao wenyewe ya kulishia mifugo maana hapo ndipo watapunguza mifugo yao na kufuga kisasa.

Kila mwaka tunajinasibu kuwa Tanzania tuna mifugo mingi Africa, lakini haina maana ikiwa ufugaji wenyewe ndo huu wa vita na kuumizana na ufugaji usio na maana.

Sipendi mtindo wa kifugaji wa kimasai na Kisukuma, wanaleta migogoro maeneo mengi waliokaribishwa. Then, ni waharibifu sana wa uoto, maana wanakata miti sana then malisho yakiisha wanawaachia jangwa hapo na wanaenda kuharibu kwingine. Mbona hayo mambo hayapo sehemu zenye udhibiti mzuri wa ardhi kama Kilimanjaro, Tukuyu, Mbozi n.k?

Serikali ifanye kazi yake vizuri, hili litakuwa janga baadae.
 
Why only Morogoro ? Mwigulu upo ? Au buko nje ya nchi unakula krismas ? Nakumbuka wakati mifugo ilikatwakatwa ulifika kwenye tukio fasta Leo ni binadamu hata jamii forums huonekani..
 
Vyombo vya Usalama Kazi Kwenu
Ugomvi wa wakulima na wafugaji sijui utakwisha lini jamani.
Duh pole sana brother uliejeruhiwa.
 
Inasikitisha sana tena Sana na inaumiza lakini Serikali inastahili lawama kwenye hili.

Serikali imekua ikibwabwaja tu juu ya Maswala yawahusuyo Wafugaji na Wakulima.

Serikali haitoi maelekezo sahihi juu ya maeneo sahihi ya Wafugaji na Wakulima. Maeneo ya Wafugaji yamekua madogo kieneo ukilinganisha na idadi ya Mifugo waliyonayo. Kutokana na mvua kutonyesha mpaka sasa Wafugaji hawa wanalazimika kuvamia maeneo ya Wakulima bila ya kujali hasara zitakazowatokea wao.

Nawashauri wakulima wote kuwa,pindi waonapo maeneo yao yamevamiwa na Wafugaji hasa wa Kimaasai, watoe taarifa polisi ndipo wasindikizwe kwa pamoja kwenda kuwaondoa mifugo yao. Hawa jamaa wana mbinu nyingi sana na watakuumiza hata kama una haki katika eneo hilo.

Sheria kali zitungwe juu ya Muingiliano wa Wakulima na Wafugaji. Mwisho,Wafugaji wapewe elimu juu ya athari za mifugo mingi katika karne hii.
 
Ehh Mwenye Enzi Mungu wajalie hawa watu amani yako. ..IMENIKUMBUSHA KAINI NA ABELI. .hapa ni mkono wa MOLA uingilie kati. ..pole sana majeruhi...
 
Migogoro ya wakulima na wafugaji itamalizika kwa jamii kujifunza ustaarabu zaidi badala ya sheria na matamko ya viongozi.
Hata hivyo, hali hii ni taswira ya fikra za jamii kwa ujumla. Siasa zetu mambo ni hayo hayo ila unafiki tu umetamalaki.
 
Pole sana kwa mkulima huyo kwa kweli inatia uchungua sana, hiv hawa wamasai mbona wanafanya matukio na kusababisha wananchi wazawa wa maeneo husiko waishi kama wapo ALLEPO? Nan yuko nyuma yao unaowafanya wawe viburi namna hiyo? Hiv wakulima wakiamua kufyeka mifugo yao yote itakuwaje? Maana tumechoka kila siku kusikia habar za wamasai kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima tena kwa makusudi
 
Hii migogoro itaisha lini
Kwa asili kuna mikoa au maeneo ya kilimo na mikoa/maeneo ya ufugaji. Kwa nini wafugaji waruhusiwe kutangatanga nchi nzima kama vile maeneo yote nchi nzima ni ya kwao? Serikali ndiyo inaendeleza migogoro hii kwa kuwapendelea wafugaji nakupuuza haki za wakulima katiks maeneo yao. Wafugaji wadhibitiwe. Uzururaji ukomeshwe.
 
Mhh, inasikitisha sana kuona watu wanajichukulia sheria mkononi kama vile hakuna mamlaka zenye kudhibiti wakosaji
 
Manisha ya dunia ya Leo Ni ya mashaka mno siku zote wafugaji ndio chanzo cha mapigano haya
hawa wamasai si warudi huko kwao arusha wakachungie huko huwa najiuliza "ingekuaje kama makabila mengine wangeenda mikoa yao kulima na kufanya makazi"
 
Hao wamasai wanasumbua hizo Jamii, inabidi tuwahamishie kule Mara Tarime wakapambane na wakurya nazani watatulia
 
Mkulima mmoja wa Kitongoji cha Upangwani Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata ya Masanze JImbo la Mikumi Morogoro jana amejeruhiwa vibaya kwa kuchomwa mkuki mdomoni na kutokezea nyuma ya shingo yake, ambapo alipelekwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadae amekimbizwa hospitali ya mkoa MOROGORO ili kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na kwa matibabu zaidi.

Kijana huyo AUGUSTINO MTITU alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani yake kufukuza Ng'ombe wasiharibu mazao shambani kwake, Kipande cha mti kinachoonekana hapo mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali, Inasemekana MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa.

Ofisi Ya Mbunge Mikumi, Profesa Jay inatoa wito kwa Serikali kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.

Imetolewa na:-
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Mikumi.
View attachment 450434
View attachment 450435
View attachment 450436
View attachment 450437
View attachment 450438

Matatizo mengi yanayotukabili watanzania yanachangiwa na siasa.
Watendaji wengi wako kisiasa zaidi kuliko kitaalamu.
Kila siku tunawaona wakijinadi kwenye runinga ili waonekane na siyo kutatua matatizo.
Njia pekee ya kupona na kuiponya nchi ni pale siasa zitakapotolewa kwenye utendaji.
Lakini tatizo lipo kwani kuondoa siasa kwenye utendaji ni vigumu kwani hao watendaji ni wateule wakisiasa.
Sasa viongozi wachukue dhamira ya dhati ya kuteua watumishi wa umma wenye weredi badala ya kutoa complimentary kwa makada fulani.
 
Back
Top Bottom