Mikoa 5 Tajiri Tanzania na Mikoa 5 maskini zaidi Tanzania 2020

game over

JF-Expert Member
Jan 1, 2016
10,770
25,025
Mikoa Tajiri GDP per Capita in Thousand Tsh.
1. Dar es Salaam - 4,678,751
2. Iringa - 4,028,544
3. Mbeya - 3,788,604
4. Ruvuma - 3,396, 587
5. Kilimanjaro - 3,393,587

Mikoa masikini Tanzania
1. Kagera - 1,168,661
2.Kigoma - 1,479,389
3.Singida - 1,622,891
4. Dodoma - 1,759,347
5. Tabora - 1,777,039

Chanzo : NBS
IMG_8943.jpg



My Take: Mikoa ya nyanda za juu kusini ina potentials zaidi ya kukua sababu ya mapinduzi makubwa yanayoendelea kufanyika kwenye Kilimo, muda wa kwenda kuwekeza Nyanda za Juu kusini.
 
Iringa, Ruvuma na Mbeya mbona bado wanajenga nyumba za tofali za kuchoma katikati ya miji yao na wana hela? 🤔

Yani Mbeya town kabisa kuna nyumba za tofali za kuchoma sio za mwaka 2000 wala 2010 zinajengwa hadi kesho
 
Iringa, Ruvuma na Mbeya mbona bado wanajenga nyumba za tofali za kuchoma katikati ya miji yao na wana hela?

Yani Mbeya town kabisa kuna nyumba za tofali za kuchoma sio za mwaka 2000 wala 2010 zinajengwa hadi kesho

Kwani kuna tatizo kujenga nyumba ya tofali za kuchoma? unadhani kujenga kwa tofali za kuchoma ni kukosa hela?
 
Tangu nijue kuwa GDP ya mkoa sijui Taifa haileti japo chupa ya mirinda ya sh. ⁵⁰⁰ huwa sihangaiki nayo.
Unakuta mtoka mkoa namba 1 kwa GDP anaishi maisha magumu kuliko yule atokaye mkoa wa mwisho kwa GDP.

Hivyo ndivyo wachumi hupima maendeleo,
Hata hivyo,
Kwa ujumla wake huwezi fananisha maisha ya watu wa Mkoa wa kilimanjaro na mkoa wa Kigoma
 
Nadhani walichozingatia hapo ni hali kibiashara na mzunguko wa fedha kwenye mikoa tajwa.......kuwa kwenye mzunguko mkubwa wa fedha ni jambo la kwanza na kuzitumia hizo pesa kuboresha maisha yako ni jambo la pili......

Ni kama ofisini ambapo Kuna mtu analipwa 400,000/= lakini anazitumia vyema kujiboreshea maisha yake kuliko hata yule anayelipwa milioni lakini ukitazama kipato utamuona huyo mwenye milioni yupo juu......

Mikoa iliyo kwenye top five ina shughuli nyingi sana za kiuchumi, kipimo , biashara na viwanda kama ulishawahi kufika maeneo hayo utakuwa shahidi katika hili.........

Pamoja kujishughulisha na yote lakini wameshindwa kuboresha standard za maisha yao.......

Kiujumla Ukiacha Dar es salaam hakuna mkoa unaoifikia Kilimanjaro kwa standard ya maisha.......maana yake Wana Kilimanjaro wametumia vyema rasilimali zao kujiboreshea maisha yao......
 
Tangu nijue kuwa GDP ya mkoa sijui Taifa haileti japo chupa ya mirinda ya sh. ⁵⁰⁰ huwa sihangaiki nayo.
Unakuta mtoka mkoa namba 1 kwa GDP anaishi maisha magumu kuliko yule atokaye mkoa wa mwisho kwa GDP.
Miko iyo ina matajiri ambao ukigawanya kwa pesa zao na idadi wanabeba wengin

Ishi ni kwamb maskini wapo tu kama kawa
 
Back
Top Bottom