fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 3,569
- 4,632
SEHEMU YA KWANZA: URAFIKI WA DHATI.
Ni kwenye ile wilaya niliyoiongelea kwenye ile stori yangu ya jinsi nilivyokutana na singo maza wa kiarabu.
Ni miaka mingi imepita, wakati huo nilikuwa kidato cha kwanza.
Marehemu mama yangu alikuwa na rafiki yake, mama mmoja ambae alikuwa mpambanaji sana kwenye maisha.
Huyo mama alikuwa akifanya biashara ya kupika na kuuza chakula, na alikuwa maarufu sana kwa kupika kuku na alikuwa akitembeza kwenye mabaa. Pia alikuwa na banda ambalo kila siku mida ya mchana na jioni alikuwa akiuza vyakula.
Alikuwa na mumewe ambae alikuwa akifanya kazi kwa muhindi mmoja, usiku akilinda na mchana akifanya kazi mbalimbali hapo kwa huyo muhindi ambae alikuwa na biashara ya duka kubwa na malori ya kukodisha, malori ya tani 7 na tani 10.
Alibahatika kupata watoto 2 mmoja wa kike ambae nimwite Bankorwa japo sio jina lake, na wa kiume nimwite Sagala,nalo sio jina lake.
Huyu mama alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa mama yangu. Mama akipata wageni humwita huyo mama Bankorwa kuja nyumbani kumsaidia kupika. Kutokana na urafiki huo nami pia nikawa ni rafiki wa huyo mama na wanae wakawa ni wadogo zangu, Sagala alikuwa akisoma la saba na Bankorwa alikuwa la tano.
Nikitoka shule nilikuwa naenda kwa huyo mama namkuta akifanya kazi za maandalizi ya upishi nami nikawa nasaidia kazi, kama mtoto wa hapo nyumbani. Yule mama alinizoea sana na mara kadhaa alikuwa akinituma kwa mama, na mama pia mara kwa mara alikuwa akinituma kwa huyo mama. Mara kadhaa mama alikuwa ananipa pesa kumpelekea huyo mama.
Nilikuwa nikifurahia sana maisha hayo maana yule mama alikuwa akinipa finyango ya nyama ya kuku na ilikuwa tamu mno hata sijui alikuwa anapikaje, na alikuwa anapata oda ya kuku mara kwa mara.
Katika mazingira ya ajabu, huyu mama alianza kupata mikasa ya ajabu, ambayo ndio msingi wa stori hii. Hii ni stori ya kweli kabisa. Naiandika nipendavyo mimi, ukiisoma sawa na usipoisoma pia sawa, ukitaka kutoa mapovu we toa, mie sitahangaika na mtoa mapovu.
Itaendelea baadae kidogo.