Migodi hatarini kufungwa kufuatia agizo la Rais Magufuli

Kwa mara ya pili namuunga mkono Rais aya mambo ya kutetea wananchi kama Rais ndo tuliyomtuma sio kukimbizana na wakina Lema na Lissu kumbe wanotafuna nchi anaenda nao kupakwa majivu
 
Yaanini hatari Manjagata.Hili suala ni kuhandle kwa uangalifu mkubwa.Australia wako juu sana duniani kama siyo kuongoza lakini hadi sasa wanaexport concentrates.Rais anashauriwa vibaya.Kuna nchi zilushajaribu kufanya hiki tunachota kukifanya zikaanguka vibaya sana
Tuliache liongoze linavyotaka, lakini mwisho wa siku atakuwa mdogo kuliko hata piriton! Anafikri wawekezaji wanajipelekea tu huo mchanga bila makubaliano? Wacha tuone. Tatizo naye anafanyiakazi hata habari za mitaani kwenye vijiwe vya wanywa kahawa na wabrash viatu! Akisikia wananchi wanaongelea habari za mchanga kusafirishwa naye anakuja kuropoka huku kwamba tunaibiwa sana! Unaibiwa nini? Mbona hujapiga marufuku ndege zinazotua ngorongoro na kuondokea huko huko bila ukaguzi?
 
kwa kuweka sawa tu, hawa watu waliingia mkataba wa kuchimba dhahabu pekee, ambapo serikali inakata kodi, lakini hizi wanaiita masalia by products(concentrates) hizi hazipo kwenye mikataba inawezekana kabisa zilikuwa hazikatwi kodi,

concentrates/by product masalia, huu ni muunganiko wa madini yenye ukaribu sana kwenye periodict table, kama SILVER,GOLD,COPPER NK.
haya yote yanapatikana kwenye sulphate ores, ambayo kwa teknolojia ya kawaida wanayotumia hawawezi kutenganisha..

lakini hili ukiangalia wamefanya hivi kwa makusudi tu kama tukiwazuia watatafuta njia mubadala tekinolojia ya uchenjuaji inakua kila siku..

kama wakiona vipi waende tu lakini najua ndo mwanzo wa kuja na njia mpya au kurudi mezani tena.
Rudia tena kujifunza maana naona umekariri periodical table ukaona na wewe utoe comments. Tanzania hakuna precious au base metals zinazo tokana na sulphates. Sulphate zinazopatikana Tanzania ni kama gypsum.
Kuhusu kuibiwa ni nadharia iliyo jengeka Tanzania kila aliye nacho hajapata kwa nguvu na maarifa yake bali kwa wizi. Wataalam wa serikali kupitia TMAA walifanya utafiti katika ya mwaka 2014 na 2015 uwezekano wa kuanzisha smelter and refinery hapa Tanzania ili by products za Bulynkulu na Buzwagi ziwe processed hapa...Ripoti yao ipo kwenye mtandao wa MEM jipatie nakala ili ushibishe ubongo. Jibu by product zetu combined haziwezi kuhalalisha ujengwaji wa s na r hapa. Kama kuna faida basi serikali au watanzania wengine wachangamkie fursa hiyo wajenge na Acacia watapeleka hapo. Nchi nyingi Duniani kama Canada,Australia,Indonesia nk wanapeleka Japan sisi tu ndo tunaibiwa....kazi kweli kweli

Mahitaji ya smelters ni mitaji mikubwa kwani gharama za uendeshaji ni kubwa sana. Mathalani,ili kufanya uchenjuaji wa Ni na Co hapa nchi mgodi wa Kabanga utahitaji umeme wa kiasi cha 80MW kwa siku. Wakitengeneza concentrate peke yake watahitaji 40 MW huo umeme uko wapi? Na tambua mpaka sasa migodi mingi umeme wa Tanesco ni kwa ajili ya dharura tu hivyo umeme ni wa diesel generator....sasa hiyo ni migodi ya dhahabu peke yake je smelter??
 
Hakuna uwezekano wa Acacia kwa sasa kujenga mtambo wa kuchenjua shaba na fedha kwa kuzingatia kiasi cha shamba na fedha kilichopo. Hi ni sawa na mtu kukulazimisha ujenge kiwanda cha kukamulia mafuta ya alizeti kwa sababu unavuna magunia 20 ya alizeti kila mwaka.

Siamini kama Acacia wana uwezo wa kuendesha mgodi wa Bulyanhulu bila ya kusafirisha nje Au-Cu-Ag concentrate. Ni hii concentrate ndiyo profit margin yao. Kama serikali itasimamia maagizo yake, mgodi wa Bulyanhulu, ulio wa pili kwa ukubwa baada ya ule wa Geita, upo hatarini kufungwa. Ni muhimu sana wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu na suppliers wote, kuanza kujiandaa kwa chochote kinachoweza kutokea.

Kwa hatua hii, kuna ujumbe mzito unaopelekwa kwa wawekezaji wote Duniani.
 
Halafu ooh hatufukui makaburi,hapa ndo tumepigwa Sana na waliopita MAGOGONI. Ndio tungeanzia kuyafukua hapa makaburi tumeliwa mno,watu walikua wanapewa vinyago vya dhahabu Kisha wanabariki huu UNYONYAJI
 
Naangalia naona akili za watanzania zilivodumaaa jana share za acacia ktk stock markt zimeshuka kwa 18℅ sasa angalia impact kwenye export mapato, kodi za ndani, employment zote zitakula kwa watanzania dah kuna mtihani mkubwa unakuja
Unaongea vitu vikubwa sana kwa akili za gavana wa bank kuu achilia mbali waziri kuzielewa, magufail hakuna anachokijua zaidi ya "hewa, Kira mahari ni hewa tu"
 
Naangalia naona akili za watanzania zilivodumaaa jana share za acacia ktk stock markt zimeshuka kwa 18℅ sasa angalia impact kwenye export mapato, kodi za ndani, employment zote zitakula kwa watanzania dah kuna mtihani mkubwa unakuja
Na Raia wa kigeni wananyang'anywa pasipoti utafikiri magaidi! Kweli wawekezaji watakuja hapa tena?
 
Lazima ajira ya kusafisha mchanga na kupata dhahabu ibaki kwetu.

Hayo makampuni sasa yataacha "kupata hasara" kwa kuacha kusafirisha mchanga na badala yake yasafirishe dhahabu.

Hii ni awamu ya serikali inayotumia akili. Enzi za mikataba ya Kafumu ya kuruhusu madudu kama kuuza mchanga wa dhahabu badala ya dhahabu yenyewe zimekwisha.

Viva Magufuli. Let us do the right thing at any cost.
asante mkuu kw awazo maridadi
 
Wataalamu watuambie huo mchanga ukisafishwa hapa bongo kuna tatizo gani? Kama hatuna mitambo itatulazimu kiasi gani kuwekeza kununua mitambo? Wataalamu tusaidieni hapo tutani tujadili kitaalamu zaidi siasa ikiwa kando.
Watu wasichokijua ni kwamba Bulyanhulu hatuna copper ore kama ilivyo kwa Zambia au DRC. Pale Bulyanhulu kuna gold ore, copper na silver ni trace amount ambayo huwezi kufanya extraction. Acacia wanachofanya ni concentration. Na ule siyo mchanga wenye dhahabu bali ni mawe yaliyosagwa, dhahabu ikaondolewa. Kukabakia kiasi kidogo sana cha dhahabu, copper na silver kwenye mawe yaliyosagwa. Kiasi kile ukisafirisha kama kilivyo huwezi kupata faida. Wanafanya concentration kwa kuyapatia yale madini artificial behaviour. Baada ya concentration, mchanga uliokuwa, kwa mfano, na 0.01% copper, utaweza kufikia hata 10%. Lakini mchanga huo wa container 1 wenye 10%Cu umetokana na mchanga zaidi hata ya containers 100 za ore ya kawaida iliyokuwa na 0.01% copper.

Swali linakuja, unaweza kutengeneza plant ya kufanya uchenjuaji wa mchanga unaohesabiwa kwa containers? The answer id no. You need hundreds of tons to have a processing plant which we do not have. Swali rahisi, hivi unaweza kununua mashine ya kusaga mahindi kwa sababu kila mwaka unapata magunia matano? Ipi ni economically viable, kubeba magunia matano na kupeleka kwa mwenye mashine au kununua mashine yako? Japan imewekeza katika teknolojia hiyo. Inapokea thousands of concentrate containers from all over the world including technologically advanced countries like Australia.

Uamuzi wa kuzuia concentrates kwenda nje hautasababisha plant kujengwa nchini, sitarajii. Labda kitakachotokea ni kutokuchenjua madini ya shaba na fedha.
 
Ndio akili zenu zilipofikia chuki hasadi na roho mbaya si mmepewa tanzanite one nyie wazawa sasa ile pale inawafia. Haya mambo sio kukurupuka kama ngoma ya mdundiko yataka kuangalia mapana yake haya
Haya makampuni kila mwaka yanatangaza hasara huku yakiendelea kuacha mashimo na makorongo ya kutosha......bora wafunge ili wasiendelee kuingia hasara.!
 
Hakuna uwezekano wa Acacia kwa sasa kujenga mtambo wa kuchenjua shaba na fedha kwa kuzingatia kiasi cha shamba na fedha kilichopo. Hi ni sawa na mtu kukulazimisha ujenge kiwanda cha kukamulia mafuta ya alizeti kwa sababu unavuna magunia 20 ya alizeti kila mwaka.

Siamini kama Acacia wana uwezo wa kuendesha mgodi wa Bulyanhulu bila ya kusafirisha nje Au-Cu-Ag concentrate. Ni hii concentrate ndiyo profit margin yao. Kama serikali itasimamia maagizo yake, mgodi wa Bulyanhulu, ulio wa pili kwa ukubwa baada ya ule wa Geita, upo hatarini kufungwa. Ni muhimu sana wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu na suppliers wote, kuanza kujiandaa kwa chochote kinachoweza kutokea.

Kwa hatua hii, kuna ujumbe mzito unaopelekwa kwa wawekezaji wote Duniani.
Ili kuanzisha smelter unahitaji kiasi cha chini kabisa 150,000 tons za concetrate . Buzwagi na Bulyankulu kwa pamoja wana safirisha 50,000 tons kwa mwaka,tena zikiwa na wastani wa 15% copper.
Kwa misimamo hii tusubiri watanzania wenzetu kupunguzwa kazi
 
Ndio akili zenu zilipofikia chuki hasadi na roho mbaya si mmepewa tanzanite one nyie wazawa sasa ile pale inawafia. Haya mambo sio kukurupuka kama ngoma ya mdundiko yataka kuangalia mapana yake haya

Madini ni "non-renewable source" yaani ikichimbwa ndo inaishia hivyo. Isipochimbwa haiozi.

Swali ni je, tangu wawekezaji wameanza kuchimba nchi imefaidika kiasi gani? Ukijibu hilo utahitimisha dai lako la "chuki hasadi na roho mbaya"!
 
Hivi wewe mining Industry unaifahamu au unaongea kishabiki.Mimi ndiyo professional yangu na huko West Africa siyo kwamba nimeongea kiushabiki.Nimefanya kazi kwenye mining Industries za Ghana,Senegal,Mali,Burkina Faso napafahamu vizuri.Ninaifahamu vizuri mining industry vizuri kuanzia kwenye booming ya 1990s.Rais wa Senegal Mack Sall ni Geologist by Professional nenda kaangalie anachokifanya nchini mwake kwenye mining.Ghana,Mali(achana na south afrika) wanatuzidi sana kwenye uzalishaji wa dhahabu Afrika.Tatizo wabongo ujuaji mwingi.Mimi nasema hatuibiwi tunakosa sera nzuri tu.Tusijidanganye Acacia na Anglo wakifunga migodi yao Uchumi utayumba hatari
Nimekusoma mkuu lakin najiuliza sana mkuu kuhusa kutoa mikataba si kama malipo yatakuwa makubwa ya kuvunja mkataba?
 
Mkuu, Tanzania tuna mazombie mengi mno! Ndo maana mengine yameng'ang'ania kutuongoza huku yana vyeti vya wizi! Eti kuna taahira jingine humu linasema tuna furnace za kuyeyusha huo mchanga, nabaki mdomo wazi ni lini hiyo mitambo ilijengwa hapa nchini? Kwa ufupi Rais wangu anakurupuka sana bila kupata ushauri kutoka kwa wadau wengine, anajifanya yeye ndo final say kumbe uelewa wake ni average sana na hana tofauti na mwananchi wa kawaida tu!! Wachumi wamshauri, wataalam wa madini wamshauri. Nashangaa Muhongo naye mtaalam wa madini madini lakini anabaki kuwa yes man tu!!
Mkuu sio tutafteni chakula tu kwa sasa mengine tumwachieni yeye anajua kila kitu sijui hana mshauri! Nmechoka kumsikia eti
 
Nimekuwa mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu kwa muda wa miaka 9 na ninachofikiri watu wanatoa mawazo yao hawaelewi nini kinaendelea pale.si vibaya tukieleweshana Bulyanhulu wanazalisha mchanga ambao unaitwa copper concentrate concentrate inajazwa kwenye contena za ft 20 na inasambazwa vizuri kwa usawa na kupimwa uzito na baada ya hapo sample zinachukuliwa.kwa kifupi kuna Dhahabu shaba na fedha. Hapa tuwe makini sample zinachukuliwa na kampuni na zinafanyiwa analysis na sgs pale pale mgodini na watu wa TMAA nao wanachukua sample na wanaenda kudanya analysis wanapokujua wao serikalini na hii ni kwa kila contena baada ya hapo macontena yanayosafirishwa kila kitu kinakuwa wazi kuna shaba kiasi gani dhahabu na fedha na ndiyo mafisa wa TRA na TMAAwanakuja na kuweka seal macontena yotekabla ya kusafirishwa hivyo hakuna wizi unafanyika watu amuelewi na hata hao maafisa wa TRA na TMAA wanajua ukweli. Kwa taarifa hata hizo smelting company kabla ya kuprocess nao wanachukua sample na kuzifanyia analysis kama zinaendana na zile ambazo zimetumwa na kampuni na kama deviation ni tatizo.
Kwa hiyo ndugu zangu watanzania tusishabikie vitu ambavyo hatuvielewi hata matofari ya dhahabu yanayozalishwa nayo yanapelwkwa kwenye smelting kwa ajili ya kupata pure gold sababu yote yanayoAlishwa kuna impurities zamadini mengine.
Watu wa TMAA wawaeleze ukweli wanancho kuliko huu upotoshaji unaofanyika
 
Back
Top Bottom