Michepuko matatizo kwa wanandoa

Ndoa ni bonge la mtihani,Ukiona mtu anaingia kwenye ndoa halafu baadae yanamshinda maana yake mtihani huo kwake umekuwa mgumu,kwa hiyo km wewe mtoa mada mtihani huo umekushinda basi juu kuwa sio wote unaowashinda.
Kwa hyo ndoa ni mtihani..Na wengine hatupendi mitihani sasa sijui itakuwaje. Nilitegemea ndoa iwe ni furaha na sio mtihani au unaonaje mkuu
 
Watu wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawajawa tayari yaani mtu bado anatamani mambo ya kuhuni huni ila kaingia kwenye ndoa...Msichana bado yupo na chalii wake wa chuo na mwanaume bado yuko na demu ambaye wanafanya wote kazi..Halafu wanatengeza ndoa hiyo itaitwa ndoa ama maigizo...
Wengine unakuta waliacha hizo mambo zote lakini walivyoingia tu figisufigisu zikaanza.
 
Siku hizi ndoa nyingi zimekua na matatizo lukuki mpaka hakuna heshima ya ndoa tena. Wanandoa wanachepuka kila siku mpaka mtu unajiuliza kwa nini watu wanaamua kuoana. Wanandoa wanaachana kila siku sababu zikiwa likuki ila nyingi michepuko ndo inasababisha. Na hao bao hawajaacha unakuta hakuna aman ndani ya nyumba wanaishi ilimradi siku ziende tu. Ukiangalia wanandoa wengi wanapatwa na magonjwa ya zinaa(Ukimwi,gono n.k). Mda mwingine ukitafakari unaona ni bora uishi kivyakovyako tu siku ukijisikia unatafuta mtu mnabanjuka maisha yanaenda. Wanandoa hembu tupeni sababu zinazosababisha hizo purukushani na mnadhani nini kifanyike kuepusha haya yote. Na ambao hamjaoa/Olewa mnawashauri kitu gani kabla kuingia chamani ili yasiwapate yanayawapata wanandoa walio wengi.
The only things I can say if you/we are not ready for marriage or don't know the meaning of the marriage then stay single until you get answers of these two things.. Thanks..
 
Kati ya taasisi ambazo bwana shetani anapigana nazo kuhakikisha hazipo salama ni NDOA, so kuelewa hii kitu napo unaweza kuwa na jibu mujarabu, hapo mambo mengine ni extra issues za kuonesha NDOA ina fgsufgsu but lijamaa at works!!
 
Hali ya ndoa nyingi siyo kama inavyoongekea, nafikiri kuna chumvi nyingi juu ya tuhuma hizi. Marafiki zangu, ndugu zangu, wafanyakazi wenzangu wengi tu wako happy kwenye ndoa zao. Ni wachache tu wenye figisu figisu.

Halafu pia Ndo nyingi hazivunjiki kama inavyosemwa. Nimejaribu kuangalia katika ma classmate, workmates na ndugu ninaowafahamu ambao wamefunga ndoa kuanzia 2005, ni wa 4 tu kati ya 46 ndo wametengana, mmoja sababu ya michepuko ya mwanamke, wawili tabia za wanaume lakini siyo michepuko, na mmoja tuhuma za ushirikina kwa mwanamke.

Nafikiri tunapenda ku generalize sana mambo bila kuwa na data. Naamini ndoa nyingi ziko imara na zina upendo ukiacha mikwaruzano ya hapa na pale ambayo ni kawaida sana.
Mkuu unanipanipa moyo ila kati ya hizo ndoa 46 najua kuna ambazo haziko sawa ila ndo hivyo kwa sababu walishasaini cheti inabidi wavumiliane. Na ukiangalia watoto na mambo mengine ndo yanawafanya wabaki kwenye ndoa.
 
Huyo parment nae ana mchepuko wenye michepuko hapo mnyororo unaendlea.

Halafu inamana nae hatatamani ndoa?
Bora uwe na mtu mwenye mchepuko kuliko kuwa na mke/mume mwenye mchepuko. Akizingua unaachana nae unatafuta mwingine,ukiwa kwenye ndo sasa sijui utamuachaje.
 
Wala haina fomula ndugu, muombe tu Mungu Akupe mwenza wa kukufaa, naweza nkakuambia ndoani ni kama vitani kumbe ukapata mke mwema ndoa yako ikawa Paradiso
Kwa hyo hapo ni kuotea..Ukiotewa imekula kwako. Kazi mbona ipo kumpata mwenza wa paradiso
 
The only things I can say if you/we are not ready for marriage or don't know the meaning of the marriage then stay single until you get answers of these two things.. Thanks..
Sasa utakuta kuna hao wanaolazimisha,mtu hayupo tayari utasikia bby nna mimba yako tuonane tu tutunze kiumbe chetu.
 
Asilimia kubwa ya wanawake huficha madhaifu yao pale mnapokuwa hamjaoana na yote hiyo ni kwa kuwa wanataka ndoa, baada ya ndoa hukunjua makucha yake na mume kuhisi sicho alichotaraji.

Wanaume nao asilimia kubwa huvutwa na uzuri/urembo wa binti na kukimbilia kumuoa, akishamuweka ndani anaona hana mvuto tena haswa pale nje anapoona watoto wakali zaidi tena wanaojirahisi.

Hayo ni machache kati ya mengi na pia wapo wengine asili yao ni kuchepuka tu hata umbebe na mbeleko gani, nadhani wengi hawaingii kwenye ndoa kwa kumuogopa mungu na kuacha kuzini........wengi huingia ili tu kuhakikisha anamdhibiti fulani na kumfaidi sababu ya uzuri wake, pesa zake nk
U have a point mdau.
 
Ndoaaaaa. Haina formula. Unataka ingia hutaki acha. Husikatishe watu tamaa
Husikatishe=Usikatishe

Nafikiri hajakatisha tamaa amezungumzia hali halisi ya ndoa ya sasa kisha akaomba ushauri kutoka kwa wanandoa.
 
Unaweza tafuta mtu wa kubanjuana nae permanent ila kuoa huoi. Siku hizi wadada wengi ni movie type unaweza ukaingia ukajuta.
Wanaume wengi sana wanafanya hivyo sikuhizi,ni wewe tu ndio umechelewa.

Ndoa za sasa zinakatisha tamaa.
 
Pokea like nyiingii. Na pia watu hufikia kusema kuwa wasichana warembo wanataka kuolewa na watu wenye pesa tu hii nayo ni generalization ya hali ya juu. Kwa kuwa huko maofisini na mitaan warembo kibao wanaolewa na wanaume wa kawaida wanaanza maisha ya kawaida kabisa ya kupanga chumba kimoja mpk wanakuwa na maendeleo kiuchumi..sasa ukiyapima kwa upande wa mastaa ndo unabaki kugeneralize kuwa wasichana wanataka kuolewa na wenye fedha
Wawili kati ya1000.
 
Kuchepuka huenda si kubaya. Ila tatizo ni huruma watu walokuwa nayo mf. Mtu anaolewa na mtu ambae hampendi kisa eti "tumetoka mbali" mbali my foot!??? Wewe unajua humpendi afu unadanganya roho yako eti " atabadilika ahaaaaaaaaa alishinwa kumbadilisha mama yake wewe utaweza? Sasa ndoa ndo iyooooo tiyari ndani unakutana na pande la mtu, sio choyo macare kibaooo! Loh lazima nionje karanga. Za kununua baadae
 
Back
Top Bottom