Michango ya wana JF kuhusu Q-Net imeniokoa nisitapeliwe Mwanza

Kuna jama yangu mmoja mpuuzi sana! Baada ya kunizoea hapo Mwanza akawa anakuja ofisini kwangu Nyegezi kunishawishi!

Siku nilienda hapo ofisini kwao maeneo ya Isamilo baada ya kufika tu wakaanza GOODMORNING! Nikachukuliwa na dada mmoja kwenye chumba maalum akaanza kunipa maelekezo,hakika ni maneno ya kutia moyo sana kama ukitanguliza taa lazima uumie!

Baada ya mazungumzo na yule dada nikatoka chumbani nikaingia ukumbini ndo nilikutana na maajabu! Kuna Bwana mmoja alitookea Shinyanga akijitambulisha kuwa alikuwa Mwalimu na kwa sasa kaamua kuachana na kazi ya Ualimu na kujiunga Q-NET na anatengeneza pesa nzuri ila ukimwangalia kajaa stress na sura yake haina nuru!

Nilipokuwa naondoka eneo hilo nikiwa na mashaka makubwa juu ya Q-NET niliikuta gari aina na BMW akiwa anaondoka nayo dada mmoja lakini nikavuta kumbukumbu zangu kuwa gari hii nilimuona nayo yule jama kila mara akiwa anakuja ofisini kwangu Nyegezi!

Nikajifunza jambo moja kuwa hawa jamaa wana gari yao ambayo huitumia kwa kila mmoja wao akipata mteja ili kumuonesha mtu amefanikiwa hivyo kuwafanya kujiunga kichwa kichwa kwa kushawishiwa na gari ya mwana Q-NET!

Kila mmoja awe makini hakuna hela nyepesi hapa duniani!
Hawa ni wengine wapo maeneo ya mkolani
Ila kuna dada na mume wake wao wana nyumba kubwa na gari range
Nao wanasema vitu vyao vyote wamepata kupitia Q-net na watu wameanza kuwaita freemason kwa wanavyodai na nilifika hadi hapo wanapo kaa kwasababu nilipelekwa na vijana wengi wanaenda ila wakaaminishwe juu ya mafanikio watakayo yapata
Ila hesabu zangu ziligoma kuweza kupata mtu wa kumshawishi afanye biashara ya 6M and ni kama Virtual na sio physical zaid
 
😂😂😂😂😂 kikundi cha wehu haha “Good morning”! Yani mtu bado unatoa million 3! Walio wajinga wanaendelea kuliwa hakuna pesa bila kufanya kazi ni bora vikoba kuliko hao wehu wa good morning
Tuzidi kutoa maarifa tu mkuu ili na wengine wapate kuelewa mkuu
Bila kufanya hivyo watu wengi watakuwa gizani
 
😂 nilishtuka mapema kwasababu kuna kitu kama hii ilitwa idea debeter back then 2021 niko chuo walikuwa wana opearate kama hao q-net wanavyofanya
Walinipiga 10k chuo ila kuna wengine walipigwa mpak 1M kwahiyo nikashtukia deal ila nilijua hichi kitu nitapata ufafanuzi zaid jf
Yani una bahati sana mkuu, hizi network marketing sio za kujihusisha nazo kabisa, zinafilisi na kulemaza ubongo.
 
Za siku nyingi wana JamiiForums, natumaini mu wazima.

Naomba nitoe shukrani zangu kwa JF kwa maada mbalimbali zimekuwa zinasaidia sana, mimi si mtoa maada sana ila msomaji mzuri.

Niende kwenye point. Siku ya leo, nilipigiwa simu na ndugu yangu kwenye ukoo huku Mwanza kuwa ana mchongo kwa kibiashara wa hela na hvyo hawezi niacha mimi nyuma.

Hivyo kwakuwa ninaheshimiana naye ilibidi niitikie wito, na nilivyofka eneo la tukio na kama nyumba ya mtu ambayo imekodiwa kwa ajili ya mafunzo hayo, ambayo na mimi nnaenda kuyapokea.

Nlkutana na vijana wengi wengine wakidai wao ni madoctor Bugando na wengne wako chuo Bugando na baadhi ya watu mbalimbali kadri ya walivyojitambulisha.

Shida ilianza kweny mafunzo yenyewe ya Q-net kwasababu siasa zilikuwa nyingi kuhusu mwaka ilipo anzishwa, mara udhamini na Man City na kuwatengezea special order ya saa wachezaj wa Man City pia udhamini wa CACFL yote hayo ni kutaka kuniaminisha kuwa kinacho endelea ni kizuri.

Walianza sema natakiwa niwe na mtaji wa MILION 6 ili na mimi niungwe kwenye network nianze kupiga pesa hapo ndipo akili ikaanza kucheza na kukumbuka baadhi ya thread za JF kuhusu kalinda.

Nimewakubalia na nimejaza fomu ila sijalipia hela yoyote kwanza ili nije nijihakikishie kwenye page ya JF.

Nashukuru kwa niliyo yapata hapa ingawa yalipostiwa nyuma kidogo ila yamenifungua sana.

Ila huruma ni kwa ndugu yangu kwasababu yeye ameshapigwa na ni mtoto wa kike amemaliza chuo mwaka jana ila ame-manage kupata MILION 3 ili kujiunga na hiyo kitu.

Nilichopanga nitaongea naye tu ila sijui kama atanielewa kwasababu ameaminishwa sana mpaka kufikia hatua ya kupelekwa kwa baadhi ya watu wanaosimamia hyo Q-net huku MWANZA-NYAHINGI kwenye nyumba zao na wanaishi na familia zao kabisa na kumuonesha yeye na baadhi ya vijana wengne yale wao hao watu waliyo yapata kupitia Q-net.

Ninatamani niandike zaidi ila naomba niishie hapa na NINAWAOMBENI SANA SANA WANA JF MSICHOKE KUELEKEZA WATU kwasababu vijana wapya wanaingia mjini na utapeli upo.
Duuh nakumbuka hawa jama walikua na ofisi nje kwetu makumbusho 2018
Nikaulizia wakaniambia 4M
Sasaivi naona wamepanda mpaka 6M
Kiukweli kwa kipindi kile kilichobisaidia sikua na hio ela
Ila hao jamaaa ni wanaku manipulate unaona utajiri huu apa ,,, wana brain wash
Huyo ndugu yako mkuu mpaka umtoe hapo umuombee pia maana sio kawaida
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom