Michael Jackson - Thriller

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Sep 15, 2024
146
166
images-26.jpg
images-24.jpg
images-25.jpg
MICHAEL JACKSON - "TRILLER"

Mwigizaji na mwanamitindo Ola Ray aliyetokea kwenye Video ya 'Thriller' ya Michael Jackson inadaiwa kuwa alilipwa kiasi cha pesa $2,500 sawa na Tsh Milion 6.8 wakati huo1983 ambazo ni sawa na $8,000 Tsh Milion 21.8 leo.

Hata hivyo Ola Ray alisema kwamba alitaka kufanya Video hiyo bure kwa sababu ya jinsi alivyokuwa shabiki mkubwa wa Michael Jackson.

( katika picha ni huyo dada ndio mwana mtindo anaitwa. ola Ray)

Thriller" ni kibao cha Muziki kilichotamba sana mwaka 1984 ambacho kiliimbwa na msanii Michael Jackson.

Kibao hicho kili rekondiwa katika studio ya Epic. Nchini Marekani, kilishika nafasi ya nne kwenye chati za Billboard Hot 100 na namba moja kwenye chati za Radio & Records, wakati nchini Uingereza, kilishika nafasi ya kumi.

Mnamo tar. 20 Februari 2006, single hii, vilevile video yake, zote zilitolewa tena kwenye albamu ya nyimbo mchanganyiko ya Visionary:

The Video Singles. Video ya Thriller ulitazamiwa na MTV[1] kama muziki bora wa video wa "muda wote" (karne), na wenyewe unafikirika kuwa kama ndiyo moja ya alama ya nyimbo za Michael Jackson. Wimbo ulitolewa mapema kabisa nchini Uingereza, mnamo mwezi wa Novemba 1983.

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202

#funguka

Je? Ni video ya msanii Gani wa Bongo fleva kwa sasa iliyotengezwa kwa gharama kubwa na inasumbua katika chart mbalimbali , bila kusahau kuwania Tuzo kubwa ulimwenguni..
 
Back
Top Bottom