Miaka takribani 50 ya Uhuru Tanzania: Ni yapi ya kujivunia?

Labda tujivunie "amani na utulivu" au...
Zaidi ya Amani na utulivu. vitu vingine vya kujivunia ni pamoja na:
-Umoja wa watanzania
-Kuanzishwa kwa Mpango wa kuboresha Elimu ya Msingi(MMES).
-Kuongezeka kwa vyuo vikuu
-Utaratibu wa kubadilishana uongozi kila baada ya miaka kumi.
-Kupungua kwa vifo vya watoto, ingawa vifo vy kina mama viko pale pale.
-Kuchangia ukombozi wa Nchi zilizo Kusini mwa Afrika.
-Watanzania kushika uongozi katika taasisi za kimataifa-UN na UN-HABITAT

Napata wakati mgumu kidogo kukumbuka mengine mazuri ambayo tunaweza kujivunia.
Naomba mchango wa mengine ya kujivunia.
 
Tanzania inafikisha miaka 46 ya Uhuru tarehe 9 Disemba 2007. Ningependa kuwakaribisha wadau kujadili mafanikio makubwa na ya msingi ambayo tumeyapata na vile vile kujadili changamoto tulizonazo na jinsi ya kuzitatua.
Hakuna kabisaa!
 
Tumeuza NBC, TTC(Sigara), Tanzania Breweries, Tunabinafsisha Mbuga za Wanyama, Tumegawa madini,Viongozi wetu wanaishi kama wapo peponi, zahanati hazina dawa, Katiba yenye viraka,


Shule za msingi, sekondari, vyuo na Vyuo vikuu vimeongezeka, Tuna baraza kubwa la Mawaziri(Limevunja rekodi), Jengo Jipya la Bunge, Amani(hapa nina wasiwasi, manake watz wengi hawana uhakika wa chakula), Demokrasia ya Vyama vingi.

Kwa ujumla matatizo yanaongezeka kuliko mafanikio. Kama ingekuwa ni graph basi ungeona gradient inashuka tangu tulipopata uhuru mpaka leo. Ukiangalia mafanikio mengi yalipatikana 60's and 70's.
 
Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa usanii, na kuonekana ni sifa muhimu katika mafanikio ya mtu in the bongoland.
 
jamani la kuondoshwa kodi ya kichwa vipi si la kijivunia? ilikuwa watu huhama nyumba lkn sasa buheri wa hamsa wa hamsini

Eeeeh. Tuwapongeze CHADEMA. Ndio walianza kufuta kodi za manyanyaso waliposhinda kuwa chama kiongozi( wenyewe CCM wanajiita tawala) kule Karatu. CCM ikaiga hii sera. Lakini wamerudisha michango ya manyanyaso kimya kimya kupitia MMEM na MMES.

Asha
 
Kesho ni siku ya Uhuru. Itakuwa vizuri kama wadau mtakaofuatilia kwa sherehe hizi mkatuleta kwenye JF mafanikio na changamoto yatakayoainishwa na waheshimiwa kesho.
Naomba kutoa hoja.
 
Miaka 46 ya Uhuru na changamoto zijazo

2007-12-09 10:34:51
Na Mhariri

Leo Taifa letu linasherehekea miaka 46 tangu tupate uhuru mwaka 1961. Kwa uchambuzi wa haraka haraka tunaona kuwa tumepitia katika mlolongo wa mambo mengi sababu ni dhahiri Tanzania ya 1961 si ya 2007.

Awali ya yote tunapongeza kazi kubwa iliyofanywa na serikali zilizopita hadi iliyopo madarakani hivi sasa ambazo zimefikisha taifa hapa lilipo.

Kubwa na ambalo yafaa tujivunie ni kudumishwa kwa amani, utulivu na umoja wa kitaifa ambavyo vimeweka kando pamoja na mambo mengine uasi, chuki za kikabila na vita kama ilivyo kwa baadhi ya majirani zetu.

Hata hivyo, wakati tunasherehekea leo, hatua budi kutizama changamoto ambazo zinalikabili taifa ambazo yafaa zifanyiwe kazi kwa dhati.

Kiuchumi, bado maisha bora kwa wananchi hayajawa dhahiri kwani bado masikini wanaongezeka na matajiri wanakuwa matajiri zaidi.

Ni muhimu iandaliwe mikakati kabambe ya kusaidia wanyonge. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinagawanywa ipasavyo ili kuendelea kulinda amani tuliyoijenga kwa miaka mingi.

Ikumbukwe watu wenye njaa na fukara si rahisi kuwatawala. Wakati wote ni purukshani, uhalifu huongezeka na kadhalika.
Uboreshaji wa huduma za jamii uzingatiwe hasa hospitali.

Siyo siri kwamba Watanzania wengi hufa kwa kushindwa kujitibu na kuendelea kwenda kwa waganga wa kienyeji, wanawake wengi hufa kwa kushindwa kwenda hospitali kujifungua kwa ajili ya umbali na huduma duni na kuombwa rushwa.

Miundombinu na nishati bado tunategemea reli ya Muingereza na Mjerumani mji, Mkuu una barabara mbili kuu za kuingiza na kutoka mjini alizojenga Mwingereza za Bagamoyo, Morogoro na Pugu tunahitaji mabadiliko.

Umeme ni tatizo tunaendelea kuishi kwenye miradi ya umeme iliyobuniwa na kuasisiwa na Mwalimu Nyerere mfano Mtera, Kidatu , Nyumba ya Mungu na Hale. Vyanzo vingine vibuniwe kuboresha sekta ya umeme.

Nchi yetu ni tajiri lakini watu wake hawana maji mji mkuu Dar es Salaam mpaka leo tunaendelea kutumia maji kwa vyanzo vya Ruvu na Mtoni alivyoacha Muingereza tuwe wabunifu zaidi kusaidia kupunguza matatizo ya watu wetu.

Taifa letu limebahatika kuwa na rasilmali nyingi pengine kuliko taifa lolote la Kusini ya Sahara. Lakini lindi la umasikini bado ni kubwa na uchumi wetu haujaonyesha matumaini makubwa.


Kama tatizo ni sera au sheria zetu, basi maeneo hayo yatizamwe ili tuondoke hapa tulipo tuelekee kwenye neema zaidi.

Ni imani yetu kwamba serikali yetu ya Awamu ya Nne itazishughulikia kwa makini changamoto hizo na nyinginezo kwa lengo la kuinua hali bora ya maisha ya Watanzania. Hakuna kisichowezekana kama nia ipo.

Na zaidi ya yote, wananchi yafaa kuweka nguvu zetu pamoja kwa kushirikiana na serikali ili kukabili changamoto hizo ambazo nyingi ziko ndani ya uwezo wetu.

Kila mmoja wetu awajibike pale alipo na ashiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa letu. Tusitegemee wageni toka nje watuletee maendeleo bali nguvu zetu wenyewe. Kila mtu ashiriki itawezekana.

* SOURCE: Nipashe
 
Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa usanii, na kuonekana ni sifa muhimu katika mafanikio ya mtu in the bongoland.


Ndiyo invicible, usisahau pia tumekuwa washindi wa BIGBROTHER kutokana na malezi na makuzi mazuri ya CCM (lol!)
 
Miaka 46 ya uhuru; vijana hawajawezeshwa - Lwakatare

na Dauson Harold na Amana Nyembo


LICHA ya Tanzania kutimiza miaka 46 ya Uhuru, bado vijana hawajawezeshwa kuwa mstari wa mbele katika kudai haki na kutokuwa waoga, ukizingatia wao ndio kundi muhimu linalotakiwa kujadili hatima ya nchi katika kuleta mabadilikoya kisiasa, kielimu na kukuza uchumi.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatare, katika kongamano lililoandaliwa na vijana wa chama hicho kujadili miaka 46 ya uhuru na nafasi ya kijana katika kuleta mabadiliko katika nchi yake.

Lwakatare alisema vijana ni nguvu kazi ambayo inategemewa na inayoweza kubadili sura ya nchi na kupata maendeleo, lakini kundi hilo limekuwa halipati nafasi kutokana na kijana kukulia katika mazingira magumu ambayo hayampi nafasi.

"Tangu nchi yetu imepata uhuru sasa ni miaka 46 ambayo ni umri wa mtu mzima na ambaye ana wajukuu, lakini rasilimali tulizopewa na Mungu bado hazijaweza kutunufaisha kwa kipindi chote hicho kutokana na vijina wengi kuishi maisha yasiyokuwa na msimamo.

"Kupata uhuru na kuwa huru ni vitu viwili tofauti… vijana wetu hawako huru katika siasa na kupata elimu iliyo bora hali inayosababisha akili zao zinasinyaa, lakini nchi zilizoendelea taasisi za elimu zimekuwa maeneo muhimu ya kuzalisha vijana wanaoleta mabadiliko katika maendeleo," alisema.

Alibainisha kuwa suala la ufisadi linaanzia katika familia na iwapo kijana atakulia katika mazingira ya ufisadi naye pia atakuwa fisadi katika biashara na hata siasa, hivyo lazima kuwe na changamoto katika mzingira yanayomzunguka kijana anapokuwa.

Alisema CUF ina mikakati kuanzia mwakani kujenga jumuiya za vijana wasiokuwa waoga na walio tayari kutafuta maendeleo kwa kudai haki na si kwa njia ya kudanganywa kwa kupewa fulana au kupikiwa pilau.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Juma Duni Haji, alisema kuna tabia ya kusifia serikali kila mara kuwa inafanya vizuri, lakini alichogundua ni kwamba uhuru ulidaiwa kwa ajili ya kuondoa umasikini, ujinga na maradhi lakini kwa sasa matatizo hayo yamezidi.

Alisema hata watawaka wa leo wameshalibaini hilo lakini wameshindwa kulifanyia kazi ipasavyo na kuishia kubadili majina ya mikakati ya kupambana na matatizo hayo bila mafanikio.

"Tumekuwa tukisia mikakati na mipango mingi, mara kupunguza umaskini, mara Mkurabita na pia kuna Mikopo ya JK, lakini hii yote ni kuwafanya wananchi kusahau," alisema.

Mtoa mada katika kongamano hilo, Ndimara Tegambwage, alisema sasa vijana waangalie mbele na kuona siasa ya sasa ni yao na kuangalia mambo kwa makini na wawe tayari katika kujenga chuki na kuona wana haki ya kuingia kwenye madaraka katika vyama vyote vya siasa.

TANZANIA DAIMA
 
mich.JPG


Kipanya na miaka 46 ya Uhuru
 

Attachments

  • mich.JPG
    mich.JPG
    25.9 KB · Views: 41
Kusema kwamba hakuna mafanikio yoyote tuliyopata tangu tupate uhuru ni DHAMBI to say the least. Hebu tufanye mjadala wa kiutu uzima, tuangalie mazuri yaliyopo; mabaya tumeyasema tangu JF ianzishwe; hakuna haja ya kuyarudia hapa; hapa tuzingatie yale MAZURI, ambayo tunaweza kuwaambia hata jirani zetu wa nchi jirani kuwa kwa hili watanzania tumejitahidi. Kwa mtindo wa kukandia kila kitu tunajiharibu akili wenyewe, itafikia mahali hata mtu utashindwa kutetea nchi yako mbele ya wageni.
Mimi najivunia mambo kadhaa;
1. Uhuru (mtu akitaka kuudefine, fine, lakini ukweli ni kwamna tuna uhuru)
2. Umoja (makabila mia na ushee lakini hakuna ukabila, acha ule unaosemwa na Mswahili and company kuhusu TRA and the like.
3. Amani (hata kama ni ya woga lakini ipo)
4. Lugha moja inayowaunganisha watanzania wote (ona wengine wanavyopata shida kwa ajili ya kuongea lugha tofauti)
5. Kukua kwa kiwango cha elimu. Vyuo vimeongezeka; idadi ya wasiojua kusoma imeshuka sana; upeo wa kufikiri unapanda chati (kwamba tunajadili mambo kiufundi hapa JF ni ushahidi tosha wa hilo
6. Demokrasia umekua. (hii kelele hapa JF nayo ni demokrasia; kelele za Zitto bungeni ni demokrasia; Kuzomea viongozi ni demokrasia(inayojieleza kinamna)maandamano ya waislam kupinga ujio wa Papa ni demokrasia; magazeti kuchora vikatuni vya kumsema raisi waziwazi ni demokrasia, nk nk
7. Kujenga na kulinda heshima ya nchi katika mataifa mengine. ( mtabisha hadi asubuhi lakini tukubali tanzania is a name you can be proud of in some corridors..Jk kwenda kuwa Mwenyekiti katika vikao nyeti huko Ny kila mara sio jambo la kawaida, kuna nchi ziko juu kiuchumi lakini hazipati heshima iliyonayo Tz. Uteuzi wa mama Asha Rose Migiro ni kielelezo cha heshima hiyo.)
8. na mengine madogo madogo

Ugomvi wetu ni kuwa hatujaendelea kwa kiwango ambacho tungetakiwa tuwe tumeendelea kwa kuzingatia mazingira mbalimbali; lakini sio kwamba hatujabadilika kabisa tangu uhuru

Guys, lets give credit where its due
 
WanaJambo wenzangu, hii kwa kweli hoja kubwa sana na ya nguvu na mjadala ni mzuri. Kwa kweli naomba msome interview hii ya Baba wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere mwaka 1998 miezi kadhaa (less than a year)kabla ya kifo chake... Kwa kweli uisome uielewe kisha uangalie kama kweli hatujafanikiwa, mimi naamini mafanikio yapo (albeit small as compared to expectations)....
Najua wengi tuna(wana)sema kwamba umasikini wetu ni kutokana na sera za Mwalimu na mambo mengi, lakini mimi kama MTanzania nimesoma interview hii na kwa kweli nimegundua mapungufu mengi niliyokuwa nayo kuhusu mambo yote yaliyomo ndani ya "Sera ya Ujamaa na Kujitegemea" pamoja na so-called "Mwalimu Ideologies"

Tafadhali soma (soma in between the lines) kisha tujiulize swali hilo "Miaka 46 ya Uhuru - ni yapi ya kujivunia"

Naomba kuwakilisha......
 
Kusema kwamba hakuna mafanikio yoyote tuliyopata tangu tupate uhuru ni DHAMBI to say the least. Hebu tufanye mjadala wa kiutu uzima, tuangalie mazuri yaliyopo; mabaya tumeyasema tangu JF ianzishwe; hakuna haja ya kuyarudia hapa; hapa tuzingatie yale MAZURI, ambayo tunaweza kuwaambia hata jirani zetu wa nchi jirani kuwa kwa hili watanzania tumejitahidi. Kwa mtindo wa kukandia kila kitu tunajiharibu akili wenyewe, itafikia mahali hata mtu utashindwa kutetea nchi yako mbele ya wageni.
Mimi najivunia mambo kadhaa;
1. Uhuru (mtu akitaka kuudefine, fine, lakini ukweli ni kwamna tuna uhuru)
2. Umoja (makabila mia na ushee lakini hakuna ukabila, acha ule unaosemwa na Mswahili and company kuhusu TRA and the like.
3. Amani (hata kama ni ya woga lakini ipo)
4. Lugha moja inayowaunganisha watanzania wote (ona wengine wanavyopata shida kwa ajili ya kuongea lugha tofauti)
5. Kukua kwa kiwango cha elimu. Vyuo vimeongezeka; idadi ya wasiojua kusoma imeshuka sana; upeo wa kufikiri unapanda chati (kwamba tunajadili mambo kiufundi hapa JF ni ushahidi tosha wa hilo
6. Demokrasia umekua. (hii kelele hapa JF nayo ni demokrasia; kelele za Zitto bungeni ni demokrasia; Kuzomea viongozi ni demokrasia(inayojieleza kinamna)maandamano ya waislam kupinga ujio wa Papa ni demokrasia; magazeti kuchora vikatuni vya kumsema raisi waziwazi ni demokrasia, nk nk
7. Kujenga na kulinda heshima ya nchi katika mataifa mengine. ( mtabisha hadi asubuhi lakini tukubali tanzania is a name you can be proud of in some corridors..Jk kwenda kuwa Mwenyekiti katika vikao nyeti huko Ny kila mara sio jambo la kawaida, kuna nchi ziko juu kiuchumi lakini hazipati heshima iliyonayo Tz. Uteuzi wa mama Asha Rose Migiro ni kielelezo cha heshima hiyo.)
8. na mengine madogo madogo

Ugomvi wetu ni kuwa hatujaendelea kwa kiwango ambacho tungetakiwa tuwe tumeendelea kwa kuzingatia mazingira mbalimbali; lakini sio kwamba hatujabadilika kabisa tangu uhuru
Guys, lets give credit where its due

Mkuu heshima mbele..
Hapo umeisha maliza mjadala mkuu, haswaaaaaaaaaaaa.. haturidhiki na tulipo, kwani hatupaswi kuwa tulipo baada ya miaka yote 46, pamoja na utajiri wote wa asili alio tujalia maulana!
 
Binafsi nitarudia mada hii kuizungumza kwa mtazamo wangu binafsi kwani wote waliotangulia wmekuwa na tafsiri zao tunapofikia matumizi ya neno maendeleo.

Kwa hakika Tanzania imepiga hatua kubwa sana ktk makuzi yake ya kiumri, yaani yapo mabadiliko mengi sana ya watu na miji yetu lakini hatuwezi kusema kuwa haya ni maendeleo hali maisha ya wananchi wake yamezidi kuwa duni kabisa.
Toka tumepata uhuru maisha ya Mtanzania yamekuwa yakikadiriwa kuwa pato la mwananchi ni chini ya dola moja kwa siku na sidhani kama kuna mtu anaweza kutupa data kamili la ongezeko la senti hizo na thamani yake toka tupte uhuru kwani uwezo wa mwananchi bdo ni duni na wengi tunapima mabadiliko ya kisayanasi duniani - availability ya vitu kuwa kigezo cha maendeleo yetu. hata huko Guinea Bissau kuna cellular phone hatuwezi kusema nchi imeendelea ati kwa sababu simu zimeweza kufika hadi kwao wakati uwanja wa biashara duniani (Utandawazi na soko huria) ni wazi leo hii kuliko wakati wowote ule.
Nchi haina Umeme, maji, Hospital kulingana na makuzi ya miji ama population yetu.
Wakati tunapata Uhuru wa bendera, Tanganyika ama niseme Tanzania bara ilikuwa changa sana na pengine nchi maskini kuliko nchi zote huru za wakati huo..
sasa tunapopima mafanikio ni muhimu tufahamu kwanza ni yapi tunayotaka kuyazungumzia kwani neno UHURU lina tafsiri kubwa zaidi ya Umoja, demokrsia, makabila na kadhalika kwani haya yote ni matokeo ya Utawala uliokuwepo na yanaweza kutokea chini ya Mtawala mkoloni. Kuna nchi kadhaa ambazo zimetawaliwa hadi leo zimeweza fikia mafanikio kama haya kwa sababu lengo la kupata UHURU hutokana na kudhalilishwa kwa wananchi wake kiuchumi na Siasa hutumika kama chombo cha kuweza kufanikisha malengo haya hutumika kama nyenzo itakayoweza kuharakisha UHuru huo wa kiuchumi... hii ndio hatua ya kwanza tuloanza nayo sasa tutazame wapi tumefikia ktk kuutafuta Uhuru huo. Je, umeshapatikana?
Nitapenda sana kufahamu mafanikio yetu ikiwa tutaweza kuzingatia nini maana ya UHURU na malengo yake kisha tupime mafanikio hayo kulingana na UHURU huo...
Hatuwezi kusema Tanzania imefanikiwa kiasi fulani kwa kutazama vitu nje ya UHURU wenyewe kwa mfano kutaja idadi za shule hali Tanzania chini ya mkoloni tulikuwa hatufiki millioni 18 leo tumesimama millioni 40, hilo ongezeko la watu tunalipa nafasi gani ktk upimaji wa mafanikio haya!...miji yetu ilikuwa midogo leo hii imepanuka sana na idadi ya wakazi wake imeongezeka mara dufu ukichanganya na wageni tokanchi jirani lakini mapanuzi ya mahitaji ya miji hii imekuwa chini ya kiwango cha ongezeko hilo kisi kwamba hatuwezi kuweka madai ya kuongezeka nguzo la umeme hali asilimia ya wananchi wasiweza kupata umeme bado imesimama pale pale...
Kama alivyosema Mwanahaki, wananchi wengi wamechoshwa na hawa watalawala weusi ambao kwa tafsiri yo Uhuru wetu ulikuwa ni kumwondoa Mkoloni na nafasi yao wakamate watawala weusi.
Ni kipi leo hii hawa watawala wetu weusi wanachokinya tofauti na mkoloni kiasi kwamba maana ya neno UHURU tumeweza kulijengea mafanikio. Binafsi hat Muungano wetu sii jambo la kujivunia kwani chini ya mkoloni ingewezekana kabisa nchi zetu kuungana na wala sio mkoloni aliyesimamisha muungano huo. Kwa hiyo tutzame kilichotufanya tuweke madai ya UHURU na leo hii tumefanikisha kitu gani...
Bila shaka la kwanza kabisa ni kuwa na viongozi wetu wenyewe ambao kwa sauti za wananchi wengi hawa ni Viongozi wa kudumu sawa kabisa na watawala wakoloni.
 
Azimio jipya,
Ndugu yangu sgukran sana kwa kipande ulichotupa link. Huyu mwandishi Robert Mndeme bomba sana na hsa nukuu hii hapa imenifungua:-
Kutoka kitabu 'Maadili ya Taifa na Hatima ya Tanzania', somo la 'Mtazamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu ukombozi', Ibrahim Mohamed Kaduma anaandika: "Wakati wa uhai wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Julios Nyerere, alitamka kwamba...Ukombozi wa Mtanzania hautakamilika mpaka kupitia hatua kuu tatu: Uhuru wa bendera, Uhuru wa fikra na Uhuru wa kiuchumi.

Tatizo kubwa la Azimio la Zanzibar lilikuwa kuruka kipnde cha uhuru wa Fikra kuingia Uhuru wa kiuchumi. Pengine yawezekana tulichukua muda mrefu sana wakati wa Nyerere tukijazwa Ujinga kwani hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kujikomboa kifikra hasa baada ya kuondoka ktk Ujamaa na kuingia Ubepari. Tulikuwa tumeandliwa kutazama upande mmoja tu na kuwa Ubepari ulikuwa shetani na dhambi kubwa kwa hiyo hatukuweza kujiandaa kifikra jinsi ya kukabiliana na shetani huyo...bado leo hii wananchi tumejaa watumwa wa fikra za mkoloni na viongozi wetu wamechukua nafasi ya mkoloni kuendeleza tawala zote mbili FIKRA na UCHUMI.

Inabidi nikitafute hicho kitabu cha Ibrahim Mohammed Kaduma.....
 
Back
Top Bottom