BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,810
Karibu kwenye mfululizo mwingine wa maandishi juu ya Hip Hop Kulture, This time tunafanya reflection ya miaka 20 ya Mr Blue ndani ya Rap Game.
For the past Two weeks, Mr Blue katokea sana kwenye Timeline yangu pale Youtube na pia Instagram. Being a Philosopher I always know when am asked by the Universe to do something. So here it is.
Kwanza kabisa tofauti na washiriki wengi wa hip hop ya Bongo, Blue hajawahi kuwa mwanangu kwa maana we have spent time together kama ambavyo nimefanya na wengi ndani ya Game.
Hivyo maandishi haya yatahusu Philosophical reflection ya nini Blue kawakilisha kwenye Rap, na ni namna gani muziki wa Rap unao uwezo wa kumtoa mtu kule chini kabisa na kumpa ramani lakini pia kumfanya awe mtu bora zaidi kwa wengine ukiacha mafanikio ambayo anayapata.
Yes, Superstar anayetokana na Muziki wa Rap mara nyingi sana huwa anakuwa na Street Codes ambazo haziwezi kubadirishwa na pesa pekee in a long run. How? Tutafika huko.
Nakumbuka mara ya mwisho namuona Blue kwenye Show nilikuwa Singida pale Regency Hotel & Resort 2020 kama sikosei. Nilikuwa naishi pale kwa siku mbili tatu nilipokuwa Singida kikazi. Na usiku mmoja Mr Blue alikuwa na Show pale.
Na actually nilifika Singida na siku ya kwanza sikufikia Regency, Lakini night nikaenda Club moja pale nikakutana na wanangu Joslyn (Mzee wa Perfume) na mwanetu mmoja wa kuitwa Ommy.
Wakanambia umefikia Hotel gani? Nikawatajia wakasema amia Regency bana! Maana Ommy alikuwa Manager pale. So wakanikwala.
Hivyo after kama siku moja hivi ndio Blue akawa na Show Pale, nikaweza kuwepo kwa hiyo Show and we hang out kwa muda mchache sana so hajawahi kuwa mwanangu.
Lakini Muziki wa Mr Blue na anachowakilisha kwenye Rap Game ndio nataka tukifanyie reflection hapa. Ni miaka 20 sasa, nini ambacho Mr Blue anatufundisha juu ya Muziki wetu wa Rap na Kulture yetu ya Hip Hop.?
Blue ni miongoni wa Rappers ambao nawakubali kwa ujio wao kwenye Rap na zaidi ya yote kwa kuvumilia mengi sana na akabaki kuwa yeye.
Kwa wanaokumbuka shule zetu za Sekondari kulikuwa na Tittle ya debate moja maarufu inauliza “Money or Education which is More Important” Blue ni miongoni mwa Rappers wachache ambao wanaweza wakatujibia swali hili kwa ufasaha zaidi.
Hili swali linaweza likajibiwa vyema kwenye Hip Hop na magenge ya aina 3. Genge la kwanza ni la Mr Blue na Sugu. Hawa na wengine wengi waliacha shule na kujikita kwenye muziki huku wakiwa na record ya kufanya vizuri tokea shule ya Msingi. Kwa namna moja au nyingine Rap ili-affect masomo yao.
Genge la pili ni Mwana FA, Nikki Wa Pili, and the likes hawa wameenda shule na wamepata kujulikana na watanzania wengi kupitia muziki wa Rap. Kwa namna moja Rap haikufanya wasisome.
Lakini Genge la Tatu ni la watu kama Gego Master, Lugombo Makanta, Nikki Maujanja, Nyeke Da Nyiki, Mfalanyombo and the Likes, hawa wameenda Shule na hata siku moja hawajawahi kuiacha Kulture yao. Wapo wengi kwenye office nyingi.
Lakini swali ambalo Magenge hayo yatalijibu tunali-twist kidogo swali litasema “Shule Na Muziki Bora nini?”
Blue anasema mara ya kwanza alipelekwa Studio na Dogo Hamidu -Nyandu Tozzy. Hapa you have to stop kidogo.
Ukisikiliza Collabo ya Nyandu Tozz, Blue na Rayvan ya kuitwa “Tupa Mawe“ blue anasema “Ona Napiga Collabo na Mwanangu wa Maisha” akimaanisha Nyandu Tozz. This is how far back they go.
Tunawazungumzia watoto wadogo kabisa kuingia kwenye Muziki wa Rap. Blue ameanza Rap ni dogo hajafikisha miaka 18. Anakuja na hit song ya “Mr Blue” ana miaka 15 hivi hapo 2003.
Akijulikana kama Lil Sama hii ikiwa ni effect ya Lil Romeo na Lil Bow Bow kutoka majuu. Na kwakuwa Dudubaya alikuwa anapenda kuona madogo wakichana ndio maana alikuwa na Dogo Hamidu hivyo ilikuwa rahisi madogo hawa wawili kuclick na kuwa sehemu ya himaya ya Mzee mzima Dudu.
Akiwa kama Lil Sama na akiwa na Dudu alirekodi lakini ngoma hazikutoka, ilipokuja kutoka “Mr Blue” kama ngoma ndio ikaja sasa kubadirisha kila kitu including Jina.
Part 2 tutaanza sasa kupitia kismati kinacholetwa na rangi ya Blue na tuweze kuelewa persona aliyojitengenezea Blue kwa kutumia rangi hii.
This is Metaphysical analysis ambayo sio kwamba kijana huyu wa miaka 15 kipindi hicho alijua anachofanya laaaaaaah! Hii ni kukuonyesha kuna frequency uki-Tap inn kwa kujua au kutokujua zenyewe zinakufanyia kazi.
Kama uliwahi kusoma ngazi saba za Emcee kama ambavyo nilizipanga kuziunganisha na Chakras basi utaelewa kwanini Rangi ya Blue ni Throat Chakra na ni ngazi ya juu sana. Sasa Mr Blue alichagua Throat Chakra hata kama alikua hajui ni nini
Mwananuziki Regina Spektor alisema “Blue lips, Blue Veins, Blue, the Colour of the planet from far, far away.” Blue is the most human Colour. Why? Because blue is non-threatening, blue is all about calmness and relaxation.
Colour blue represents Communication, Speaking, Listening, Purification, Creativity, Aunthentic self Expression, Body Language.
Let me take you back, Your first social media had a blue icon (Facebook), how about Twitter, Apple store, Email, LinkedIn, Zoom !? You know what they do represent? Self-expression.
Sasa basi kwa kijana huyu wa Kuitwa Lil Sama kuamua kuachia ngoma ya kuitwa “Blue Blue” kwa kujua (kitu ambacho siamini) au kwa kutokujua alikuwa ame-Tap-into this frequency of the colour blue. And that frequency changed his name.
Karudie kusikiliza ile ngoma ya kuitwa “Blue Blue” at 15 Years Old the Kid was expressing high level of creativity(Blue), Communication (Blue) , Body Language (Blue) he was so energetic na ukiangalia ile Video unakutana na Redbull (Energy and Blue).
Sky looks Blue, Ocean looks Blue na ndio maana mwanadada Regina Spektor kwenye ngoma yake ya “Blue Lips” alisema Blue is the colour of planet from far.
blue is non-threatening, blue is all about calmness and relaxation. Na hivi nadhani wengi ndio wanamchukulia Mr Blue. Na ndio persona yake.
Watu wanabatizwa kwenye maji. Tunajua maji ni colorless lakini blue inawakilisha maji and hence purifucation zote zinafanyika kwenye maji. Hivyo ulivyoona Blue inawakilisha purification hapo juu hiyo ndio sababu. This Nigga never lost his soul. did you notice that?
And you know what? Blue is illusion (Maisha yote ya Kibitozi aliyokuwa anayaonyesha alikuwa anawaaktia na wengi mliamini) yes we say out of blue. You know anything about Blue Monday? The weekness of this color energy is depression. Na tutafika huko.
The kid was innocent, the kid was pure. Can you imagine at 15 Years old unaanza majukumu ya kulisha familia? Ukienda shule, nyumbani watu hawali, ukifanya Muziki unapata hela, ukipata hela mama na ndugu wanakula. Unafanyaje?
Hivyo Blue akakata shule form Two pale, na kuanzia hapo ndio hii story ya Miaka yake 20 tunaipitia, Tujifunze na tujitafakari wote kwa pamoja ambao tupo kwenye hii Kulture “Shule na Muziki bora nini?”
Hivi umeshajua ya kwamba watoto waliolelewa na mama pekee na wakaingia kwenye Rap wanakuwa na vipaji vikubwa sana? Do you know why?
Blue kwa muda mrefu alikuwa na Mama pekee, hii ni kama ritual vile kwenye maisha ya Rappers ambao wanakuja kufanya vizuri kwenye Game ya Rap. Hivyo na yeye alipitia hii ritual. Mzazi mmoja nyumbani mwingine yupo lakini haonekani na pengine hasaidii malezi yako.
Ndio maana baada ya kufaulu vyema shule ya msingi na kuchaguliwa kwenda sekondari hata fedha ya vitu muhimu vya kwenda navyo shule alikosa.
Hivyo umeshajua nyumbani maisha mabovu, lakini ukijaribu kuchana mistari ya wakali kama Professor Jay watu wanaona ebanaaaa! Eeeeeh! Hii kitu unaweza, kwanini? Your throat can take it. And Throat is Blue energy center.
Hivyo Blue aliamini anaweza baada ya kuaminishwa mtaani, japo ni yanki lakini akaona let me try. Kujaribu imo. Mapema tu walete. The first Rapper kuingiza muonekano wa watoto wakali wa kipindi hicho Tanzania. Watoto kama Lil Bow Bow, Lil Romeo. Blue akawa kama sky alionekana kila kona.
Shule na Muziki bora nini? Blue aliona bora Muziki? Yes, Shule akabwaga. Majukumu yakaanza na umaarufu ukapanda. Nimwambie tu hayupo peke yake The God Emcee RAKIM alibwaga shule sababu aliona “Elimu na Pesa bora pesa”.
Familia ya Rakim ilikaa chini na maamuzi yakapita “bora Pesa” achana na Elimu. Today Rakim ni God Emcee. Na hii sio maana kwamba Rakim alitaka pesa kwenye Rap, Nah alipofanya tu pesa zikaja nyingi na yuko shule. Pesa ambayo wazazi wake hawakuwahi kuiingiza kwa mara moja. Tena alitoa ngoma mbili tu.
Lakini baadae,Kati kati ya muziki mr Blue anakuja kugundua what the f..ck.! Yaani naibiwa na naowaona wananiongoza? Mbona hela zinakuja Dusko? Mbona kama vile bora shule? Maana aliona kabisa utoto wangu ndio kitu watu wanatumia kutonipa nachostahili.
Blue anasema kwamba aliwekwa chumba kimoja na Mzungu na Lugha haikuwepo. Nadhani hapa ndio mwanangu akaona kama ningemaliza hadi Sekondari si ningekuwa na Lugha ya kuombea maji? - Doubt inaanza. bora shule.
Muziki (Money) na Shule (Education) ni kama tu swali la Jaymoe la Mvua na Jua. Dully wa kutuambia sisi wa DSM kwamba bora Mvua? Muuza kahawa atauza vipi? Sugu na FA walituambia bora mvua FA akatoa sababu za kisiasa. Sugu akatoa sababu za kutoka Mbeya.
Unadhani ingenyesha Mvua pale kwenye Show ya JayMoe show ingeendelea.? Katika mazingira kama haya ambayo Blue alikutana nayo maishani Shule na Muziki bora nini? -Mwanangu Blue hakukosea bora Muziki, hicho kiingereza tutavumilia.
Hivi ushawahi kujiuliza inakuaje mtoto mdogo wa miaka 15 anajiita Mister (Mr). Have you noticed kwamba hii ni ishara ya kukuonyesha majukumu yalianza mapema sana? Or you just bypassed this sign?
Watu kama Jongwe walikuja kujiita Mr mwaka 1998 this time inatoka Album ya Tatu “Niite Mr Two” at this time he was 26 Years old.
This Kid Blue single ya kwanza na umri ule anajiita Mr haikukushangaza? My Nigga we need to learn from our own. Hip Hop kulture ina kila somo kwa anayetaka kujifunza.
Genge la pili la kujibu hili swali limetuonyesha ya kwamba Shule na Pesa (Muziki) vyote muhimu. Tunaona Mwana FA kati kati ya umaarufu alirudi shule, na shule hii ni chuo. Iliwezekana sababu alimaliza secondary Education.
Lakini tukienda mtoni mwanangu Master kabisa Master P yeye story yake tofauti kidogo. Yeye basketball ndio ilimpeleka shule. Lakini alipopata majeraha ambayo yalifanya asiendelee na Basketball scholarship yake ilikatwa.
Yaani ni hivi, kama unapelekwa College kwasababu ya kipaji chako cha basketball basi wanahitaji Shule na Basketball, ukikosa kimoja unakosa vyote.
Baada ya kukosa vyote Master P alichagua muziki, akapata pesa, akawa maarufu lakini kwasababu level aliyokuwa amefikia kielimu ilikuwa nzuri basi baadae akarudi chuo. Hivyo kabla ya kuacha masomo kwasababu ya pesa kuna level inatakiwa ufikie.
Twende kwa mwanangu Nick Cannon, ni mwaka juzi tu hapa kamaliza 4 Year degree hapo Howard University na bado akiwa maarufu kabisa.
Hili ndio somo Hip Hop inatufundisha kutoka kwenye Genge la pili la Muziki na Pesa bora nini. Genge hili linasema bora vyote. Unatakiwa uweke balance maana in Long run vyote vinahitajika.
Hip means to know, Hip Hop inakuhitaji kujua yale yote ambayo ni muhimu kuyajua. Our 5Th Element ni Knowledge Elimu ya mtaani na Elimu ya Darasani vyote hivyo Hip Hop inakuhitaji kuvijua. Hip Hop ni Elimu huwa hatukimbii shule.
Tunayo kauli inasema Hip Hop ni zawadi ya Mungu kwa watoto wa Mtaani. Kwenye Goma la Blue FT Becka la kuitwa “Pesa” Blue anasema “Nishatembea kwa Miguu kabla ya kuwa Mr Blue/ hakuna sister Duu wala brother duu aliyenijua/ zaidi ya joto mvua na jua/ na msoto ulionikuza nikakua/“
Kilichomtoa Blue kwenye Msoto ni huu muziki wa Rap. Heshimu Kazi. Heshimu Rap. Heshimu Hip Hop.
Lengo kuu la Mr Blue kujihusisha na Muziki wa Rap anasema alikuwa anapenda hii kitu. Hivyo alianza sababu alipenda. Hakuwahi kufikiria kama atapata pesa kupitia hii kitu.
Ukiacha kuupenda Muziki, alitaka kujulikana hilo ndio lengo lake, Watu wamjue ya kwamba yupo. Sasa hapa kidogo tuweke sawa, Ni hivi kuna watu wanayo mafanikio mazuri tu ya kimaisha. Lakini sio watu maarufu.
Hip Hop inakupa Chance ya kuwa Famous, na kupitia umaarufu huo kuna mambo yanakuwa rahisi wewe kuyatatua. Music Connect souls of human beings.
Na ndio maana tunasema music is spiritual, we have been connected na watu kama Jay Z, DMX, 2Pac, Big na hatujawahi kukaa nao popote but their music connect us All. The Power of Music, The Power of Rap Music.
Hivyo tulisema rangi ya Blue inawakilisha uwezo mzuri wa kuwasiliana (Communication) kila Interview ya Mr Blue utakayofanikiwa kuiona anao uwezo mkubwa sana wa kuzungumza na kujieleza.
Na mara chache nilizopata kumsikiliza ni kama vile anasoma sana maandishi ambayo nafundisha kila siku kupitia hii mitandao au miaka yake 20 ndani ya Game basi amepata elimu pana juu ya Muziki na maisha yahusuyo muziki na wanamuziki na Maisha kwa ujumla.
Nilishasema ya kwamba kama ulikuja kwenye Hip Hop just to get Money, maana yake umeingia na mguu mbaya. Watu wapo huku kwasababu wanapenda hii kitu, hawawezi acha hata wawe hawana hata kumi. Blue is one of them, anasema anapenda hii kitu na kwake lengo halikuwa pesa. Alitaka tu ajulikane.
Hivyo akipima mafanikio yake kwa kupenda hii kitu anasema amefanikiwa sana maana licha ya kujulikana ameweza kupata pia uwezo wa kulisha familia yake na kupata maisha nafuu.
Ebu fikiria mtu ambaye ametokea kwenye maisha ya chini kabisa anafanikiwa kuweza kuiwezesha familia yake yote sio watoto wake na mke wake pekee ndugu zake wote kwa upande wa Mama Ake.
Yeye ndio pekee anaonekana anayo mafanikio. Na kwasababu anaujua huo msoto ni jukumu lake kusaidia hao wote. Na anafanya hivyo. Kwa miaka hii 50 ya Hip Hop hiki ndio kitu Hip Hop imewezesha kwa mamilioni ya vijana. Have a respect for this Kulture. Na kama ulikuwa unaichukulia poa think twice.