Miaka 12 ya Bongo Movie bila uwepo wa Steven Kanumba

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
87
103
Steven Charles Kanumba alizaliwa 8 Januari, 1984. Alikuwa miongoni mwa waigizaji maarufu nchini Tanzania.

Aliingiza katika tasnia ya uigizaji miaka ya 90 na na kujizoelea umaarufu mwaka 2002 baada ya kujiunga na kundi la Kaole Sanaa Group.

Aliwahi kupewa tuzo ya mwigizaji bora wa kiume nchini kwa miaka mitatu mfululizo mwaka 2006, 2007 na 2008. Alikuwa mwigizaji wa kwanza kufanya kazi nje ya nchi na waigizaji akiwemo Mercy Johnson.

Alifariki tarehe 7 Aprili 2012 akiwa na umri miaka 28 na kifo chake kimekuwa ni pigo katika tasnia ya filamu.
 
Kanumba alikuwa overrated tu
Ukiangalia movies zake kwa macho ya kawaida yasiyo na upendeleo utaelewa

Hata hivyo aendelee kupumzika kwa amani
 
Kanumba alikuwa ana uthubutu, kwa kizazi cha bongo fleva namfananisha na bwana Naseeb Abdul. Miaka 28 tuu kaacha legacy.
 
Kanumba alikuwa overrated tu
Ukiangalia movies zake kwa macho ya kawaida yasiyo na upendeleo utaelewa

Hata hivyo aendelee kupumzika kwa amani
Yule dada aliyeigiza Kwenye The Shock ya Kanumba unamjua?
 
Kanumba alikuwa overrated tu
Ukiangalia movies zake kwa macho ya kawaida yasiyo na upendeleo utaelewa

Hata hivyo aendelee kupumzika kwa amani
Kanumba legacy yake aliyoacha kwenye sanaa akiwa na miaka 28 hata uishi miaka 200 hutoifikia
 
mwamba alikua mbele ya muda, angepewa nafas ya kuishi mpaka leo basi kina de caprio wangekuja bongo na kiswahili wangeongea, mixer kuiona tz kwenye nomination za oscar awards huko, zile ambitions za kutaka zaid, kutoridhika na alipo na kutaka kufika duniani, ndo kulimtofautisha na wenzake, tuseme r.ip kwa one of goats wa bongo movies.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom