DOKEZO Mhindi tapeli wa viwanja Kigamboni, anataka kutapeli wananchi kwa kutumia makampuni hewa 4

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

taheltz

Member
Jan 26, 2024
19
58
Habari ndugu zangu, nimekutana na utapeli wa kiwanja maeneo ya Kisota Kigamboni.

Mpaka sasa nipo njia panda kupata haki yangu pamoja na wahanga wenzangu zaidi ya 10, ambao tumenunua
viwanja hivyo kwa nyakati tofauti tofauti bila kujuana., ni zaii ya 300m tunataka kutapeliwa, maana viwaja maeneo yale bei ipo juu.

Kwa kifupi tulinunua viwanja hivyo katika kampuni nne tofauti zinazomilikiwa na mhindi mmoja anayejulikana kama SYED ABBAS RIZIV jina maarufu anaitwa ABBAS

Majina ya kampuni zake anazozitumia katika utapeli ni
1) Interflow commercial (T) Limited
2) Rubab Investment
3) Jasman East Africa limited
4) Multimodal transport Africa lImited

Kipindi tunanunua tulifuata taratibu zote za manunuzi, kwa sababu viwanja hivyo vilikuwa na hati, tulienda kufanya search manispaa , na kupita kila sehemu palipohitajika, hadi tukafikia kupata approval ya manispaa katika harakati za kufanya transfer, yani viwanja tumepewa na hati original kabisa na tulizikagua na kuna baadhi walizibeba hadi wizarani zikakaguliwe na zilitambulika ni halali

Katika kipindi cha ununuzi kuna baadhi yetu tulifika katika ofisi za kampuni husika kwa kuelekezwa na madalali, na ili ufike hapo ofisini lazima kuwepo appointment, bila hivyo huingii.

Wakiwa na appointment na wewe, unakuta ofisi kabisa na bango la kampuni, mnazungumza biashara, ila ikifika mahali kwenye malipo, basi mhusika bwana Abbas anasema kampuni tunaifunga kwa hiyo anakupa account nyingine tofauti na ya kampuni ili ufanye malipo, ili kujiweka safe side baadhi yetu walitaka Abbas mmiliki wa kampuni hizo ku-sign, kwamba anaruhusu malipo yafanyike katika accout tofauti za kampuni

Kwa utaratibu huo tumejikuta wengi tukinunua na wengine kununua kupitia kwa mwakilishi wake anayefahamika kama Juma Nkumbi

Mgogoro unaanza baada ya huyo Abbas kukamilisha mauzo ya viwanja vyote. Jamaa anaruka futi 100 kwamba hajauza kiwanja chochote ili hali, kwenye mauziano baadhi alikuwepo mwenyewe na mauziano mengie alikuwa akisimamia muwakilishi wake

Jamaa ili kutuvuruga akaenda kuwekea caveat viwanja vyote, akizuia transfer zote na hapo akafungua kesi kimya kimya bila kutujulisha ili asikilizwe upande mmoja.

Kipindi anaweka mazuio kila mhanga alikuwa anahangaika kivyake ndipo tukaanza kujuana ni kundi kubwa la watu analichezea mchezo na ndipo tukagundua kwamba kuna kesi zishafunguliwa ya kila mmoja

Baada ya kukuta tumefunguliwa kesi kila mmoja wetu hapo ndipo tuka-organize iwe kesi moja, na jamaa alipoona kesi inamshinda, akaanza visa vya kuchelewesha kesi kuanza kusikilizwa, kila siku anakuja na jipya maji yalipo fika shingoni, kesi yenyewe akaifuta kabisa ila caveat/zuio la kuendelea na transfer hakulitoa.

Kutokana na kuifuta kesi hiyo, ikabidi sasa tumshitaki yeye, why anaweka mazuio ili hali na kesi kashafuta. Baada yakuona tumemfungulia kesi amekuja na sababu tele mahakamani akizuia kesi tuliyomfungulia isisikilzwe, yani anavuta vuta muda, na haoneshi nia ya kumaliza kesi na sisi tum- stack zaidi ya mwaka na miezi kadhaa

Visa nje ya mahakama, anaweka walinzi wengi kwenye maeneo yetu, na hata walioanza ujenzi materials zimeanza kuoza, ni hasara kubwa. Anatusumbua na kututesa watu wengi bila mashiko.

Tumeandika barua nyingi kwa vyombo husika wachunguze hizi kampuni zake maaana zimekaa kimichongo, hazilipi kodi, yani kampuni zote zinatumia ofsi moja, na bango la ofisi linabadilika kulingana na mteja wa siku hiyo, na ofsi inafunguliwa kwa appointment maalum

...............
Katika kufuatilia tumegundua jamaa ana kesi nyingi zinazofanana na hizo, na pia ameshatangaza hati zake zimepotea katika magazeti ya serikali, ili hali sio kweli hati tunazo sisi
.....
Ombi langu pamoja na wenzangu , tuanomba jambo hili mliangazie ikiwemo wawakilishi wa vyombo husika vya ardhi, takukuru, TRA na hususani mheshimiwa waziri ambae tumeshafanya jitihada za kumtafuta bila mafanikio , ili aliangazie suala hili kwani sio suala la mtu mmoja, linagusa zaidi ya watu kumi , hivyo kuwa kero kubwa kwa sisi kama wananchi

makampuni haya manne yachunguzwe vizuri , inaonekana yameanzishwa kutapeli na kusumbua wananchi

Majina ya kampuni ni
1) Interflow Commercial (T) Limited
2) Rubab Investment
3) Jasman East Africa limited
4) Multimodal transport Africa lImited

Mtu huyu anaetusumbua ni mhindi anaejulikana kwa jina la ABBAS na hata mawasiliano yake ni 0778 999 999 na msaidizi wake ni 0754 022 897

Hawa watu hawana nia njema na sisi wanatupiga chenga kila siku jambo lisiishe, na wengi hatujui hatima yetu maana viwanja tumenunua ili kujistiri na familia zetu , ila mwaka sasa umeisha jamaa wanatukimbia kimbia mahamani
.....
Natanguliza shukrani, naomba wahusika walifuatilie hili maana ishakua kero ya wananchi

Natanguliza shukrani, Asanteni sana, naombeni ushirikiano wenu
 
Eneo kubwa la kigamboni maeneo ambayo ni potential & premium yanamilikiwa na wenye asili ya wahindi,waarabu au wapemba mfano Scaba Scuba, Akbar, Oil com, Dar es salaam zoo, fun city, water com, Alimu, Manji, Maridori na wengineo.

Ndugu zangu shikamaneni muwe na umoja pambaneni na huyo Abbas, huyo jamaa ni tapeli kipindi cha Magu alikimbia kigamboni naona Sasa amerudi kwa kasi.
 
waziri atusaidie kwakweli, maana uyo mhindi hataki hata kukutana na sisi, anatumia mawakili wenye njaa na kuwapa maagizo tu yeye hatokei
Hapa Jerry Silaa anafaa kabisa kuwasaidia sababu ana moyo huo.
 

Attachments

  • IMG-20240509-WA0000.jpg
    IMG-20240509-WA0000.jpg
    24.8 KB · Views: 26
Eneo kubwa la kigamboni maeneo ambayo ni potential & premium yanamilikiwa na wenye asili ya wahindi,waarabu au wapemba mfano Scaba Scuba, Akbar, Oil com, Dar es salaam zoo, fun city, water com, Alimu, Manji, Maridori na wengineo.

Ndugu zangu shikamaneni muwe na umoja pambaneni na huyo Abbas, huyo jamaa ni tapeli kipindi cha Magu alikimbia kigamboni naona Sasa amerudi kwa kasi.

Scaba scuba ana kesi kibao kigamboooni
 
Mie nikiwa nafanya ishu za malipo (Malipo serious) lazima nivizie angle fulani nipige picha MHUSIKA au Ofisi kisiri siri.

Pia transfer ya hela nalipia kwa SimBank ili nibaki na vielelezo solid..

Mazungumzo huwa nayahifadhi kwa ajili ya follow up... Dunia ya Sasa aisee ni kuishi kisungura.. poleni sana.
 
Back
Top Bottom