Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,497
- 15,210
Hakuna jambo jema kama kufanya kazi ya halali hapa duniani na haijalishi iwe na hadhi gani, bali kikubwa ni halali na inakidhi mahitaji yako hata kwa kiasi fulani
Na kamwe usijisikie mnyonge kwa hiyo kazi ambayo unayo sasa kwani ndio kazi yako,endelea kupambana mpaka pale utakapo fikia katika level nyingine ya maisha
Kumekuwa na kasumba ya baadhi yetu kubeza kazi au shughuli za watu wengine kwakuwa tu tupo katika ofisi fulani fulani ambazo ni mashuhuli,tambua kwamba wote hatuwezi kuwa katika level moja ya maisha,kwahiyo tambua na heshimu kazi na shughuli za watu wengine pia
Nakumbuka wakati naenda kujiunga na masomo ya elimu ya juu,baba yangu alinipa ushauri mzuri sana,alisema Mwanangu huko unakoenda muheshimu kila mtu hata wale wanao fanya usafi vyooni kwani hakika bila wao hamtakuwa na mazingira mazuri ya kuishi
Niliyakumbuka hayo maneno vizuri sana,na kwa hakika nilikuwa nawaheshimu sana na kuwapenda sana,na niliona furaha zao kila mara nilipo wasalimia kwa upendo na tabasamu kubwa,maana imezoeleka mtu akijiona msomi basi kwake yeye watunza bustani na wafanya usafi si chochote kwake
Na huu ndio mtazamo wa wengi wetu,tumejawa na dharau na viburi kwa wale ambao wanafanya kazi ambazo hazina hadhi kubwa,tambua kwamba ewe boss bila mfanya usafi ofisini kwako hiyo ofisi haitakalika
Ewe mwananchi tambua kwamba bila wafanya usafi katika vituo vya mabasi na daladala hizo stand zitakuwa ni majalala,tujenge tabia za kuheshimu kazi za watu kwani hakika zina umuhimu mkubwa sana,ni kwa vile tu tunazichukulia for granted.
Kazi yangu ya hadhi ya chini haibadilishi utu wangu na ubinadamu wangu,bado nabakia binadamu mwenye utashi na utu wangu pia, tuheshimu kazi ya mtu haijalishi ina hadhi ndogo kiasi gani
Ijumaa Mubarak
Ni hayo tu!