Mhe. Simbachawene usimwogope mheshimiwa rais, elimu bure haitekelezeki

Hoja Binafsi: Kiukweli kabisa kuanza na elimu bure kwa levels zote (darsa la kwanza = form IV) haliwezekani kutokana na ukweli kwamba hakukuwa na muda wa kutosha kujipanga kimiundo na kiutawala. Serikali ingeanza hatua kwa hatua, yaani wangeanza darasa la kwanza walioanza mwaka huu, next year wangeongeza madarasa na baadae wangekava madarasa yote. Approach hii ingetoa fursa kwa Serikali kushughulikia changamoto za elimu bure kwa umakini na kuboresha zaidi. Hili lilishakuwa gumu tangu wakati wa kampeni, ila upeo wetu ulitudanganya kuwa linawezekana.
 
Serikali haijaharibu kitu, mbona iko vizuri sana. "WANA MACHO LAKINI HAWAONI, WANA MASIKIO LAKINI HAWASIKII"

Queen Esther

Yaani nashindwa kabisa niseme nini. Siasa mbaya sana! Badala ya hoja unajibu kishabiki!

Kuna watu siyo wafuasi wa vyama(mimi nikiwa mmoja wao) wanapenda Tanzania isonge mbele, wanapochallenge(as opposed na kupiga vigelegele) wanasaidia kuwafanya viongozi kutafakari na kuchukua hatua stahiki na maamuzi sahihi. Sasa watu wote wawe ni wa kusifia tu kama nchi haiwez kufika popote.

Ni uwaz usiopingika suala hili la Elimu Bure lilipaswa kwanza lianze angalau mwez Julai, wakati huo Serikali ingekua ina miez 8 na zaidi, hivyo ingejipanga! Kwa sasa imeharakisha bila sababu yoyote! Mambo ya kitaalam yasifanywe kufuata matakwa ya kisiasa
 
HATA INGEANZAJE MSINGETOSHEKA!!! MKO KAMA TUMBO LA KUZIMU LILIALO NIPEEE NIPEEEE!!!

Queen Esther

Hoja Binafsi: Kiukweli kabisa kuanza na elimu bure kwa levels zote (darsa la kwanza = form IV) haliwezekani kutokana na ukweli kwamba hakukuwa na muda wa kutosha kujipanga kimiundo na kiutawala. Serikali ingeanza hatua kwa hatua, yaani wangeanza darasa la kwanza walioanza mwaka huu, next year wangeongeza madarasa na baadae wangekava madarasa yote. Approach hii ingetoa fursa kwa Serikali kushughulikia changamoto za elimu bure kwa umakini na kuboresha zaidi. Hili lilishakuwa gumu tangu wakati wa kampeni, ila upeo wetu ulitudanganya kuwa linawezekana.
 
Nianze kwa meseji hii niliyotumiwa na Mkuu mmoja wa shule. "Kaka wapi, naomba unirushie 20,000/=, nipo hapa Morogoro mjini nimetoka mlimani leo, nilifika kutoa pesa ya matumizi ya shule. Afisa elimu nimemfuta anipitishie hundi yangu kaniambia nirudi tena bush niitishe Kikao cha Bodi kipitishe kwanza bajeti ya shule na pili bodi iridhie kufanya manunuzi. Nimechanganyikiwa nauli kurudi kijijini 10,000 nikishuka napanda pkpk 10,000 tena. Jumla nauli 40,000/= kuja na kurudi. Kuitisha kikao cha Bodi wajumbe 10 nalipa kila mmoja 20,000/= bado sahani ya wali maharage. Pesa niliyoingiziwa 360,000/ Katika pesa hii asilimia 35 ni uendeshaji wa shule (vitambulisho, shajala, maandalio,ulinzi, umeme, maji na fedha za kujikimu. Na fedha za kijikimu isizidi asilimia kumi ya fedha hizo za asilimia 35. Walimu wa sayansi wa kujitolea nimeshawaachisha. Kwani mwongozo haujawazungumzia kabisa. Kwa hiyo hapa Fizikia,hisabati, biolojia na kemia vijana hawafundishi tena, nirushie tafadhari nataka nilipie chumba sasa hivi hakuna gari za kurudi bush mpaka kesho". Huyu atatoa wapi pesa ya kuitisha kikao cha Bodi , bure bila posho watakuja kweli na maisha yalivyo magumu vijijini na mkwara wote wa Magufuli pesa zimeingizwa mabilioni ole wake Mkuu wa shule atakaye zipiga? Mhe. Simbachawene usiogope kumwambia ukweli Magufuli elimu itakufia, potelea mbali akutoe uwaziri kwani ubunge si utabaki?.
Ndalichako na wasaidizi wako wote katika wizara naomba sana mjipange kikamilifu, ili tuweze kuona muelekeo sahaihi wa elimu yetu nchi
 
Banah wewe acha kupaniki, tatizo watu mmepaniki sio viongozi sio wananchi,sikiliza kwenye jambo lolote zuri hakuna kinachokosa kasoro, hii notion ya kulalamika kila wakati sio sahii kwa kulijenga taifa,mwanzo wakuitekeleza hii sera ya elimu bure lazima iwe na changamoto, lakini itafika mahala ita-gain momentum, kila mtu awajibike katika nafasi yake sio bla bla na kuilaumu serikali kwa kitu kila wakati ni makelele tu,jua serikali ni pamoja na wewe
 
ELIMU BURE IMEANZA KWA MAFANIKIO MAKUBWA MNO SEMA MIRIJA YA ULAJI YA WAKUU WA SHULE NA BODI IMEKATWA NA NDIO WANAONGOZA KWA KULALAMIKA WEE HUKU WANAFICHAFICHA UKWELI KUWA WIZI WAO UMEBANWA.MALALAMIKO MENGINE MENGI NI YA KIPIMBI TU.

BINAFSI SINA SHAKA NA HILO,SHIDA YANGU KUBWA NI KUTAKA KUJUA HIZI SHULE ZA SERIKALI AMBAZO HAZIKO KWENYE MPANGO WA ELIMU BURE KULIKONI?MFANO HII ILIMPIO YA HAPA DAR NI MOJA KATI YA HIZO.KWANINI ZENYEWE SIYO BURE?KWANINI SERIKALI IENDELEE KULIPISHA ADA NA MICHANGO KWENYE SHULE HIZO?
 
Bodi ya shule haipo kwenye muongozo wa malipo,bodi hailipwi chochote kwa mujibu wa sera ya sasa.
 
20000 kwa mjumbe wa bod tena kijijini na sahani ya wali maarage juu.!!!!!!!!!

hapa nahitaji elimu kidogo kujustfy vinginevyo huu ujumbe ni hekaya yu . tuambie huyo mwalimu ni wa milima ipi hiyo pikipiki 10000
Umezaliwa Muhimbili, likizo siku moja kamsalimie bibi na babu kijijini au baba kashawahamishia babu na bibi mjini.Kuna maeneo pkpk 25,000.
 
wakuu wa shule baada ya kukatiwa mirija ya ulaji wa pesa z michango ya wazazi kila siku wana kazi ya kulalama tu humu. Nyie chezeni tu na Magufuli mtafukuzwa kazi ooho!
 
Sera ya Elim bure inatekelezeka Mkuu, kila kitu ni wakati tu! Usiogope changamoto unazoziona!.Hizo Changamoto ndizo zitatufikisha tunapoenda!. Tutazoe tu, tutakubali,tutaandika changamoto,tutazitatua taratibu na zitatoweka na kuja zenye Sura nyingine Mkuu.
 
Bodi ya shule haipo kwenye muongozo wa malipo,bodi hailipwi chochote kwa mujibu wa sera ya sasa.
Fedha za kujikimu isizidi asilimia 10 kutoka kwenye asilimia 35 fedha za uendeshajiya waweza kulipa wajumbe wa Bodi, kwa uchambuzi wa Mwongozo niliofanikiwa kupata nakala yake, lakini kwa shule inayopata ruzuku mil 2 fedha hii asilimia 10 kutoka kwenye asilima 35 ya mil 2 haifiki hata laki moja. Kama sipo sahihi afisa wa TAMISEMI kama ni members wasaidie ufafanuzi tafadhari walimu wakuu wasifugwe.
 
tusiongopeane hili la elimu bure kwa ccm ni ngumu mno ata wafanyeje hii muvi mpaka mwezi wa 3 star atakua kafa
elimu bure kwa chadema yenyewe ingewezekana au siyo? ?? ingewezekanaje tofauti na hii? ?? tufafanulie basi kidogo ili kutetea hoja yako. bila ushabiki
 
Nilipopata nafasi ya kusoma MA Ed. pale Udsm kuna kozi inaitwa Research Methodology. Mojawapo ya objectives ya ile course ni kumwezesha muhitimu kutoa maamuzi hasahasa ya mambo yahusuyo elimu kwa kuzingatia matokeo na mapendekezo ya research zilizopita ktk swala husika.
Kuna ombwe lazima tukubaliane ktk mfumo wetu Elimu & Siasa za nchi. Hzi pilikapilika za kutafuta dola zitatuathiri sana.
Na sana zaidi hats wataalamu wa hzo research ambao kwenye taasisi za serikali wanaweza walau kuwa na MA au PhD za elimu huku hawatambuliki wala hawafai. Haya tunayoyaona yataendelea tu maana hata ukitaka kutatua tatizo itakupasa ilitambue kwanza tatizo.
 
ELIMU BURE IMEANZA KWA MAFANIKIO MAKUBWA MNO SEMA MIRIJA YA ULAJI YA WAKUU WA SHULE NA BODI IMEKATWA NA NDIO WANAONGOZA KWA KULALAMIKA WEE HUKU WANAFICHAFICHA UKWELI KUWA WIZI WAO UMEBANWA.MALALAMIKO MENGINE MENGI NI YA KIPIMBI TU.
nakuunga mkono kamanda
 
Sera ya Elim bure inatekelezeka Mkuu, kila kitu ni wakati tu! Usiogope changamoto unazoziona!.Hizo Changamoto ndizo zitatufikisha tunapoenda!. Tutazoe tu, tutakubali,tutaandika changamoto,tutazitatua taratibu na zitatoweka na kuja zenye Sura nyingine Mkuu.
Maneno mazuri ya kutia matumaini.
 
Nadhani serikali ilitoa maamuzi ya elimu bure mezani bila kwenda mashuleni na kuwasikiliza wadau gharama za uendeshaji shule zikoje. kama familia ya watu watatu 360,000/= kwa mwezi hazitoshi iweje taasisi ya watu zaidi ya 700?. "HAPA KAZI TU""

Uchaguzi wa Mwaka jana ulikuwa mgumu huko uGambani so walikuwa tayari kuahidi chochote
 
wakuu wa shule baada ya kukatiwa mirija ya ulaji wa pesa z michango ya wazazi kila siku wana kazi ya kulalama tu humu. Nyie chezeni tu na Magufuli mtafukuzwa kazi ooho!
Ukiogopa kufukuzwa kazi usiombe kazi. Ukiogopa kifo cha maji usisafri majini.
 
Kama elimu bure mpaka sekondari haitekelezeki, je elimu bure mpaka chuo kikuu itatekelezeka??
 
Hebu nidadavulie mchanganuo wa utekelezaji wa sera ya elimu bure kupitia UKAWA....samahani...mkuu...

Sera sio mstari wa Biblia ukariri kichwani kama unania kweli yakujua Sera ya Ukawa tafuta Document...zao ukitegemea ziwekwe humu utangoja sana
 
Back
Top Bottom