Mhe.Rc Paul Makonda anapata wapi pesa za matamasha na shughuli kama za kulisha watu wote wa Arusha Nyama Choma?

musicarlito

JF-Expert Member
Dec 29, 2020
457
672
Wasalaam

Bila shaka kama kusingekuwa na makandokando yanayosemwa au kutuhumiwa,pamoja na kauli yetu ya kukiri udhaifu.."binadamu hajakamilika"...lakini basi lau tukachukua katika mizania mtu kama mhe.Antony Mtaka angekuwa anafanya kazi hizi za Makonda...basi Mhe.Paul Makonda ni kiongozi bora sana

Mhe.alioongoza hafla kubwa ya maandamano ya gari za land.rover ikafana sana tuliona mitandaoni

Hatukupoa ikaja siku ya wanawake duniani wakachinjwa ng'ombe 400 tuliambiwa watu walikula nyama mpaka ikakinai

Hatujapoa kuna zoezi kushirikiana na ubalozi wa India wa watu kupata udhamini wa masomo

Haitoshi kuna kliniki za kufuatilia haki za watu kisheria hasa waalimu

Haya ni machache mengi wanayajua wana Arusha wenyewe


Hoja ya msingi...Arusha na wakazi wake wengi bado wana matatizo yale yale yanayo wakumba watanzania wa mikoa mingine kama umasikini...huduma mbovu za afya elimu nk

Hii nguvu kubwa ya matamasha ambayo ni ghali mhe.anaitoa wapi?

Haiwezi kuleta shida baadae katika maslahi ya taifa...ikumbukwe mwalimu Nyerere kwa nia njema kabisa hakufurahia wafanyabiashara kuingia serikalini


Mikoa mingine wanauliza vipi mbona hawafanyiwi kama Arusha?

Kama kuna njia isiyo na mashaka basi mhe.Paul Awe Raisi wa wakuu wa mikoa wafundishe wenzake
 
We mzee izo shida za Afya na elimu umeziona wapi kwa Arusha ulishaskia mwanafunzi Arusha anakaa chini au mjamzito amekosa kitanda?
Ukumbuke pia makonda Hana hata mwaka tangu amefika Arusha huwezi kutegemea kwa hyo miezi ajenge masoko au mabarabara nlikua simkubali makonda lakini ni kiongozi anayefanya kazi kuanzia kwa matajiri na maskini mikoa mingine kama hizo fursa za kwenda India zikija zitagawiwa kwa wachache nyie hamtajua makonda anafika had kwa mtu wa chini fursa ziwe sawa hata huo msaada wa kisheria mikoa mingine uende ofisini wewe ila makonda anawatoa ofsin wakafate wananchi sasa hapo kosa lake nini mnaanza Kuhoji et mbona hajajenga hospital 😂hiyo mikoa mingine wakuu wenu wamewajengea hospital??? Si Bora huyu watu wanapata misaada ya kisheria juzi tena alikua na clinic ya Bure ya afya watu kibao wamesaidiwa
Acheni chuki yeye ajenge hospital na mbunge afanye nini
Hata kama anamapungufu yake binafsi kazi anaipiga na Kubwa anawagusa wananchi wa chini
Mmeshazoea viongozi wanakaa tu ofisini watu wazito ndio anakula nao huyu wadau wakichanga anakula nyamachoma na wananchi wake maskini nyie inawauma nini
Si uchawi huo
 
Back
Top Bottom