Mhe Rais, Ziara za Kushtukiza Imetosha sasa Fanya za Kimkakati

Tanzania tunamipango tena mizuri tu kwa maendeleo yetu, shida ni utendaji wa baadhi ya watumishi waliopo jikoni huko. Uncle John ameenda BOT kutumbua uozo na kuwapanga upya kimkakati ili waende sawa na kasi yake. Tatizo la mtoa mada sijui anapresha inayopelekea kuogopa kufumaniwa na uncle.
Mkuu atanifumania wapi mie mkulima wa nyanya? Huu ni mchango tuu wa mawazo kwa nchi yangu. Au mie sistahili kutoa fikra zangu ila ni nyie tuu Wakurugenzi ndio wenye haki hiyo?
 
Shida ni kwwamba hao wataalamu wakipewa nafasi wangemdanganya Mh.Rais hakuna ambaye angemwambia Rais kuna majina hewa watu wanalipwa......tatizo la wataalam wetu unao wasema mkuu hawana uchungu na nchi yetu.....Mfano tu suala la kuagiza sukari njee ya nchi hili nalo lilikuwa linamsubiri Anko Magufuli? angalia bandari hao wataalamu unaosema bila majaliwa kwenda hayo madudu usingeyajua.......Muhimu tuzidi kumwombea our beloved President......
 
Ni sawa kabisa. Lakini kuna taasisi za kitaalamu zaidi ambazo zinatakiwa kutenda mambo yao kitaaluma na bila woga au unafiki kama BOT. Pale hakuna siasa, na mhe Rais akikutana nao ni kikao cha kina sana na pengine anaweza kuja na mapendekezo ambayo wao kama wataalamu pia wakamkatalia na kumwambia hivyo sio sawa bali tufanye hiki na kile na baada ya majadiliano wakaelewana na mambo yakasonga mbele kwa faida ya nchi.
Hapo ndio pasipo hitaji kushtukizana kama bandarini, unawaambia next week nitakuwa hapo tujadili hali ya kiuchumi na fedha ya nchi. Watu wanaandaa mapendekezo yao kizalendo zaidi na bila woga.
Elewa mkuu, usitegemee kupata wazo la maana kwa mtu ambaye akili yake imejaa woga na mchecheto wa kufukuzwa kazi. Hao wezi na wabadhilifu yeye kama Rais kuwajua sio kosa, akabidhi majina yao kwa vyombo tajwa na washughulikiwe kwa mujibu wa sheria ili yeye apate fursa ya kuwa karibu sana na hawa wataalamu wetu.
Nakubali hoja. 1. Tukumbuke kwamba Rais anapokutembelea kwa kukushtukiza na hata mkuu yeyote, kisaikologia ameanza kukunyonghonyesha. Huwezi kujibizana na rais. Hata kama una majibu sahihi. Rais sio mtu wa kubishiwa. 2. Kutumbua majibu ni muhimu sana. Nadhan taarifa na report zinazofuata baada ya public dismissals ndio waandishi watuletee. Kwa sasa utumbuaji unatufurahisha kwa kuwa wale walioibia jamii tunawaona wakivuliwa nguo hadharani. Je wana hoja za kitaalamu kujitetea baada ya kupewa siku 3 nk kujitetea. 3. JPM yuko vizuri ktk utendaji. Dira ya nchi si majipu tu na kukusanya mapato. Watendaji wafanye wajibu zao. Wakimuachia kila kitu kutoka Dar hadi mikoani basi atahitaji 25 years kutumbua majipu yote Tz. 4. Nchi isiende ki ushabiki, aliyeiba arudishe bali mwenye cha halali asaidiwe apate zaidi. Kwa sasa tukoje hapo?
 
Blaza ziara za kimkakati watafanya mawaziri...yeye anataka safisha na kutoa uhuni katika kazi sa umma,hilo analolifanya ni kubwa na sahihi sana.
Ukitaka kushika mwizi humpi taarifa kwamba unamjia na huwezi kukaa na mwizi eti mjadiliane mikakati na changamoto!!
Hii nchi tushaambiwa na tumeona imechezewa saaqna,na hicho pia ni chanzo kikubwa cha maendeleo duni hapa nchini,Sasa tusiamini sisi tunajua saaana chakufanya kuliko Rais aliyekaa madarakani na kufanya kazibora 20 yrs. Kunawatu (sio mtoamada) hawajawahi hâta kuwa ma monitor darasani lakini wanataka kumfundisha Rais jinsi yakuongoza.
 
Nimeona tena Leo Rais kafanya ziara ya kushtukiza (kama ilivyoripotiwa) katika taasisi nyeti sana nchini nayo ni BOT.
Hapo ndio ambapo anaweza kupata dira na mwelekeo wa hali halisi ya uchumi na nguvu ya taifa kifedha. Hivyo ilikuwa vyema kwa wataalamu wetu pale kuwaandaa kwa ujio wa Rais wa mara ya kwanza ili wajipange na kumueleza kiufasaha nini kinafanyika, changamoto zake, wanahitaji msaada gani toka kwake kama Rais na wamepanga kufanya nini ili uchumi upae na sarafu yetu iwe strong.
Ziara za kushtukiza zimeshajenga picha kuwa ni kukamuana majipu na kufukuzana kazi, na sidhani wataalamu kama utawavamia na kutegemea kupata neno la manufaa kwao kama utapata huku wakiwa na tension kuwa hapa pengine nafukuzwa kazi.
Sasa tembelea maeneo muhimu na ukute wataalamu hata wafanyakazi wa kawaida wakiwa na mood ya kujadiliana nawe nini kifanyike tutoke hapa tulipo hayo ya kuwashtukiza mafisadi,wezi na wabadhilifu achia vyombo vyako vinavyohusika PCCB, POLISI,TISS, nk waendelee lakini chini ya close supervision yako.
Hii itasaidia kuondoa unafiki wa watumishi wakuonapo bali watakupa fact hata za udhaifu wa maamuzi ya serikali na nchi itasonga.
Ukiwa kazini muda wote unatakiwa uwe umejiandaa halafu kama ni mbunifu na unamipango mizuri huhitaji kujiandaa ila kama kunamagumashi kibao ya riport ndio inabidi ujiandae kuchakachua hivyo kwangu Rais aendelee tu kushitukiza uchakachuaji report utaisha.
 
Nimeona tena Leo Rais kafanya ziara ya kushtukiza (kama ilivyoripotiwa) katika taasisi nyeti sana nchini nayo ni BOT.
Hapo ndio ambapo anaweza kupata dira na mwelekeo wa hali halisi ya uchumi na nguvu ya taifa kifedha. Hivyo ilikuwa vyema kwa wataalamu wetu pale kuwaandaa kwa ujio wa Rais wa mara ya kwanza ili wajipange na kumueleza kiufasaha nini kinafanyika, changamoto zake, wanahitaji msaada gani toka kwake kama Rais na wamepanga kufanya nini ili uchumi upae na sarafu yetu iwe strong.
Ziara za kushtukiza zimeshajenga picha kuwa ni kukamuana majipu na kufukuzana kazi, na sidhani wataalamu kama utawavamia na kutegemea kupata neno la manufaa kwao kama utapata huku wakiwa na tension kuwa hapa pengine nafukuzwa kazi.
Sasa tembelea maeneo muhimu na ukute wataalamu hata wafanyakazi wa kawaida wakiwa na mood ya kujadiliana nawe nini kifanyike tutoke hapa tulipo hayo ya kuwashtukiza mafisadi,wezi na wabadhilifu achia vyombo vyako vinavyohusika PCCB, POLISI,TISS, nk waendelee lakini chini ya close supervision yako.
Hii itasaidia kuondoa unafiki wa watumishi wakuonapo bali watakupa fact hata za udhaifu wa maamuzi ya serikali na nchi itasonga.

!
!
Well said mkuu.
Ila Selikali ya Magufuli ni ya Viwanda
 
Mkuu mbona naona inakuwa ngumu kunielewa? Mie sikatai hayo ila BOT mfano, ni taasisi nyeti sana. Hivi Gavana asubuhi yuko ofisini mara anaona Rais huyo mlangoni na anamwanbia niitie wakurugenzi wote tujadili mwelekeo wa nchi ni sawa hiyo? Kazi za kitaalamu zinataka maandalizi ya maelezo ili mjadala wa tija uwepo tofauti na za siasa.
Tusiwazie ubaya tuu kama wizi na ubadhilifu, ndio maana ifike mahali ujio wa Rais uwe faraja kwa watendaji kuwa mawazo yao yatasikilizwa na kufanyiwa kazi badala ya hofu tuu. Hofu ibaki pake vyombo vya dola vitakapo kutembekeeni
ndugu mwalimu hiyo kafanye na wale watoto wa chekechea wanaokujaga kusoma twishen kwako
 
!
!
Well said mkuu.
Ila Selikali ya Magufuli ni ya Viwanda
Unajua watu wamejaa ushabiki tuu, tunaposema kutumbua kuendane na mikakati sijui kwa nini watu hawaelewi. Hivi hivyo viwanda vitatoka ndani ya hayo majipu tukiyakamua? Au ukikamua jipu badala ya kutoka usaha tutapata mazao bora ya kilimo? Viwanda, kilimo, ufugaji miundo mbinu na kadhalika inahitaji MKAKATI ambao ni lazima Rais akae na wataalamu wake kwa kina na kujua nini kifanyike ili kufikia hayo malengo. Au watu wanadhani Magufuli ndio anajibu la yote hayo na wataalamu wao ndio wanapaswa kumsikiliza yeye?
Chuki ni sumu mbaya sana moyoni, tumeibiwa sana na utawala uliopita wa serikali ya ccm hiihii na sumu ya chuki imejaa mioyoni kiasi kwamba hatuoni kingine zaidi ya kukomeshana tuu. Tukomeshe sawa, lakini tu focus mbele zaidi vinginevyo miaka mitano itapita tupo kwenye majipu tuu na hakuna cha kiwanda hata cha pipi, kilimo kitakuwa sio cha tija, miundombinu mipya haitafikiriwa huku jesh la vijana wanaomaliza masomo linaongezeka kwa maelfu na ajira wala fursa za kujiajiri hakuna.
Na badala ya kuwa tumepunguza matatizo ndio yanaongezeka. Tuamke na kuacha mihemko, yeye ajenge vyombo vyake vya usalama na vifanye kazi ipasavyo na hayo majipu yatatumbuliwa tuu huku yeye akiongoza mapambano ya kuleta maendeleo.
Ukimkuta RPC usiku ameshika bunduki yuko kwenye patrol na askari wake wala huwezi kumsifu kama kiongozi bora bali utajua kuna kasoro mahali kwani kwa nini yeye siku zote aongoze mapambano akiwa field?
 
Back
Top Bottom