Mhe. Edward Lowassa Na Familia yake washiriki ibada ya Mwaka Mpya KKKT Monduli

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Taifa Mhe.Edward Lowassa ameshiriki Ibaada Ya Mwaka Mpya Pamoja na Familia yake katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha.

Katika Ibaada hiyo Aliongozana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Kalist Lazaro,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mhe.Isack Joseph,Wakili Msomi John Mallya pamoja na Viongozi wengine.

Pia Mhe.Lowassa aliwatakia Heri ya Mwaka Mpya Watanzania wote na kuwaambia wafanye kazi kwa bidii.
View attachment 452851 View attachment 452853 View attachment 452855
Mbona siku hizi hatoi mapesa mengi makanisani na misikitini?

Sadaka katoa elfu tano tu kwa nini!!
 
Nimefurahi kuona mwanasiasa wa upinzan Edward lowasa akiwataka watz kufanya kazi kwa bidii hili jambo ni la busara ndio maana mm nisiye na chama namuunga mkono yeyote anayetoa kauli za kuijenga nchi yetu. Wanasiasa wengine wanapaswa kuwa na uzalendo kuonesha utaifa kwanza kuliko kugombania madaraka kwa kutoa kauli za kupotosha ama kuhamasisha vurugu kitu ambacho si kizuri kwa ustawi wa uchumi na pia mwisho wa siku wanaoumia ni wananchi wa kawaida wenye vyama na wasio na vyama MEANWHILE wanasiasa wakiendelea kula bata bila bughugha
 
Huyu Mzee angebaki CCM angekufa au saa hizi angekuwa kapararaizi, manake loneliness ingemtesa Sana. Just imagine tangu 2008 CCM walipomwachia zigo la ufisadi ahangaike nalo alone wakati wakati walipiga wote, Na walivyo mdamp kwenye Kura za maoni, Na jinsi JPM asivyotaka utani Na rushwa, saa hizi angekuwa anabaki nyumbani akiamka wanamlundikia magazeti ya kusoma huku anapukuta miwani yake ya kusomea, yaani sipati picha. Anyway nampongeza Sana kwa maamuzi magumu aliyochukua kuhama genge la wala rushwa (ingawa hajasafishika), kuzunguka zunguka na yule tapeli wa hi kwenye ziara za kichama kuendelea kujichanganya Na wananchi, imemsaidia na kumuimalisha zaidi kiafya kutoka kwenye msongo WA Mawazo, pressure, sukari, shock, ...
 
Back
Top Bottom