Mh. Rais, tengeneza mfumo kupitia sheria!

Mh. Rais, moja wapo ya namna nzuri kabisa ya kutengeneza mifumo ni kwa kupitia sheria!
Tuliposema tatizo la nchi hii ni mfumo, mkatukejeli kwamba kinachotakiwa ni mtu hata kama ni dikteta uchwara na kweli tukampata na mkadai nchi itanyooka...je sasa kelele za nini?
Ukawa huwa mnapinga kila kitu! Haha! Hawa jamaa wameamua kua kila kitu wapinge tu!
stroke nikisema wengine wenu ni kama maiti kiakili ingawa mnatembea kweli nitakuwa nimekosea? Leo unataka sheria itungwe, kwani hazipo? Unapata taabu gani kukiri kwamba tatizo la nchi hii ni mfumo? Kwamba kwa mfumo uliopandwa, ukalelewa, ukarutubishwa na ukakomaa na CCM hatufiki?

Naona dawa inaanza kuingia na akili taratibu zinaanza kurudi ila kumbuka, wachagua hovyo wasilalamike hovyo wakianza kutendewa hovyo. Mlilikoroga na sasa linyweni, acheni kulialia, mliyataka na sasa yamekuwa! Mlichagua kama vipofu sasa tulieni mnyolewe bila maji!
 
Mkuu msingi wa kuwa na sheria nzuri unatokana na uwepo wa Katiba nzuri, mimi siyo mwanasheria lakini najua sheria haziwezi kuheshimiwa kama katiba ni mbovu, ndicho kinachotokea hata sasa.
Hata ukiandika nyingine, kuna watu ita wakwaza na wengine watafurahia. mfano ni hii tunayo sasa, wewe una naona haifai wengine wanasema hiyo hiyo inafaa.
 
Good, kuna katiba mpya iliyo kubaliwa na wawakilishi wa wananchi wote kidemokrasia, usubiri ipigiwe kura hiyo. Ukitaka iandikwe nyingine kuliko ilivyo sasa, majibu yatakuwa haya kama ya sasa kwasababu wawakilishi ni wale wale.
 
Ni kweli system itajengwa vizuri kama yatakiwa yanabebwa na sheria. Tatizo ni pale tunapokuwa na kiongozi ambaye haoni tatizo kuvunja sheria ili tu afanikishe mambo yake. Hapo ndipo unakuja umuhimu wa katiba ambayo haimpendelei mtu tofauti na hii ya sasa ambayo Mkulu is practically untouchable
 
Watawala wanaiogopa hii katiba waliyoitengeneza wenyewe. Nadhani ulishawahi kumsikia pogba akisema hana mpango na katiba mpya na wala hakuahidi katiba mpya. Katiba sio kipaumbele kwake.
Who is he?! . Hata akisema katiba sio kipaumbele chake, amechaguliwa sio kwa sababu ya vipaumbele vyake, bali kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo atake asitake, ni kipaumbele chake au sio kipaumbele chake, it doesn't matter much!, as long as Katiba iko kwenye ilani ya CCM, lazima aitekeleze tuu apende asipende kwa sababu ilani ya uchaguzi ya CCM ndio mkataba wa kuchaguliwa kwake, na sio vipaumbele vyake!.

Paskali
 
Mh. Rais kwanza nikupongeze kwa juhudi zako za wazi kabisa za kuinyoosha nchi ambazo sisi wananchi tumeziona na tunaziunga mkono!

Juhudi hizi ni hatua moja kubwa sana kuelekea Tanzania ya maendeleo!

Mh. Rais, ili juhudi hizi zisikome pale utakapomaliza muda wako kama Kiongozi wa Taifa hili, ni vyema ukaandaa mifumo ambayo itapelekea nchi kujiendesha kwa ufanisi bila kutegemea weledi wa yeyote!

Mfumo ambao yeyote anaweza kuwepo lakini bado matokeo yakawa Yale Yale, wengi tunayoyataka!.

Mh. Rais, moja wapo ya namna nzuri kabisa ya kutengeneza mifumo ni kwa kupitia sheria!

Sheria kwa muda mrefu sana imekua nyenzo bora kabisa ya kushape society!

Sheria imesaidia kutatua changamoto nyingi sana over the years!

Kupitia sheria jamii zimekua zikirithishana tamaduni na kanuni mbali mbali!

Mfano , tunataka labda safari za Rais ziwe controlled, itungwe tu sheria ndogo itakayoweka kikomo cha safari za rais kwa mwaka siku na mwezi! Kuwe na utaratibu wa kuhakikisha kua yote hayo yanafanyika.

Kupitia sheria mambo mengi sana yatasuluhishwa na tutakua tumetengeneza system ambayo itakua inajiendesha yenyewe!

Asante kwa kuzingatia haya, na ni imani yangu kwamba, itatokea ikawepo juhudi kuhakikisha kwamba mifumo bora inajengwa kupitia sheria, that will be your legacy sir! Thanks!
Umenena, ndio mmaana wengine walileta Azimio la Arusha na kwa hiyo hawakuwa na shida ya kukimbizana na mabepari kwani walijikuta wanabanana wenyewe na wengine kuamua kuihama nchi.
 
Kumbe hata hujui kua hujui??? Katiba haiwezi beba kila kitu!!!

Ndio maana nasema sheria maana huko hata bylaws zitasaidia! Jifunze then come and argue!
nimefuraahii !! nchi ina katiba itengeneze by- laws? sijui unaelewa unachoandika? na halmashauri watengeneze katiba siyo?
 
Ukawa huwa mnapinga kila kitu! Haha! Hawa jamaa wameamua kua kila kitu wapinge tu!

Wangalau leo umeweka ushabiki pembeni ila ulitakiwa uende kwenye jambo linalotakiwa bila kuzungukazunguka. Sema inatakiwa katiba mpya yenye maoni ya wananchi kutoka ile rasimu ya kina Warioba sio ya yule jamaa aliyefariki juzi.
 
Good, kuna katiba mpya iliyo kubaliwa na wawakilishi wa wananchi wote kidemokrasia, usubiri ipigiwe kura hiyo. Ukitaka iandikwe nyingine kuliko ilivyo sasa, majibu yatakuwa haya kama ya sasa kwasababu wawakilishi ni wale wale.
Uelewa wa watu walikuwepo 2014 siyo sawa na 2017.
 
Uelewa wa watu walikuwepo 2014 siyo sawa na 2017.
Hata kama watu walibadilika kwa asilimi 30, vifugu watakavyo pitisha kuna vingine havita kupendazesha. Nchi nyingi wali dhani katiba ndio muarobani wa shida zao, lakini wakajikuta tatizo lao lipo kwenye kundi la watu fulani katika nchi hiyo na sio katiba. Mfano mzuri ni Kenya, ukabila upo pale pale na katiba mpya ilitakiwa kuyasafisha hayo. Afrika ya kusini, walibadili katiba lakini weusi bado ni masikini na ndio wana maisha magumu kama zamani au zaidi ya zamani. Mifano ni mingi sana Serbia, Iraq, kote huko bado ni matatizo. Lakini wakati huo huo, kuna nchi ambazo zilibadiki katiba na wanaishi vizuri kutokana na kutokuwa na makundi yanayo tete maslahi binafsi. Hapa kwetu kwa hali ilivyo sasa tunayo makundi, kwa hiyo usishangae ukibadili katiba na majibu yakawa haya haya unayo yapata sasa hivi.
 
Mimi sidhani tatizo kubwa la nchi hii ni upungufu wa sheria. Upungufu mkubwa uliopo ni nia ya dhati kusimamia utekelezaji wa sheria hizo kwa haki na bila ubaguzi wa aina yoyote. Tuanze na hilo la usimamizi wa sheria zilizopo kwa dhati kabla ya kutunga sheria yoyote mpya. Tulipoambiwa kuwa vitendo vya ufisadi na rushwa vitatokomezwa kwa njia ya mahakama maalum, baadhi yetu tulishangaa kwa sababu mahakama zilizopo hazipata kushindwa kusikiliza mashauri hayo. Tatizo ni kigugumizi katika kuwafungulia mashtaka wahusika. Na chanzo cha kigugumizi hicho ni kwamba takriban vitendo vyote vya ufisadi vinahusisha wakubwa ambao wakiguswa wengi wataumbuka. Ili haki isitendeke tukaambiwa pia makaburi hayafukuliwi!
 
Nimepatwa na mshtuko wa moyo. Samahani Stroke, kwani ID yako imevamiwa na Ukawa au ni wewe unayeandika post hii? Dadekiii, ngoja tukae mkao wa kula. Mpaka 2020 akili zitakuwa zimeanza kurudi taratibu. shwetani wakubwa kabisa
 
Hata kama watu walibadilika kwa asilimi 30, vifugu watakavyo pitisha kuna vingine havita kupendazesha. Nchi nyingi wali dhani katiba ndio muarobani wa shida zao, lakini wakajikuta tatizo lao lipo kwenye kundi la watu fulani katika nchi hiyo na sio katiba. Mfano mzuri ni Kenya, ukabila upo pale pale na katiba mpya ilitakiwa kuyasafisha hayo. Afrika ya kusini, walibadili katiba lakini weusi bado ni masikini na ndio wana maisha magumu kama zamani au zaidi ya zamani. Mifano ni mingi sana Serbia, Iraq, kote huko bado ni matatizo. Lakini wakati huo huo, kuna nchi ambazo zilibadiki katiba na wanaishi vizuri kutokana na kutokuwa na makundi yanayo tete maslahi binafsi. Hapa kwetu kwa hali ilivyo sasa tunayo makundi, kwa hiyo usishangae ukibadili katiba na majibu yakawa haya haya unayo yapata sasa hivi.
Kwa maoni yako hakuna sababu ya kubadili katiba?
 
Kwa maoni yako hakuna sababu ya kubadili katiba?
Nacho juwa mimi kwamba tunayo katiba mpya tiyari na inacho subiri ni kupigiwa kura ya maoni na wananchi waikubali au waikatae. Wakikata ndio itarudisha kurekebisha ili ipigiwe kura tena. Lakini ukisema tuanze upya kabisa na mchakato mzima wa katiba, tutakuwa kila siku tuna fanya hii michakato isiyo na mwisho.
 
Nacho juwa mimi kwamba tunayo katiba mpya tiyari na inacho subiri ni kupigiwa kura ya maoni na wananchi waikubali au waikatae. Wakikata ndio itarudisha kurekebisha ili ipigiwe kura tena. Lakini ukisema tuanze upya kabisa na mchakato mzima wa katiba, tutakuwa kila siku tuna fanya hii michango isiyo na mwisho.
Hapo nimekusoma
 
Back
Top Bottom