Mh. John S. Malecela atunge kitabu cha historia ya maisha yake

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,773
2,182
Sina hakika kama Mh. John S. Malecela ana mpango wa kutumia muda wake wa kustaafu kutunga kitabu kuhusu maisha yake ya siasa na utumishi wa umma. Hivi karibuni nimemaliza kusoma kitabu kiitwacho "Riding on a Tiger" kilichoandikwa na Mh. Moody Awori aliyekuwa Makmu wa Rais wa Kenya (2002 - 2007) ambaye ameeleza maisha yake ya kisiasa. Ni kitabu kizuri sana. Nilipokuwa nikisoma nikakumbuka kwamba hivi karibuni gazeti la Raia Mwema lilichapisha mahojiano lililofanya na Mh. Malecela ambapo alieleza mambo mengi ya kusisimua. Namshauri Mh. Malecela kama bado hajafikiria kutunga kitabu (autobiography). Ana material mengi. Ushauri huu pia unakwenda kwa viongozi wengine waliostaafu (Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete, Judge Warioba n.k). Wito ni: Viongozi wetu manapostaafu andikeni autobiography zenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…