Mh. Angellah Kairuki waache watumishi wa Umma wapambane na hali zao

Jan 29, 2017
61
66
Katika hali ya kuwakatisha tamaa watumishi wa Umma waliochoka kusikia Matamshi bila vitendo, Leo tena ameibuka Mh. Angellah Kairuki bungeni alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalum Susan Masele, na kusema kuwa nyongeza na upandishaji wa Madaraja kwa Watumishi uliathiriwa na Vyeti feki. Serikali itanza kupandisha madaraja muda wwote kuanzia Sasa.

Mhe. Angellah, Mungu anakuona. Mara ngapi mmetoa matamshi na ahadi tamu kwa watumishi? Je, yalitekelezeka? Majibu nafikiri unayo.

Hapa naomba utambue kuwa watumishi wa Umma sasa wako na nyoyo safi kabsa, walishajituliza kisaikolojia na walishapokea hali zao za kimaisha. Ili kutunza heshima yako tafadhali waacheni watumishi wapambane na hali zao. Walishajua kuwa kuajiriwa ndio chaguo lao, wale mihogo au mkate siagi yote maisha.

Mnapokuja na Matamshi yasio ya vitendo ni kuwasubua na kuharibu afya za kiakili.

Pitia kidogo hapa mwone jinsi watumishi walivyokata tamaa..
sketch-1504617602584.jpg

=#Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni#=

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo wanayofanya hata nchi zingine zinafanya kwa sababu tofauti.. sio la ajabu. Ni kuvuta subira tu.. wangesema hawapandishi au kuongeza hapo ingekuwa ishu kubwa ila sio haya watu kupenda kulalamika tu kama vile wao wanajua linalojiri... mnaboa shaaaaaa wote msio na subira ya kutaka kuona mazuri yanaendelea kutendwa awamu hii.
 
Endelea kuwa mvunilivu mkuu,unajua hii nchi ilikuwa imefika pabaya.Ilifikia kipindi kuna wafanyakazi walikuwa wanapandishwa daraja kila baada ya dakika moja na ni wafanyakazi wale wale tu!!!
 
Huyu waziri naye, majibu yake yalishakuwa yale yale, hata kama ikifika 2018 , atajibu kama alivyojibu leo
 
Hayo wanayofanya hata nchi zingine zinafanya kwa sababu tofauti.. sio la ajabu. Ni kuvuta subira tu.. wangesema hawapandishi au kuongeza hapo ingekuwa ishu kubwa ila sio haya watu kupenda kulalamika tu kama vile wao wanajua linalojiri... mnaboa shaaaaaa wote msio na subira ya kutaka kuona mazuri yanaendelea kutendwa awamu hii.
Ni vema baadhi ya nyuzi kama hizi uwe unapita kimya sababu kubwa ni kwamba akili yako haina akili.
 
Tuvute subira kwani tulipatwa na majanga gani ya dharura?
 
kama hiyo ahadi itatimizwa mwaka huu nitatembea uchi kutoka Kisasa hadi Dodoma mjini.. Mtumishi gani ambae hajui kwamba Seri-kali imefulia mbaya. Hata fedha za uhamisho watumishi hawalipwi
 
Hayo wanayofanya hata nchi zingine zinafanya kwa sababu tofauti.. sio la ajabu. Ni kuvuta subira tu.. wangesema hawapandishi au kuongeza hapo ingekuwa ishu kubwa ila sio haya watu kupenda kulalamika tu kama vile wao wanajua linalojiri... mnaboa shaaaaaa wote msio na subira ya kutaka kuona mazuri yanaendelea kutendwa awamu hii.
Hizo nchi nyingine unaweza kututajia ili nasi tujifunze?
 
Ni vema baadhi ya nyuzi kama hizi uwe unapita kimya sababu kubwa ni kwamba akili yako haina akili.

Ukweli unauma eeeeh.. nimemjibu mwenzio happo post ya kabla.

Utajiju wewe ungekuwa na akili kubwa ungejiongeza na sio kulia lia.. kazi zipo kwingine
 
Huyu waziri ni kati wa wale mh rais aliwaita wapumbavu!anafanya kazi kwa mazoea tuh!hana hoja kabsa!hajiongezi kabsa!
 
Huyu Mama ni Msukule tu masikini hana anachojua zaidi ya kua waziri picha tu ..... Hapo mpaka amuulize PM aseme nini na PM nae hajui nae Anamuuliza Boss wake jibu analojibiwa uko ni acha kieleele....Na Ngoma inaishia apo....Hivyo tumsamehe japo ana akili timamu
 
Back
Top Bottom